bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Judges 5
Judges 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 6 →
1
Siku ile Debora na Baraka, mwana wa Abinoamu, wakaimba kwamba:
2
Kwa kuwa walikuwako waliowaongoza Waisiraeli, kwa kuwa nao watu wamejitoa wenyewe, kwa hiyo mtukuzeni aliye Bwana!
3
Sikieni, ninyi wafalme! Sikilizeni, ninyi watawalaji! Mimi, mimi mwenyewe na nimwimbie Bwana, na nimshangilie Bwana Mungu wa Isiraeli!
4
Bwana, ulipotoka Seiri, ulipopita mashambani kwa Edomu, nchi ikatetemeka, mbingu nazo zikanyesha, mawingu nayo yakanyesha mvua.
5
Milima ikatukutika mbele ya Bwana, nao Sinai mbele yake Bwana, Mungu wa Isiraeli alipotokea.
6
Siku za Samugari, mwana wa Anati, barabara zilikuwa zimekufa, hata siku za Yaeli; nao walioshika njia hupitia zile za kupotokapotoka.
7
Kwao Waisiraeli hakukuwa na wakulima, walikuwa wamekoma, walikuwa wamekoma kweli, mpaka wewe, Debora, ulipotokea, nawe ukawatokea Waisiraeli kuwa mama yao.
8
Walikuwa wamejichagulia miungu mipya; lakini vita vilipofika malangoni, haikuwako ngao wala mkuki kwao waume wa Waisiraeli, nao walikuwa maelfu arobaini.
9
Moyo wangu huwaelekea waongozi wa Waisiraeli waliojitoa wenyewe miongoni mwa watu. Mtukuzeni aliye Bwana!
10
Ninyi mpandao punda weupe, nanyi mkaliao mazulia, nanyi mtembeao njiani: yafikirini mioyoni!
11
Wapiga mishale wanapocheza pamoja nao wachota maji, ndipo wayatangaze matendo ya Bwana yaongokayo, hayo matendo yaongokayo ndiyo, aliyowatendea wao waliokuwa wakulima kwao Waisiraeli. Ndipo, watu wa Bwana waliposhuka kufika malangoni.
12
Amka! Amka, Debora! Amka! Amka, uimbe wimbo! Inuka, Baraka, upate kuwateka wanaotaka kukuteka, mwana wa Abinoamu!
13
Ndipo, waliosalia waliposhuka kuwaendea wale watukufu, Bwana naye akashuka kuja kwangu nao hao mafundi wa vita:
14
Efuraimu ndiko, walikotoka waliozaliwa Amaleki, Wabenyamini nao wakakufuata pamoja na watu wako wengi, kwao Wamakiri wakatoka wajuao kuongoza watu, kwao Wazebuluni wakatoka wao walioshika bakora, nazo zilikuwa zao waandaliaji wa vita.
15
Wakuu wa Isakari wakawa naye Debora, tena kama Isakari vilevile naye Baraka, ndiye aliyejihimiza kwa miguu yake kumkimbilia pale bondeni. Lakini kule kwa vijito vya Rubeni kulikuwa na mambo, ndiyo mashauri ya mioyo yaliyo makuu.
16
Mbona unataka kukaa tu mazizini kwa kondoo? Unataka kusikiliza mazomari yanayopigiwa makundi? Kweli vijitoni kwa Rubeni yako mashauri makuu ya mioyoni!
17
Wagileadi wakasalia ng'ambo ya Yordani, mbona Wadani nao hukaa ugenini kwenye merikebu? Waaseri nao hukaa tu pwani kwenye bahari, kweli huwa kimya katika bandari zao.
18
Lakini Wazebuluni ni watu wasiojiangalia kufani, Wanafutali nao ndivyo, walivyo kwao mashambani vilimani.
19
Wafalme wakaja kufika huku, wapige vita; wafalme wa Kanaani ndio waliovipiga kule Taanaki kwenye maji ya Megido, lakini nyara, ijapo ziwe za fedha kidogo tu, hawakuzipata kabisa.
20
Toka mbinguni wametupigania, nyota zilipokuja, zikaziacha njia zao kwa kupigana na Sisera.
21
Kijito cha Kisoni kikawaporomosha, hicho kijito cha Kisoni kilicho kijito cha kale; roho yangu nawe, wakanyage kwa nguvu!
22
Ndipo, zilipopiga shindo kwa kukimbia kwato za farasi, wanguvu waliowapanda walipowakimbiza.
23
Ndivyo, asemavyo malaika wa Bwana: Uapizeni Merozi! Waapizeni! Waapizeni wao wenyeji wake! Kwani hawakufika kusaidiana na Bwana, hawakusaidiana na Bwana kwao walio mafundi wa vita.
24
Yaeli ndiye atakayetukuzwa kuliko wenzake, mkewe Mkeni Heberi ndiye, watakayemsema mahemani, apate kutukuzwa zaidi kuliko wenzake.
25
Alipomwomba maji, akampa maziwa, akampelekea mafuta ya maziwa katika chombo kitukufu.
26
Akaukunjua mkono wake kuchukua uwambo, nao mkono wake wa kuume ukashika nyundo ya wahunzi, akakivunja kichwa chake Sisera na kukipiga nyundo, akakiponda na kulitoboa paji lake.
27
Miguuni pake akaanguka magotini, kisha akalala, kweli akaanguka magotini miguuni pake; alipopiga magoti, ndipo, alipoanguka, akawa mfu.
28
Anachungulia dirishani na kulia kwa sauti kuu, mamake Sisera anachungulia katika vyuma vya dirisha: Mbona gari lake limechelewa kuja? Mbona magurudumu ya magari yake yanakawia hivyo?
29
Wenzake wakuu wa kike wakamjibu, nao ni werevu wa kweli, naye mwenyewe akajijibu maneno yaleyale ya kwamba:
30
Labda wameona nyara za kujigawanyia: mwanamwali mmojammoja au wawiliwawili wa kila mtu mmoja, tena ziko nguo za rangi, ndizo nyara zake Sisera, hizo nyara ni nguo za rangi zilizofumwa vizuri, ni nguo za rangi za mbalimbali, ni zenye darizi pande mbili za kupatana na shingo zao walio wenye hizo nyara.
31
Hivyo na waangamie wote walio adui zako, Bwana! Lakini wao wampendao na wawe kama jua lenyewe, likija kucha lenye utukufu wake! Kisha nchi ikapata kutulia miaka 40.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21