bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Amos 7
Amos 7
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 8 →
1
Haya ndiyo maono, Bwana Mungu aliyonionyesha: Nimemwona, alivyotengeneza nzige hapo, mimea ya vuli ilipoanza kuchipuka; nayo ilikuwa ya majani ya vuli iliyochipuka, watu walipokwisha kumkatia mfalme majani ya ng'ombe.
2
Ikawa, nzige walipokwisha kula majani ya nchi, nikasema: Bwana Mungu, waachilie! Yakobo atawezaje kusimama? Kwani yeye ni mdogo.
3
Ndipo, Bwana Mungu alipoigeuza roho kwa ajili ya hayo naye Bwana akasema: Hayatakuwa.
4
Hili ndilo ono, Bwana Mungu alilonionyesha: Nimeona, Bwana Mungu alivyouita moto kuja kumgombea. Nao ukala vilindi vikubwa vya maji, ukataka kula napo pa kulimia.
5
Ndipo, niliposema: Bwana Mungu, acha hapo! Yakobo atawezaje kusimama? Kwani yeye ni mdogo.
6
Ndipo, Bwana alipoigeuza roho kwa ajili ya hayo, naye Bwana Mungu akasema: Haya nayo hayatakuwa.
7
Hili ndilo ono, alilonionyesha: Nimemwona Bwana Mungu, alivyosimama juu ya ukuta uliosimama sawasawa kwa kujengwa kwa kipimo cha timazi, naye alishika kipimo cha timazi mkononi mwake.
8
Bwana akaniuliza: Unaona nini, Amosi? Nilipojibu: Kipimo cha timazi, Bwana akaniambia: Utaniona, nitakavyowapima walio ukoo wangu wa Isiraeli, sitaendelea tena kuwapita tu.
9
Vilima vya Isaka vitaangamizwa, napo patakatifu pote pa Isiraeli patabomolewa, nami nitawainukia walio mlango wa Yoroboamu kwa upanga.
10
Ndipo, Amasia, mtambikaji wa Beteli, alipotuma kwa Yoroboamu, mfalme wa Isiraeli, kumwambia: Amosi anakuvurugia watu humu katika mlango wa Isiraeli, nchi haiwezi tena kuyavumilia maneno yake yote.
11
Kwani haya ndiyo, Amosi anayoyasema: Yoroboamu atakufa kwa upanga, nao Waisiraeli watatekwa na kuhamishwa, watoke katika nchi yao.
12
Kisha Amasia akamwambia Amosi: Wewe mchunguzaji, nenda zako kukimbia katika nchi ya Yuda, ukajilie mkate huko na kuwafumbulia maneno!
13
Lakini huku Beteli usitufumbulie tena maneno, kwani hapa ndipo patakatifu pa mfalme, nayo nyumba hii ni ya ufalme wote.
14
Amosi akamjibu Amasia na kumwambia: Mimi si mfumbuaji wala mwana wa mfumbuaji, kwani nalikuwa mchunga ng'ombe, nikajitunzia mikuyu.
15
Ndipo, Bwana aliponichukua, akanitoa penye ng'ombe, Bwana akaniambia: Nenda, uwafumbulie walio ukoo wangu wa Isiraeli!
16
Sasa lisikie neno la Bwana! Wewe unasema: Usiwafumbulie Waisiraeli! Wala usiwahubiri walio mlango wa Isaka yatakayokuwa!
17
Ni kwa sababu hii, Bwana akisema hivyo: Mkeo atakuwa mgoni humu mjini, nao wanao wa kiume na wa kike watauawa kwa upanga, nalo fungu lako la nchi litagawanywa kwa kupimwa na kamba. Nawe wewe utakufa katika nchi iliyo na mwiko wa kuikaa, nao Waisiraeli watatekwa na kuhamishwa, watoke katika nchi yao.
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9