bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ecclesiastes 3
Ecclesiastes 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 4 →
1
Kila jambo lina saa yake, kila jambo lipendezalo chini ya mbingu lina wakati wake:
2
Kuzaliwa kuna wakati wake, nako kufa kuna wakati wake; kupanda kuna wakati wake, nako kuyang'oa yaliyopandwa kuna wakati wake.
3
Kuua kuna wakati wake, nako kuponya kuna wakati wake; kubomoa kuna wakati wake, nako kujenga kuna wakati wake.
4
Kulia kuna wakati wake, nako kucheka kuna wakati wake; kuomboleza kua wakati wake, nako kucheza kuna wakati wake.
5
Kutupa mawe kuna wakati wake, nako kukusanya mawe kuna wakati wake; kukumbatiana kuna wakati wake, nako kukataa kukumbatiana kuna wakati wake.
6
Kutafuta kuna wakati wake, nako kupoteza kuna wakati wake; kuweka kuna wakati wake, nako kutupa kuna wakati wake.
7
Kurarua kuna wakati wake, nako kushona kuna wakati wake; kunyamaza kimya kuna wakati wake, nako kusema kuna wakati wake.
8
Kupendana kuna wakati wake, nako kuchukiana kuna wakati wake; kupigana kuna wakati wake, nako kutengemana kuna wakati wake.
9
Afanyaye kazi analo pato gani kwa kusumbuka kwake?
10
Nikautazama utumishi, Mungu aliowapa wana wa Adamu kuutumikia.
11
Yote aliyafanya kuwa mazuri wakati wao, akawapa kuziwaza mioyoni mwao nazo siku zijazo; ni hiyo tu, asiyowapa: mtu asiione maana ya kazi, Mungu aliyoifanya toka mwanzo hata mwisho.
12
Ndipo, nilipojua, ya kuwa hakuna lililo jema kwao kuliko kufurahi na kufanya mema siku zao za kuwapo.
13
Haya nayo nikayajua, ya kuwa kwake kila mtu apataye kula na kunywa na kuona mema kwa masumbuko yake, hiki nacho ni kipaji cha Mungu.
14
Nikajua, ya kuwa yote, Mungu ayafanyayo, hukaa kale na kale; hapo hapana kuongeza wala kupunguza, kwani Mungu aliyafanya kuwa hivyo, watu wamwogope.
15
Yaliyoko yalikuwako kale, nayo yatakaokuwako yalikuwako kale. Naye Mungu huyazusha yaliyopitishwa.
16
Tena niliona, ya kuwa chini ya jua uko upotovu penye mashauri yanyokayo, napo penye wongofu uko upotovu.
17
Ndipo, niliposema moyoni mwangu: Mungu atamhukumu mwongofu pamoja na mpotovu, kwani kila jambo lipendezalo aliliwekea wakati wake, hata matendo yote.
18
Nikasema moyoni mwangu; Ni kwa ajili ya wana wa Adamu, Mungu akitaka kuwajaribu, waone, ya kuwa wao na nyama ni sawa.
19
Kwani jambo la mwisho linalowapata wana wa Adamu nalo jambo la mwisho linalowapata nyama ni jambo lilo hilo moja; kama huyu anavyokufa, ndivyo, yule naye anavyokufa, pumzi yao wote ni moja tu. Kwa hiyo haliko, mtu analompita nyama, kwani yote ni ya bure.
20
Wote pia hupaendea mahali pale pamoja: wote walitoka uvumbini, tena wote hurudi uvumbini.
21
Yuko nani ajuaye, kama roho za wana wa Adamu hupaa juu? au kama roho za nyama hushuka chini kuzimuni?
22
Ndivyo, nilivyoona, ya kuwa hakuna mema, mtu ayapatayo kuliko kuzifurahia kazi zake, kwani hili ndilo fungu lake yeye. Kwani yuko nani atakayempeleka mahali, atakapoyaona.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12