bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Ecclesiastes 6
Ecclesiastes 6
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 7 →
1
Yako mabaya, niliyoyaona chini ya mbingu, nayo huwalemea watu sana.
2
Mungu akimgawia mtu mali na mema ya dunia hii na macheo, asijinyime lo lote, moyo wake ulitunukialo, lakini Mungu asipompa uwezo wa kuyala, ila mgeni akiyala, basi, yanamwia ya bure, tena humwuguza vibaya.
3
Mtu akizaa watoto mia, miaka ya maisha yake ikawa mingi, siku za miaka yake zikihesabiwa ziwe nyingi kweli, lakini roho yake isipoyashiba hayo mema yake, naye asipate hata kaburi, basi, nasema: Mtoto aliyekufa katika kuzaliwa alipata mema kuliko yeye.
4
Kwani huyo mtoto huja kama si kitu, huenda gizani, nalo jina lake limo gizani.
5
Jua tu hakuliona, wala halijui; lakini hutulia kuliko yule.
6
Kama mtu angepata kuwapo miaka elfu mbili, asione mema, huyu naye haendi mahali pale pamoja, wote wanapokwenda?
7
Masumbuko yote ya mtu ni ya kukijaza kinywa chake, lakini hivyo roho yake haishibi.
8
Kwani yako mapato gani, mwerevu wa kweli anayoyapata, mjinga asiyoyapata? Au yako mapato gani, mnyonge anayoyapata akijua mwenendo ufaao machoni pa watu wanaoishi?
9
Kuyatazama yaliyoko machoni ni kwema kuliko kwenda na kuzifuata tamaa; hayo nayo ni ya bure na kuukimbilia upepo.
10
Yaliyoko yamekwisha kuitwa jina tangu kale, nayo yatakayompata mtu yamekwisha kujulikana kale; hakuna mtu anayeweza kubishana na mwenziwe amshindaye nguvu.
11
Kwani yako mambo mengi yaletayo mengi yaliyo ya bure; hayo mtu yanamfalia nini?
12
Kwani yuko nani ayajuaye yamfaliayo mtu huku nchini siku hizi za kuwapo zinazohesabika, zilizo za bure tu? maana huzila kama kivuli. Yuko nani awezaye kumwelezea mtu yatakayokuwako nyuma yake chini ya jua?
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 7 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12