bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Amos 2
Amos 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 3 →
1
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kwa ajili ya mapotovu ya Moabu matatu au manne sitayarudisha, yasiwapate, kwa kuwa mifupa ya mfalme wa Edomu waliichoma moto, hata ikawa chokaa.
2
Nitatupa moto kwao Moabu, uyale majumba ya Kerioti, nao Wamoabu watakufa katika mvurugo, makelele ya vita na milio ya mabaragumu ikisikilika.
3
Naye mwamuzi nitamng'oa katikati yao, nao wakuu wao wote nitawaua pamoja nao. Bwana ameyasema.
4
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kwa ajili ya mapotovu ya Yuda matatu au manne sitayarudisha, yasiwapate, kwa kuwa wameyakataa Maonyo ya Bwana, wakaacha kuyashika maongozi yake, ikawapoteza miungu yao ya uwongo baba zao waliyoifuata.
5
Nitatupa moto kwao Yuda, uyale majumba ya Yerusalemu.
6
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kwa ajili ya mapotovu ya Isiraeli matatu au manne sitayarudisha, yasiwapate, kwa kuwa wamewauza waongofu kwa fedha, nao maskini kwa viatu viwili.
7
Wanatunukia na kutwetatweta, mavumbi ya nchi yawe vichwani juu yao wakiwa, nazo njia za wanyonge huzipotoa. Mtu na baba yake pamoja humwendea mwanamke mgoni, Jina langu takatifu walipatie uchafu.
8
Hutumia nguo, walizopewa za kuwekea wengine, hujitandikia zizo hizo pote, wanapotambikia; nyumbani mwa miungu yao hunywa mvinyo zao, walizotozwa kuwa malipo ya makosa.
9
Nami ndimi niliyewaangamiza Waamori mbele yao, ndio waliokuwa warefu kama miangati mirefu na wanguvu kama mivule, nikayaangamiza mazao yao ya juu nayo mizizi yao ya chini.
10
Nami ndimi niliyewatoa katika nchi ya Misri na kuwaleta huku, nikawaongoza miaka arobaini nyikani, nikawapa nchi ya Waamori, iwe nchi yenu.
11
Namo miongoni mwa wana wenu nikainua wengine, wawe wafumbuaji, nao wengine nikawachagua katika vijana wenu, wajieue kuwa wangu. Au sivyo vilivyokuwa, ninyi wana wa Isiraeli? ndivyo, asemavyo Bwana.
12
Nao waliojieua mliwanywesha mvinyo, nao wafumbuaji mkawaagiza kwamba: Msifumbue!
13
Mtaniona, nikiwalemea, kama gari linavyolemewa likijaa miganda.
14
Ndipo, mwenye miguu izoeayo mbio atakaposhindwa na kukimbia, naye mwenye nguvu hataweza kutumia hizo nguvu zake kuu, wala fundi wa vita hataiponya roho yake,
15
wala mshika upindi hatasimama, wala mwenye miguu miepesi hatapona, wala mpanda farasi hataiponya roho yake.
16
Naye aushupazaye moyo wake kwa mafundi wa vita siku hiyo atakimbia akiwa uchi; ndivyo, asemavyo Bwana.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9