bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Amos 9
Amos 9
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
1
Nimemwona Bwana, akisimama penye kutambikia na kusema: Zipige nguzo pembeni juu, vizingiti vya juu vitikisike! Kisha uviponde, viwaangukie vichwani pao wote! nao watakaosalia nitawaua kwa upanga, pasiwe hata mmoja kwao, atakayekimbia, wala mmoja wao atakayepona.
2
Ingawa wapenyelee kuzimuni, huko nako mkono wangu utawatoa; ingawa wapande mbinguni, huko nako nitawabwaga chini.
3
Ingawa wajifiche mlimani kwa Karmeli juu, huko nako nitawakamata na kuwachukua; ingawa wajitoweshe machoni pangu baharini chini kabisa, huko nako nitawaagizia nyoka, awaume.
4
Ingawa waje mbele ya adui zao wakihamishwa kwenda utumwani, huko nako nitawaagizia upanga, uwaue; ndipo, nitakapowaelekezea macho yangu, niwapatie mabaya, nisiwapatie mema.
5
Hapo, Bwana Mungu Mwenye vikosi atakapoigusa nchi, itayeyuka papo hapo, wote wakaao huko waomboleze; ndipo, nchi yote itakapojitutumua kama mto wa Nili, kisha itakupwa kama lile jito la Misri.
6
Ndiye aliyepajenga pake mbinguni kuwa dari yake, nayo misingi ya kao lake aliiweka chini; ndiye anayeyaita maji ya baharini, ayafurikishe juu ya nchi kavu. Bwana ni Jina lake!
7
Ndivyo, yeye Bwana asemavyo: Ham sawasawa kama wana wa Kinubi, ninyi wana wa Isiraeli? Waisiraeli sikuwatoa katika nchi ya Misri? Nao Wafilisti kule Kafutori? Nao Washami kule Kiri?
8
Mtaona, macho yangu Bwana Mungu yakiutazama ufalme uliokosa niutoweshe juu ya nchi, lakini sitautowesha mlango wa Yakobo wote mzima; ndivyo, asemavyo Bwana.
9
Kwani mtaona, nikitoa amri, niwapepete walio mlango wa Isiraeli na kuwatapanya kwa mataifa yote, kama ngano zinavyopepetwa katika ungo, pasipatikane hata chembe moja itakayoanguka chini.
10
Wakosaji tu wa ukoo wangu watauawa wote kwa panga, ndio waliosema: Mabaya hayatatufikia, wala hayatatupata.
11
Siku hiyo ndipo, nitakapokisimamisha kibanda cha Dawidi kilichoanguka, na kuziziba nyufa zake na kuyasimamisha mabomoko yake, nikijenge, kiwe kama siku za kale,
12
wayatwae masao ya Edomu na wamizimu wote waliotangaziwa Jina langu; ndivyo, asemavyo Bwana, naye atayafanya haya.
13
Ndivyo, asemavyo Bwana: Mtaona, siku zikija, mwenye kulima atakaposhikamana na mvunaji, vile vile mwenye kuzikamua zabibu na mpanda mbegu. Ndipo, milima itakapochuruzika pombe mbichi, vilima vyote vifurikwe nazo.
14
Ndipo, nitakapoyafungua mafungo yao walio ukoo wangu wa Isiraeli, waijenge miji yao iliyoangamizwa, waipande mizabibu yao, wapate kunywa mvinyo zao.
15
Ndipo, nitakapowapanda katika nchi yao, wasing'olewe tena katika nchi yao, niliyowapa. Bwana Mungu wako ameyasema.
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9