bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Judges 15
Judges 15
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 16 →
1
Siku zilipopita, siku za mavuno ya ngano zilipokuwa karibu, Samusoni alikwenda kumwamkia mkewe na kumpa mwana mbuzi, akisema moyoni: Nitaingia chumbani kwa mke wangu. Lakini baba yake hakumpa ruhusa kuingia.
2
Baba yake akamwambia: Nilidhani, umechukizwa naye, nikampa mwenzako; je? Ndugu yake mdogo si mwema kuliko yeye? Na awe wako mahali pake!
3
Samusoni akawaambia: Mara hii sitakora manza kwao Wafilisti nikiwafanyizia mabaya.
4
Kisha Samusoni akaenda, akakamata mbweha 300, kisha akachukua mienge yenye moto, akawafunga wawiliwawili mkia kwa mkia, akatia mwenge mmoja katikati ya mikia miwili.
5
Tena alipokwisha kuiwasha moto ile mienge, akawaacha, waende mashambani kwa Wafilisti kwenye ngano; ndivyo, alivyozichoma hizo ngano zilizokwisha kufungwa miganda, nazo zilizokuwa mabuani bado, hata mizabibu na michekele.
6
Wafilisti walipoulizana: Ni nani aliyeyafanya haya? watu wakasema: Ni Samusoni, mkwewe yule mtu wa Timuna, kwa kuwa amemchukua mkewe, akampa mwenzake. Ndipo, Wafilisti walipopanda huko, wakamteketeza kwa moto yule mwanamke pamoja na nyumba ya baba yake.
7
Lakini Samusoni akawaambia: Mkifanya mambo kama hayo, kweli nitajipatia malipizi kwenu, kisha nitaacha.
8
Akawapiga akitumia mguu wa mmoja wa kupigia kiuno cha mwingine, likawa pigo kubwa sana. Kisha akaenda kukaa katika pango la mwamba wa Etamu.
9
Kisha Wafilisti wakapanda, wakapiga makambi katika nchi ya Yuda, wakajieneza huko Lehi.
10
Wayuda walipowauliza: Mmetupandia kwa sababu gani? wakasema: Tumepanda, tumfunge Samusoni, tumfanyizie, kama alivyotufanyizia sisi.
11
Ndipo, waliposhuka watu 3000 toka Yuda kwenda kwenye pango la mwamba wa Etamu, wakamwambia Samusoni: Kumbe hujui, ya kuwa Wafilisti wanatutawala? Mbona unatufanyizia mambo kama hayo? Akawaambia: Kama walivyonifanyizia, ndivyo, nilivyowafanyizia nao.
12
Wakamwambia: Tumekuja, tukufunge, tukutie mikononi mwa Wafilisti. Samusoni akawaambia: Niapieni, ya kuwa hamtanipiga ninyi, mniue!
13
Nao wakamwambia kwamba: Hivyo sivyo, sisi tunataka tu, tukufunge, tukutie mikononi mwao, lakini hatutakuua kabisa. Kisha wakamfunga kwa kamba mbili mpya, wakampandisha kutoka pale mwambani.
14
Yeye alipofika Lehi, Wafilisti wakamawendea njiani na kumzomea. Ndipo, roho ya Bwana ilipomjia kwa nguvu, nazo kamba, ambazo mikono ilifungwa nazo, zikawa kama nyuzi zilizounguzwa na moto, pingu zake nazo zikayeyuka na kuanguka mikononi pake.
15
Alipoona hapo mfupa mbichi wa taya la punda, akapeleka mkono wake, akauchukua, akaua nao watu 1000.
16
Kisha Samusoni akasema: Kwa taya la punda wanalala machungu, huku chungu moja, huko machungu mawili; kwa taya la punda nimewaua watu elfu zima.
17
Alipokwisha kuyasema haya, akautupa huo mfupa wa taya, alioushika mkononi mwake; kwa hiyo watu wakapaita mahali pale Ramati-Lehi (Kilima cha Taya).
18
Kisha akaona kiu kali, ndipo, alipomlilia Bwana akisema: Wokovu huu mkubwa umewapatia hawa kwa mkono wa mtumishi wako; sasa nife kwa kiu, nianguke mikononi mwao hao wasiotahiriwa!
19
Ndipo, Mungu alipopasua shimo lililoko Lehi, mara yakatoka maji humo, naye akanywa, mpaka roho yake ikamrudia, akapata kuwa mzima tena. Kwa hiyo hapo huitwa Chemchemi ya Mliaji, nayo iko huko Lehi hata siku hii ya leo.
20
Akawa mwamwuzi wa Waisiraeli miaka 20 siku zile za Wafilisti.
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 16 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21