bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Amos 4
Amos 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 5 →
1
Lisikieni neno hili, ninyi ng'ombe wa Basani! Ninyi mlioko milimani kwa Samaria mkiwakorofisha wanyonge na kuwaponda maskini! Ninyi mnaowaambia bwana zao: Haya! Leteni, tunywe!
2
Bwana Mungu ameapa na kuutaja utukufu wake kwamba: Mtaona, siku zikiwajia ninyi, mtakapovutwa juu kwa kulabu, hata masazo yenu yatavutwa juu kwa ndoana za kuvulia samaki.
3
Mtatoka penye nyufa za ukuta, kila mwanamke mmoja ashike njia yake ya kwenda moja kwa moja, mje kujitupa huko Harmoni; ndivyo, asemavyo Bwana.
4
Haya! Nendeni Beteli, mjikoseshe! Nendeni Gilgali, mzidishe kujikosesha! Katoeni asubuhi vipaji vyenu vya tambiko! Hata kila siku ya tatu yatoeni mafungu yenu ya kumi!
5
Chomeni mikate yenye chachu, iwe shukrani! Tangazeni, visikilike, watu watoe vipaji viwapendezavyo! Kwani ndivyo, mnavyovipenda, ninyi wana wa Isiraeli; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
6
Nami niliwapa meno yakosayo kazi mijini mwenu mote nao ukosefu wa mkate pote, mnapokaa, lakini hamkurudi kwangu; ndivyo, asemavyo Bwana.
7
Tena mimi niliwanyima mvua, miezi mitatu tu ilipokuwa imesalia mpaka mavunoni, mji mmoja nikaunyeshea mvua, tena mwingine sikuunyeshea mvua, shamba moja likanyeshewa na mvua, jingine lisilopata mvua likakauka.
8
Miji miwili mitatu ikatangatanga kuendea mji mmoja tu, ndimo wapate kunywa maji, ijapo wasishibe, lakini hamkurudi kwangu; ndivyo, asemavyo Bwana.
9
Nikawapiga ninyi, nikayaunguza mashamba na kuyakausha kabisa, tena mara nyingi nzige waliyala kwenu mashamba na mizabibu na mikuyu na michekele yenu, lakini hamkurudi kwangu; ndivyo, asemavyo Bwana.
10
Nilituma kwenu magonjwa mabaya, kama nilivyovifanya huko Misri, nikawaua vijana wenu kwa panga, nao farasi wenu wakatekwa. Nikaupandisha mnuko mbaya wa kambi zenu, uingie puani mwenu, lakini hamkurudi kwangu; ndivyo, asemavyo Bwana.
11
Niliwafudikiza wa kwenu, kama Mungu alivyofudikiza Sodomu na Gomora, mkawa kama kijinga kilichopona kwa kuokolewa, kisiteketee chote motoni, lakini hamkurudi kwangu; ndivyo, asemavyo Bwana.
12
Kwa hiyo yako, nitakayokufanyizia Isiraeli; jiweke tayari kukutana na Mungu wako, Isiraeli, kwa ajili yao nitakayokufanyzia!
13
Kwani utamwona atengenezaye milima, aumbaye upepo, amwambiaye mtu ayawazayo moyoni mwake, ni yeye ayageuzaye mapema kuwa giza akipita na kukanyaga juu ya vilima vya nchi; Bwana Mungu Mwenye vikosi ni Jina lake.
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9