bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Amos 5
Amos 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 6 →
1
Lisikieni neno hili, ninalowatolea mimi! Ni ombolezo la kuwaombolezea ninyi mlio mlango wa Isiraeli:
2
Ameanguka, hatainuka tena mwanamwali wa Isiraeli, amebwagwa, alale juu ya nchi yake, hakuna atakayemwinua.
3
Kwani hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Mji unaopeleka elfu vitani utasaza mia tu, nao unaopeleka mia utasaza kumi tu kwao walio mlango wa Isiraeli.
4
Kwani hivi ndivyo, Bwana anavyowaambia walio mlango wa Isiraeli: Nitafuteni! Ndipo, mtakapopona.
5
Lakini msinitafute huko Beteli! Wala msije kuingia Gilgali! Wala msiondoke kwenda Beri-Seba! Kwani Gilgali utatekwa na kuhamishwa, nao Beteli utageuka kuwa si kitu.
6
Mtafuteni Bwana! Ndipo, mtakapopona. Asiujie mlango wa Yosefu kama moto utakaouteketeza, kwa kuwa Beteli hakuna atakayeweza kuuzima.
7
Mashauri yapasayo mnayageuza kuwa uchungu, nayo yaongokayo mnayakanyaga uvumbini.
8
Yeye ndiye aliyezifanya nyota, zile za Kilimia nazo zake Choma, nikuchome! Yeye ndiye anayeigeuza giza kuwa mapema, tena mwanga wa mchana huugeuza kuwa giza ya usiku! Yeye ndiye anayeyaita maji ya bahari, akayafurikisha juu ya nchi! Bwana ni Jina lake.
9
Yeye ndiye anayewaletea wanguvu mwangamizo, uwatokee kama umeme, nayo miji yenye maboma ya nguvu iingiliwe na mwangamizo.
10
Wao humchukia ayakataye mashauri ya langoni sawasawa, naye asemaye ya kweli huwachafua mioyo.
11
Kwa kuwa mnamkanyaga mnyonge, mkamtoza kodi ya ngano, mmepata kujijengea nyumba za mawe ya kuchonga, lakini hamtakaa ndani yao; mkajipandia mashamba mazuri ya mizabibu, lakini hamtazinywa mvinyo zao.
12
Kwani ninayajua mapotovu yenu yaliyo mengi nayo makosa yenu yanayozidi. Mnamsonga aliye mwongofu mkitaka kupenyezewa, mkawapotoa maskini, wasishinde shaurini.
13
Kwa hiyo aliye mwenye akili hunyamaza siku hizi, kwani siku hizi ni mbaya kweli.
14
Yatafuteni yaliyo mema mkiyaacha yaliyo mabaya, mpate kupona! Ndipo, Bwana Mungu Mwenye vikosi atakapokuwa nanyi, kama mlivyosema wenyewe.
15
Yachukieni yaliyo mabaya! Yapendeni yaliyo mema! Simamisheni langoni mashauri yaliyo sawa! Ndipo, Bwana Mungu Mwenye vikosi atakapowahurumia walio masao yake Yosefu.
16
Kweli Bwana Mungu Mwenye vikosi, yeye Bwana anasema hivi: Katika viwanja vyote yatakuwako maombolezo, napo barabarani po pote watalia kwamba: Hoi! Hoi! Mkulima watamwita shambani, aje kuingia matanga, nao wajuao maombolezo watawaita, waje kuwalilia.
17
Katika mashamba yote ya mizabibu yatakuwako maombolezo, kwani nitapita kwako katikati; ndivyo, Bwana anavyosema.
18
Yatawapata wanaoitamani siku ya Bwana! Ninyi siku ya Bwana itawafaliaje? Ndiyo giza, siyo mwanga.
19
Itakuwa, kama mtu akimkimbia simba, akaja kukutana na chui, au kama mtu akiingia nyumbani, akauegemeza mkono wake ukutani, kisha akatokea nyoka, akamwuma.
20
Je? Siku ya Bwana siyo giza? Ndio, haina mwanga; ni yenye weusi, hauangazi kabisa.
21
nimechukizwa na sikukuu zenu, sizitaki; wala mnuko wa mikutano yenu ya kunitambikia usinijie!
22
Ingawa mnitolee ng'ombe za kuteketezwa nzima pamoja na vipaji vyenu vya tambiko, sitapendezwa, wala vinono vyenu vya kunishukuru sitavitazama.
23
Iondoe kwangu milio ya nyimbo zako! Nazo sauti za mapango yako sitaki kuzisikia.
24
Lakini mashauri yaliyo sawa na yaendelee kama maji, nayo yaongokayo na yawe kama mto usiokupwa!
25
Je? Ng'ombe na vipaji, mlivyovitoa nyikani miaka arobaini, vilikuwa vya kunitambikia mimi, ninyi mlio mlango wa Isiraeli?
26
Kwa kuwa mlimchukua Sikuti, awe mfalme wenu, navyo vinyua vyenu vya Kiyuni, mlivyojifanyizia wenyewe, viwe nyota zake mungu wenu:
27
basi, kwa hiyo nitawahimisha, mwende mbali kuliko Damasko. Ndivyo, Bwana anavyosema; Mungu Mwenye vikosi ni Jina lake.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9