bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ecclesiastes 12
Ecclesiastes 12
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
1
Mkumbuke Muumbaji wako ukingali kijana bado, siku mbaya zikiwa hazijafika, wala miaka haijakupata bado, unayoisema: Hii sipendezwi nayo!
2
Jua na mchana na mwezi na nyota zikiwa hazijaguiwa bado na giza, mawingu mengine yakitokea, mvua ikiisha kupita:
3
siku hizo walinda nyumba watatetemeka, nao waume wenye nguvu watapindika, nao wanawake wasagao watakomesha kazi kwa kuwa wachache, nao wake waliochungulia madirishani wataguiwa na giza.
4
Nayo milango ielekeayo njiani itafungwa, nacho kishindo cha mawe ya kusagia kitakuwa kidogo; ndipo, watu watakapoamka, jogoo akiwika, nao waimbaji wote wa kike watazipunguza sauti zao.
5
Ndipo, watu watakapoogopa kupanda juu, nako njiani wataona mastusho; ni siku zile, mlozi unapochanua maua, mapanzi wasipoweza kuruka kwa kushiba, nacho kiungo cha pilipili kisipofaa kitu; kwani hapo mtu huiendea nyumba yake, atakamokaa kale na kale, nao waombolezaji humjia mara kwa mara.
6
Kwani siku ziko karibu, kamba ya fedha itakapokatika, chano cha dhahabu kitakapopondeka, mtungi utakapovunjika kisimani, gurudumu la kutekea maji litakapokatika na kuangukia mlemle shimoni.
7
Ndipo, nalo vumbi litakaporudi mchangani, lilikokuwa, nayo roho itarudi kwake Mungu aliyeitoa.
8
Mpiga mbiu asema: Yote ni ya bure kabisa, yote pia ni ya bure.
9
Jingine ni hili: huyu mpiga mbiu hakuwa mwerevu wa kweli yeye tu, ila nao watu aliwafundisha ujuzi, akawa mwenye mawazo makuu ya kuchunguza mambo, akatunga mafumbo mengi.
10
Yeye mpiga mbiu alitafuta, aone maneno yapendezayo; nayo maneno yaliyokuwa ya kweli, yaliyoongoka, yakaandikwa.
11
Maneno ya werevu wa kweli ni kama fimbo za wachungaji au kama misumari iliyopigiliwa vema; wenye kuyakusanya waliyapata kwa mchungaji mmoja.
12
Jingine lililoko ni hili: onyeka, mwanangu, usijitie katika kazi hiyo! Kutengeneza vitabu ni kwingi mno, hakukomi, nako kujifunza mengi huchokesha mwili.
13
Na tusikie neno linaloyachanganya yote: Mche Mungu na kuyaangalia maagizo yake! Kwani hivi ndivyo vinavyompasa kila mtu.
14
Kwani matendo yote Mungu atayatakia shauri, nayo yaliyofichwa, kama ni mema, au kama ni mabaya.
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12