bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Amos 6
Amos 6
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 7 →
1
Yatawapata watuliao Sioni nao wajivuniao mlima wa Samaria, ndio wakuu wa taifa lililo la kwanza, nao walio mlango wa Isiraeli huwaendea!
2
Haya! Nendeni Kalne, mkatazame! Tena tokeni huko kwenda Hamati ulio mji mkuu! Kisha shukeni Gati kwa Wafilisti, mwone! Je? Ninyi m wema kuliko watu wa nchi hizo za kifalme? Je? Mipaka yao siyo mikubwa kuliko mipaka yenu?
3
Siku mbaya mnaiwazia kuwa mbali bado, lakini kao la makorofi mnalileta kuwa karibu.
4
Ninyi hulalia vitanda vya pembe za tembo na kujinyosha katika magodoro yenu mororo! Hula wana kondoo mkiwatoa makundini, nao ndama mkiwatoa mazizini!
5
Hujipigia mapango, tena hujitungia vinanda vinginevyo kama Dawidi.
6
Hunywa mvinyo katika mabakuli, tena hujipaka marashi yapitayo yote; lakini hivyo, Yosefu alivyovunjwa, haviwaumizi.
7
Kwa hiyo watatekwa sasa na kuhamishwa, waende mbele ya mateka; ndipo, yatakapokomea makelele ya michezo yao waliojinyosha hivyo.
8
Ndivyo, asemavyo Bwana Mungu Mwenye vikosi: Bwana Mungu ameapa rohoni mwake kwamba: Majivuno ya Yakobo hunitapisha, nikachukizwa na majumba yake, kwa sababu hii nitautoa huo mji pamoja nayo yote yaliyomo mwake.
9
Itakuwa, waume kumi watakaposazwa katika nyumba moja, watakufa.
10
Ndugu ya mtu apaswaye na kumteketeza mwenziwe akimchukua, aitoe mifupa yake nyumbani, kama anamwuliza aliomo nyumbani ndani: Yumo, uliye naye humu? atamjibu: Wamekwisha kufa! Ndipo, atakapomwambia: Nyamaza kimya! Kwani haifai kulikumbusha Jina la Bwana.
11
Kwani mtaona: Bwana akiagiza, ndipo, watakapozipiga nyumba kubwa, hata zibomoke, nazo nyumba ndogo, hata ziatuke nyufa.
12
Je? Farasi hupiga mbio mwambani? Au mtu atapalima na ng'ombe? Kwani mashauri yaliyo sawa mmeyapotoa, yawe maji ya nyongo, nayo yaliyotengenezwa, yaongoke, mmeyapotoa, yawe uchungu.
13
Mwafurahia kisicho kitu na kusema: Hatukujipatia pembe kwa uwezo wetu sisi?
14
Kwa hiyo ndivyo, asemavyo Bwana Mungu Mwenye vikosi: Mtaniona, nikiwainulia taifa ninyi mlio mlango wa Isiraeli; ndio, watakaowasonga ninyi kuanzia penye njia ya kwenda Hamati, kufikisha penye mto wa nyikani.
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 7 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9