bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Judges 2
Judges 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 3 →
1
Ndipo, malaika wa Bwana alipotoka Gilgali, akaja kupanda Bokimu, akasema: Naliwatoa Misri, nikawaleta katika nchi hii, niliyoapa kuwapa baba zenu, nikasema: Agano, nlilolifanya nanyi, sitalivunja kale na kale.
2
Ninyi msifanye maagano na wenyeji wa nchi hii! Ila pabomoeni pao pa kutambikia! Lakini hamkuisikia sauti yangu; maana yao haya, mliyoyafanya, ndio nini?
3
Kwa hiyo nasema nami: Sitawafukuza mbele yenu, wapate kuwasonga mbavuni, nayo miungu yao iwanase kama tanzi.
4
Malaika wa Bwana alipowaambia wana wote wa Isiraeli maneno haya, watu wakazipaza sauti zao, wakalia.
5
Kwa hiyo wakaliita jina la mahali hapo Bokimu (Vilio), kisha wakamtambikia Bwana.
6
Hapo Yosua alipowapa watu wa ukoo huu ruhusa kwenda kwao, wana wa Isiraeli walikwenda kila mtu kwenye fungu lake la nchi, alichukue.
7
Watu wakamtumikia Bwana siku zote, Yosua alizokuwapo, nazo siku zote, walizokuwapo wale wazee waliokaa siku nyingi kuliko Yosua, ndio wale walioyaona matendo makuu yote, Bwana aliyowatendea Waisiraeli.
8
Naye Yosua, mwana wa Nuni, mtumishi wa Bwana, akafa mwenye miaka 110.
9
Wakamzika katika mipaka ya fungu lake huko Timunati-Heresi milimani kwa Efuraimu upande wa kaskazini wa mlima wa Gasi.
10
Watu wote wa kizazi hicho walipokwisha kukusanywa kwenda kwa baba zao, wakaondokea watu wengine wa kizazi kingine wasiomjua Bwana wala matendo, aliyowatendea Waisiraeli.
11
Ndipo, wana wa Isiraeli walipoyafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana kwa kuyatumikia Mabaali.
12
Wakamwacha Bwana Mungu wa baba zo aliyewatoa katika nchi ya Misri, wakafuata miungu mingine miongoni mwao miungu ya makabila yaliyowazunguka, wakaiangukia. Ndivyo, walivyomkasirisha Bwana.
13
Walipomwacha Bwana wakamtumikia Baali, nayo Maastaroti.
14
Kwa hiyo makali ya Bwana yakawawakia waisiraeli, akawatia mikononi mwa wanyang'anyi, wawanyang'anye mali zao, namo mikononi mwa adui zao waliowazunguka, akawauza, wasiweze tena kusimama usoni pao adui zao.
15
Po pote walipotokea, mkono wa Bwana ukawapatia mabaya, kama Bwana alivyowaambia, kama Bwana alivyowaapia; kwa hiyo wakasongeka sana.
16
Ndipo, Bwana alipowainulia waamuzi, wawaokoe mikononi mwao waliowanyang'anya mali zao.
17
Lakini nao waamuzi hawakuwasikia, kwani walivunja maagano kama wagoni waliofuata miungu mingine na kuiangukia; ndivyo, walivyoondoka upesi katika njia, baba zao waliyoishika, ni ile ya kuyasikia maagizo ya Bwana. Hawakuyafanya hayo.
18
Bwana alipowainulia waamuzi, Bwana alikuwa na yule mwamuzi, awaokoe mikononi mwa adui zao siku zote za huyu mwamuzi, kwani Bwana aliwaonea uchugu, walipompigia kite kwa ajili yao waliowatesa na kuwasukumasukuma.
19
Lakini huyo mwamuzi alipokufa, wakafanya tena mabaya kuliko baba zao wakifuata miungu mingine, waitumikie na kuiangukia; hawakuacha kabisa kuyafanya hayo matendo yao na kuishika hiyo njia yao iliyokuwa ngumu sana.
20
Ndipo, makali ya Bwana yalipowawakia Waisiraeli, akasema: Kwa kuwa watu hawa wamelikosea Agano langu, nililowaagiza baba zao, wakikataa kuisikia sauti yangu,
21
mimi nami sitaendelea kufukuza mbele yao watu wa hayo mataifa, Yosua aliowaacha alipokufa.
22
Ila nitawatumia kuwajaribu Waisiraeli, kama wataiangalia njia ya Bwana, waishike, kama baba zao walivyoishika, au kama wataiacha.
23
Kwa hiyo Bwana akayaacha hayo mataifa, wakae, asiwafukuze upesi. Kwa hiyo hakuyatia mikononi mwa Yosua.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21