bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Amos 1
Amos 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 2 →
1
Maneno ya Amosi aliyekuwa mchunga ng'ombe na kondoo kwao Tekoa; ni mambo yatakayowapata Waisiraeli, naye aliyaona katika siku za Uzia, mfalme wa Yuda, na za Yoroboamu, mwana wa Yoasi, mfalme wa Isiraeli; ilikuwa miaka miwili kabla ya ule mtetemeko wa nchi
2
Alisema: Bwana atanguruma mle Sioni, ataivumisha sauti yake mle Yerusalemu; ndipo, mbuga za wachungaji zitakaposikitika, nao mlima wa Karmeli utakauka juu yake.
3
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kwa ajili ya mapotovu ya Damasko matatu au manne sitayarudisha, yasiwapate, kwa kuwa waliupura Gileadi kwa magari ya chuma ya kupuria.
4
Nitatupa moto nyumbani mwa Hazaeli, uyale majumba ya Benihadadi,
5
nitalivunja komeo la Damasko, nitawang'oa wakaao katika Bonde la Maovu, nitamng'oa naye mshika bakora ya kifalme mle Beti-Edeni; nao watu wa Ushami watatekwa na kuhamishwa kwenda Kiri. Bwana ameyasema.
6
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kwa ajili ya mapotovu ya Gaza matatu au manne sitayarudisha, yasiwapate, kwa kuwa waliwateka wote pia na kuwahamisha, wawapeleke utumwani kwa Waedomu.
7
Nitatupa moto bomani mwa Gaza, uyale majumba yao,
8
nitawang'oa wakaao mle Asdodi, naye mshika bakora ya kifalme mle Askaloni; kisha nitaugeuza mkono wangu, uujie Ekroni, ndipo, Wafilisti waliosalia watakapoangamia. Bwana Mungu ameyasema.
9
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kwa ajili ya mapotovu ya Tiro matatu au manne sitayarudisha, yasiwapate, kwa kuwa wote pia, waliowateka, waliwahamisha na kuwapeleka kwa Waedomu, hawakulikumbuka agano la Kindugu.
10
Nitatupa moto bomani mwa Tiro, uyale majumba yao.
11
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kwa ajili ya mapotovu ya Edomu matatu au manne sitayarudisha, yasiwapate, kwa kuwa waliwakimbiza ndugu zao kwa panga, wakajizuia, wasiwahurumie, kwa kuwa waliendelea siku zote kuwanyafua kwa ukali, hawakomi kuwachafukia kale na kale.
12
Nitatupa moto mle Temani, uyale majumba ya Bosira.
13
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kwa ajili ya mapotovu ya wana wa Amoni matatu au manne sitayarudisha, yasiwapate kwa kuwa waliwatumbua wenye mimba wa Gileadi, wapate kuipanua mipaka yao.
14
Lakini nitawasha moto bomani mwa Raba, uyale majumba yao, wapige makelele, kwa kuwa ni siku ya vita, pawe uvumi, kwa kuwa ni siku ya chamchela.
15
Naye mfalme wao atakwenda kuhamishwa, kwa kuwa atatekwa yeye na wakuu wake. Bwana ameyasema.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9