bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Song of Solomon 1
Song of Solomon 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 2 →
1
Na aninonee kwa manoneo ya kinywa chake!
2
Kwani upendo wako hupendeza kuliko mvinyo.
3
Mafuta yako ya kupaka hunukia vema, jina lako ni mafuta yaliyomiminwa, kwa hiyo wanawali hukupenda.
4
Nivute, nikufuate nyuma! Na tupige mbio! Hata mfalme akiniingiza vijumbani mwake, na tupige vigelegele kwa kukufurahia wewe! Huo upendo wako tuutukuze kuliko mvinyo! Wanakupenda kwelikweli.
5
Mimi ni mweusi, lakini ninapendeza, ninyi wanawake wa Yerusalemu! Nafanana na mahema ya Kedari, tena na mazulia ya Salomo.
6
Msinionee kwa kuwa mweusimweusi! Ni jua lililonichoma. Wana wa mama yangu walinikasirikia, maana waliniweka kuwa mlinzi wa mashamba ya mizabibu, lakini hata shamba langu la mizabibu sikulilinda.
7
Niambie wewe, mpendwa wa roho yangu: Unalishia wapi? Tena ni wapi, unapowapumzishia kondoo, jua likiwa kali? Mbona niwe kama mwenye kutangatanga penye makundi ya wenzako?
8
“Usipopajua mwenyewe uliye mzuri kuliko wanawake wengine, toka tu na kuzifuata nyayo za kondoo, kavichunge vitoto vyako vya mbuzi matuoni kwa wachungaji!
9
Ninakufananisha wewe, mpenzi wangu, na farasi avutaye gari la Farao.
10
Mashavu yako hupendeza kwa kili za nywele, nayo shingo yako yenye ushanga.
11
Na tukutengenezee vikufu vya dhahabu vyenye vifungo vya fedha.
12
Mfalme akiwa anakaa mezani pake, manukato yangu ya narada hutoa mnuko wao mzuri.”
13
Mpendwa wangu ni kifuko cha manemane kikaacho katikati ya maziwa yangu.
14
Mpendwa wangu ni kichala cha mhina kitokacho mizabibuni kwenye Engedi.
15
Nikikutazama, mpenzi wangu, u mwanamke mzuri, “u mwanamke mzuri kweli mwenye macho kama ya hua.”
16
Wewe nawe, mpendwa wangu, u kijana mzuri, unapendeza kweli. Malalo yetu ni majani mabichi.
17
“Boriti za nyumba yetu ni miangati, mbau zetu za kuzifunika kuta ni mvinje.”
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8