bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ecclesiastes 1
Ecclesiastes 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 2 →
1
Haya ni maneno ya Mpiga mbiu, mwana wa Dawidi, mfalme wa Yerusalemu.
2
Mpiga mbiu asema: Yote ni ya bure kabisa, kweli yote ni ya bure kabisa, yote pia ni ya bure.
3
Mtu hupata nini kwa masumbuko yake yote, anayojisumbua chini ya jua?
4
Kizazi kimoja kikienda zake, kingine huja, lakini nchi hukaa kale na kale.
5
Jua hucha, tena huchwa, kisha hupakimbilia pake pa macheo yake.
6
Upepo ukienda kusini, kisha hugeuka kwenda kaskazini; ndivyo, upepo unavyojiendea na kugeukageuka. Kwa kugeukageuka kwake upepo hurudia hapo, ulipotokea.
7
Mito yote huenda baharini, lakini bahari haijai; papo hapo, mito inaposhika njia zao, ndipo, inapojiendea na kuishika njia ileile.
8
Mambo yote huchokesha, mtu asiweze kuyasema yote, wala macho hayashibi kwa kuyatazama, wala masikio hayajai kwa kuyasikia.
9
Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako tena, nayo yaliyofanywa ndiyo yatakayofanywa tena; hakuna jipya litakalotokea chini ya jua.
10
Kama litatokea, watu wanalotaka kulisema kwamba: Hili ni jipya kweli, limekwisha kuwako siku za kale kabisa zilizokuwako mbele yetu.
11
Ni hivyo tu, wa kwanza hawakumbukwi, vivyo nao wa nyuma watakaokuwako hawatakumbukwa kwao watakaokuwako nyuma yao.
12
Mimi Mpiga mbiu nilikuwa mfalme wa Isiraeli huko Yerusalemu.
13
Nikajipa moyo, kuyatafuta na kuyapeleleza kwa werevu wa kweli yote pia yanayofanyika chini ya mbingu; ni sumbuko baya, Mungu alilowapa wana wa Adamu kulisumbukia.
14
Nikayatazama yote yanayofanywa chini ya jua, nikayaona yote kuwa ya bure, kuwa kuukimbilia upepo.
15
Yapotokayo hayanyosheki, wala yasiyokuwako hayahesabiki.
16
Naliwaza moyoni mwangu kwamba: Mimi nimejipatia werevu wa kweli mwingi, nikauongeza kuwa mwingi zaidi kuupita wa watu wote waliokuwako mbele yangu Yerusalemu, kweli moyo wangu ulipata werevu wa kweli na juzi mwingi.
17
Lakini nilipojipa moyo kujua, jinsi werevu wa kweli ulivyo, tena kujua, jinsi upumbavu na ujinga ulivyo, ndipo, nilipojua, ya kuwa hayo nayo ni kuukimbilia upepo.
18
Kwani werevu mwingi ulipo, yapo nayo masikitiko mengi, naye aongoezaye ujuzi huongeza nayo maumivu.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12