bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Amos 3
Amos 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 4 →
1
Lisikieni neno hili, Bwana alilolisema kwa ajili yenu, ninyi wana wa Isiraeli, kwa ajili ya huu ukoo wote, nilioutoa katika nchi ya Misri na kuuleta huku: Amesema:
2
Niliwajua ninyi tu katika koo zote zilizoko nchini, kwa hiyo nitawapatilizia ninyi manza zote, mlizozikora.
3
Je? Wako wawili wanaosafiri pamoja, isipokuwa wamepatana?
4
Je? Simba ananguruma mwituni, asipokuwa amepata windo? Je? Mwana wa simba analia pangoni mwake, asipokuwa amekamata?
5
Au ndege anawezaje kuanguka tanzini chini, isipokuwa mtu amelitega? Au tanzi linafyatuka na kuruka juu, lisipokuwa limekamata?
6
Au baragumu la vita likipigwa mjini, watu waliomo mjini hawashikwi na woga? Au yako mabaya mjini, Bwana asiyoyafanya?
7
Kweli Bwana Mungu hafanyi neno, asipokuwa amewafunulia njama yake watumishi wake wafumbuaji.
8
Simba akinguruma, yuko nani asiyeogopa? Bwana Mungu akisema neno, yuko nani asiyetaka kulifumbua?
9
Yatangazeni majumbani mwa Adodi! Namo majumbani mwa nchi ya Misri! Semeni: Kusanyikeni milimani kwa Samaria! Itazameni mivurugo, jinsi inavyozidi katikati yao! Yatazameni nayo makorofi yaliyoko huko kwao!
10
Ndivyo, asemavyo Bwana: Hawakujua kufanya yaliyo sawa wao waliolimbika majumbani mwao makorofi na mapokonyo.
11
Kweli hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Yuko atakayeisonga nchi hii po pote na kuvibwaga chini vilivyokuwa nguvu zako, majumba yako yapate kutekwa.
12
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kama mchungaji anavyoopoa kinywani mwa simba mifupa miwili ya mguu au kipande cha sikio, ndivyo, watakavyojiponya wana wa Isiraeli wakaao sasa Samaria pembeni kitandani juu ya mito ya hariri ya malalo.
13
Yasikieni, myashuhudie nyumbani mwa Yakobo! ndivyo, asemavyo Bwana Mungu aliye Mungu Mwenye vikosi.
14
Kwani siku hiyo, nitakayowapatilizia Waisiraeli mapotovu yao, ndipo, nitakapowapatilizia napo pa kutambikia Beteli, pembe za hiyo meza ya kutambikia zivunjwe, zianguke chini.
15
Ndipo, nitakapozibomoa nyumba za kupupwe pamoja nazo za kiangazi, navyo vyumba vilivyopambwa na pembe za tembo vitaangamia, hizo nyumba nyingi zitakapotoweka; ndivyo, asemavyo Bwana.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9