bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ecclesiastes 5
Ecclesiastes 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 6 →
1
Iangalie miguu yako ukienda Nyumbani mwa Mungu, uje kusikia! Hii inafaa kuliko vipaji vya tambiko, wajinga wanavyovitoa, kwani wao hawajui, ya kuwa hufanya mabaya.
2
Usibabaike tu kwa kinywa chako, wala moyo wako usiwe mwepesi wa kutoa maneno mbele ya Mungu! Kwani Mungu yuko mbinguni, wewe nawe uko huku nchini, kwa hiyo maneno yako sharti yawe machache.
3
Kwani ndoto huja kwa kutumikia mengi, nayo sauti ya mjinga kujulika kwa kusema maneno mengi.
4
Kama umemwapia Mungu kiapo cho chote, usikawe kukilipa! Kwani hapendezwi na wajinga; cho chote, ulichokiapa, kilipe!
5
Ukiwa hukuapa, ni vema, kuliko ukiwa hukilipi, ulichokiapa.
6
Usiache, kinywa chako kiukoseshe mwili wako, wala usimwambie malaika: Hili ni kosa tu! Unataka kwa nini, Mungu ayakasirikie, uliyoyasema, kisha aziangamize kazi za mikono yako?
7
Kwani ndoto zikiwa nyingi, nayo maneno yakiwa mengi, mengi ni ya bure; kwa hiyo umwogope Mungu!
8
Ukiona, maskini akikorofishwa, tena mashauri yaliyo sawa nayo mambo yaongokayo yakiondolewa mjini kwa nguvu, usivistaajabu, vikifanyika hivyo! Kwani aliye mkuu yuko na mkuu kumpita amwangaliaye, tena juu yao wote yuko aliye mkuu mwenyewe.
9
Kwa ajili ya hayo yote inafaa, nchi ikiwa na mfalme ayatazamaye mashamba, yalimwe.
10
Apendaye fedha hashibi fedha, wala apendaye mali hatoshewi na mapato. Hayo nayo ni ya bure.
11
Mema yakiwa mengi, basi, nao watakao kuyala huwa wengi; naye mwenyewe hupata nini, isipokuwa hii tu, macho yake yakiyatazama kwa kufurahi.
12
Usingizi wa mtu wa kazi ni mtamu, kama anakula vichache au vingi; lakini shibe za mkwasi hazimpatii mapumziko ya kulala usingizi.
13
Uko ubaya unaouguza, nami nimeuona chini ya jua, ni huu: mali zilizoangaliwa na mwenyewe mwisho zikimpatia mabaya.
14
Mali hizo zikipotea kwa kutumikiwa vibaya, naye akiwa amezaa mtoto, basi, hakuna hata kidogo kitakachokuwa mkononi mwake.
15
Vivyo hivyo, alivyotoka tumboni mwa mama yake mwenye uchi, ndivyo, atakavyokwenda tena, kama alivyokuja, asichukue kwa masumbuko yake cho chote cha kwenda nacho mkononi mwake.
16
Kweli huu ndio ubaya uuguzao. Vivyo hivyo, alivyokuja, ndivyo, atakavyokwenda; tena anapataje kwa kuusumbukia upepo?
17
Naye siku zake zote alizila na kukaa gizani mwenye masikitiko mengi kwa kuugua na kwa kukasirika.
18
Yasikie, niliyoyaona kuwa mema na mazuri! Ni haya: mtu akila, akinywa na kuona mema kwa masumbuko yake, aliyoyasumbuka chini ya jua siku zote za maisha yake, Mungu alizompa, kwani hili ndilo fungu lake.
19
Tena mtu ye yote, Mungu aliyemgawia mali na mema ya dunia hii na kumpa uwezo wa kuyala na kulichukua fungu lake na kuyafurahia masumbuko yake, basi, ajue, ya kuwa hilo ndilo gawio lake Mungu.
20
Kwani huyu hakumbuki kabisa, jinsi siku zake za kuwapo zilivyo, kwani Mungu humwitikia kwa kuufurahisha moyo wake.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12