bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ecclesiastes 4
Ecclesiastes 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 5 →
1
Nilipoyatazama tena makorofi yanayofanywa chini ya jua, niliona machozi yao waliokorofishwa, lakini sikuona aliyewatuliza mioyo; namo mikononi mwao waliowakorofisha zimo nguvu, kwa hiyo kwao hakuna atakayewatuliza mioyo.
2
Kwa sababu hii nikawawazia wafu waliokufa kale kuwa wenye shangwe kuliko wao wanaoishi bado wenye maisha.
3
Lakini niliyemwazia kuwa amepata mema kuliko wao wote wawili, ni yule asiyepata bado kuzaliwa, kwa kuwa hakuyaona hayo matendo mabaya yanayofanywa chini ya jua.
4
Tena niliona, ya kuwa masumbuko yote na kufanikiwa kote katika kazi hutoka katika wivu, mtu anaomwonea mwenziwe; hayo nayo ni ya bure na kuukimbilia upepo.
5
Mjinga hukaa na kuifunga mikono yake; basi, hujila mwenyewe.
6
Kiganja kimoja kikijaa matulivu ni vema kuliko magao yote mawili yakijaa masumbufu ya kuukimbilia upepo.
7
Nikatazama na mengine yaliyo ya bure chini ya jua:
8
kama mtu yuko peke yake pasipo mwenziwe wa pili wala mwana wala ndugu, hakomi kabisa kujisumbua, wala jicho lake halishibi kuzitazama mali, naye husema: Mimi ninamsumbukia nani na kujinyima mwenyewe mema yote? Basi, hayo nayo ni ya bure na utumishi mbaya.
9
Kuwa wawili kunafaa kuliko kuwa mmoja tu, kwa kuwa hao hupata mshahara mwema wa masumbuko yao.
10
Kwani wakianguka, mmoja humwinua mwenziwe lakini mtu aliye peke yake akianguka, ni vibaya, maana hana mwenziwe wa kumwinua.
11
Tena wawili wakilala pamoja hutiana jasho; lakini aliye peke yake atawezaje kupata jasho?
12
Tena aliye peke yake mtu humshinda, lakini wawili wataweza kusimama mbele yake. Nayo kamba yenye nyuzi tatu haikatiki upesi.
13
Kijana mkiwa mwenye werevu wa kweli ni mwema kuliko mfalme mzee, akiwa mjinga asiyejua kuonyeka tena.
14
Kwani itakuwa, yule atoke kifungoni, apate ufalme, naye aliyezaliwa katika ufalme wake awe mkiwa.
15
Nikawaona wote walioishi na kutembea chini ya jua, wakirudi upande wa huyo kijana wa pili aliyesimama mahali pake yule.
16
Nao watu wote, aliowaongoza wote pia, hawakuhesabika. Lakini watakaokuwako nyuma yake hawatamfurahia. Kwa hiyo nayo yalikuwa ya bure na kuukimbilia upepo.
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12