bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Judges 3
Judges 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 4 →
1
Haya ndiyo mataifa, Bwana aliyoyaacha, wakae, awatumie kuwajaribu Waisiraeli wote wasioyajua mapigano yote ya Kanaani.
2
Huko ni kwamba tu: vizazi vingine vya wana wa Isiraeli wayajue, wapate kujifundisha mapigano, ni wale tu wasioyajua mapigano ya kale.
3
Nayo mataifa ni haya: watawalaji watano wa Wafilisti na Wakanaani wote na Wasidoni na Wahiwi waliokaa milimani kwa Libanoni kutoka kwenye mlima wa Baali-Hermoni mpaka kufika Hamati.
4
Hao ndio, aliowataka wa kuwajaribu Waisiraeli, ajue, kama watayasikia maagizo ya Bwana, aliyowaagiza baba zao kinywani mwa Mose.
5
Ndivyo, wana wa Isiraeli walivyokaa katikati kwao Wakanaani na kwa Wahiti na kwa Waamori na kwa Waperizi na kwa Wahiwi na kwa Wayebusi.
6
Wakawachukua wana wao wa kike, wawe wake zao, nao wana wao wa kike wakawapa wana wao wa kiume, nayo miungu yao wakaitumikia.
7
Wana wa Isiraeli walipoyafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana, wakimsahau Bwana Mungu wao, watumikie vinyago vya Baali na vya Ashera,
8
makali ya Bwana yakawawakia Waisiraeli, akawauza na kuwatia mkononi mwa Kusani-Risataimu, mfalme wa Mesopotamia; nao wana wa Isiraeli wakamtumikia Kusani-Risataimu miaka 8.
9
Wana wa Isiraeli walipomlilia Bwana, Bwana akawainulia wana wa Isiraeli mwokozi, awaokoe, ndiye Otinieli, mwana wa Kenazi, mdogo wake Kalebu.
10
Roho ya Bwana ilipomjia, akawa mwamuzi wa Waisiraeli, akatoka kwenda vitani, naye Bwana akamtia Kusani-Risataimu, mfalme wa Mesopotamia, mkononi mwake, kwa kuwa mkono wake yeye ulikuwa wenye nguvu kuliko ule wa Kusani-Risataimu.
11
Ndipo, nchi ilipopata kutulia miaka 40, kisha Otinieli, mwana wa Kenazi, akafa.
12
Wana wa Isiraeli walipoendelea kuyafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana, Bwana akamtia Egloni, mfalme wa Moabu, nguvu, awashinde Waisiraeli, kwa kuwa waliyafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana.
13
Ndipo, alipokusanya kwake wana wa Amoni na Waamaleki, kisha akaenda, akawapiga Waisiraeli, nao Mji wa Mitende wakauchukua.
14
Kisha Waisiraeli wakamtumikia Egloni, mfalme wa Moabu, miaka 18.
15
Wana wa Isiraeli walipomlilia Bwana, Bwana akawainulia mwokozi, ndiye Ehudu, mwana wa Gera wa Benyamini, ni mtu mwenye shoto. Huyu wana wa Isiraeli wakamtuma kumpelekea Egloni, mflame wa Moabu, mahongo.
16
Ehudu akajipatia upanga wenye ukali pande zote mbili, nao urefu wake kama mkono; akaufunga chini ya nguo yake penye paja lake la kuume.
17
Akampelekea Egloni, mfalme wa Moabu, hayo mahongo, naye Egloni alikuwa mtu mnene sana.
18
Alipokwisha kumpelekea hayo mahongo, akawapa wale watu waliochukua mahongo ruhusa kwenda zao.
19
Lakini mwenyewe akarudia Gilgali, hapo palipokuwa na vinyago, akasema: Nina neno la njama na wewe mfalme; naye akasema: Nyamaza kwanza! Wote waliosimama kwake walipokwisha kutoka,
20
Ehudu akaingia mwake; naye alikuwa amekaa katika chumba cha juu chenye baridi yeye peke yake tu. Ehudu aliposema: Ninalo neno la Mungu la kukuambia, akainuka katika kiti chake cha kifalme.
21
Ndipo, Ehudu alipoupeleka mkono wake wa kushoto, akauchomoa upanga penye paja lake la kuume, akamchoma tumboni;
22
hata kipini kikaingia ndani pamoja na chuma cha upanga, nayo mafuta yakapafungia palipoingia upanga, kwani hakuutoa upanga tumboni, nao ulitokea nyuma.
23
Kisha Ehudu akatoka, akaja barazani, akaifunga milango ya kile chumba cha juu nyuma yake kwa komeo.
24
Alipokwisha kutoka, watumishi wake Egloni wakaja; lakini walipoona, ya kuwa milango ya chumba cha juu imefungwa kwa makomeo, wakasema; Labda amejifunika miguu yake katika chumba cha baridi.
25
Wakangoja kwa kuona soni, lakini walipoona ya kuwa hakuna anayeifungua milango ya chumba, wakachukua ufunguo, wakaifungua, mara wakamwona bwana wao, akilala chini, maana amekufa.
26
Naye Ehudu alikuwa ameponyoka, wale walipokawilia, naye akapapita penye vinyago, akapona kweli alipofika Seira.
27
Alipoingia humo akapiga baragumu milimani kwa Efuraimu; ndipo, wana wa Isiraeli waliposhuka pamoja naye kutoka milimani, naye akawaongoza.
28
Akawaambia: Nifuateni upesi! Kwani Bwana amewatia adui zenu, hawa Wamoabu, mikononi mwenu. Ndipo, waliposhuka na kumfuata, wakavivuka vivuko vya Yordani penye njia za kwenda Moabu, kisha hawakumpa mtu ruhusa kuvuka.
29
Wakati huo wakaua Wamoabu kama watu 10000, wote waliokuwa wanene nao wenye nguvu wote, hakuwako aliyepona.
30
Siku hiyo Wamoabu wakanyenyekezwa kuwa chini ya mikono ya Waisiraeli; ndipo, nchi ilipopata kutulia miaka 80.
31
Aliyemfuata ni Samugari, mwana wa Anati; akaua Wafilisti watu 600 kwa fimbo tu la kuchungia ng'ombe; hivyo yeye naye aliwaokoa Waisiraeli.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21