bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ecclesiastes 10
Ecclesiastes 10
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 11 →
1
Mainzi waliokufa huyaozesha kwa kuyachafua mafuta ya mtengeneza manukato, ujinga hufanya makuu kuliko werevu wa kweli na utukufu.
2
Moyo wa mwerevu wa kweli huelekea kuumeni, lakini moyo wa mjinga huelekea kushotoni.
3
Napo njiani po pote, mjinga anapokwenda, hupotelewa na akili, hivyo hujitokeza kwao wote kuwa mjinga.
4
Roho ya mtawalaji ikikuinukia, usiondoke mahali pako, kwani upole hutuliza makosa makubwa.
5
Yako mabaya, niliyoyaona chini ya jua, ni kama kosa litokalo kwake mwenye ukuu:
6
ni mjinga akitukuzwa sana, nao wenye mali wakikaa na kunyenyekezwa.
7
Nikaona nao watumishi wanaopanda farasi, wakuu wakienda na kukanyaga nchi kama watumishi.
8
Achimbaye mwina hutumbukia humo, naye abomoaye boma huumwa na nyoka.
9
Avunjaye mawe huumizwa nayo, naye achanjaye kuni hujiponza papo hapo.
10
Chuma kikiwa kimedugika, naye mwenyewe hakinoi, kipate makali, hana budi kutumia nguvu zaidi; hapo napo werevu wa kweli hufaa kwa kufanikiwa.
11
Nyoka akiuma mtu, akiwa hajatabanwa, bado, basi, mwenye kutabana hanacho, anachokipata.
12
Maneno ya kinywa chake mwerevu wa kweli hupendeza, lakini midomo ya mjinga hummeza.
13
Mwanzo wa maneno ya kinywa chake ni ujinga, nao mwisho ni kusema upuzi mbaya.
14
Yeye mjinga husema mengi; lakini hakuna mtu ayajuaye yatakayokuwa, tena yuko nani awezaye kumweleza yatakayokuwa nyuma yake?
15
Masumbuko, anayoyasumbuka mjinga, humchokesha, kwa kuwa hajui hata njia ya kwenda mjini.
16
Utaona mabaya, wewe nchi, mfalme wako akiwa kijana, nao wakuu wako wakila na mapema.
17
Utaona mema, wewe nchi, mfalme wako akiwa mwana wa watu wenye macheo, nao wakuu wako wakila hapo panapopasa, wapate nguvu za kiume, wasile kwa kujilewesha.
18
Kwa ajili yao wajengao kwa uvivu kipaa huinama, kwa ulegevu wa mikono nyumba huvuja.
19
Watu hufanya karamu, wapate kucheka, nayo mvinyo huwafurahisha walioko huku nchini, nazo fedha hupata yote.
20
Mfalme usimtukane hata kwa mawazo yako! Wala chumbani mwako, unamolala, usimtukane mwenye mali! Kwani ndege wa angani watayapeleka, uliyoyasema, naye mwenye mabawa atayatangaza hayo maneno.
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 11 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12