bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Song of Solomon 7
Song of Solomon 7
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 8 →
1
Miguu yako yenye mitalawanda ni mizuri mno, binti mkuu! Viuno vyako vinaviringana kama mapambo ya shingoni yaliyotengenezwa na mikono ya mtu aliye fundi kweli.
2
Kitovu chako ni kama chano kilichoviringana, kisichokosa mvinyo iliyotiwa viungo vizuri; tumbo lako ni kama chungu ya ngano iliyozingwa na nyinyoro.
3
Maziwa yako mawili hufanana na vitoto viwili vya kulungu, au na wana wa pacha wa paa.
4
Shingo yako ni kama mnara wa meno ya tembo, macho yako ni kama viziwa vya kuko Hesiboni, vilivyoko hapo langoni, papitapo watu wengi, pua yako ni kama mnara wa Libanoni uelekeao Damasko.
5
Kichwa chako hapa juu ni kama Karmeli, nywele za kichwani pako ni nyekundu kama nguo za kifalme, hata mfalme angependa kufungwa nayo hiyo misuko ya nywele.
6
U mzuri peke yako kwa kupendeza sana, mpenzi wangu, unazidisha mambo yafurahishayo.
7
Hivyo, ulivyokua, unafanana na mtende, nayo maziwa yako yanafanana na vichala vya mzabibu.
8
Nilisema: Nitaupanda mtende huu, niyashike makuti yake, maziwa yako yaniwie kama vichala vya mzabibu, nao mnuko wa pumzi yako uniwie kama wa machungwa.
9
Kinywa chako ni kama mvinyo njema inayompendeza mpendwa wako, akiinywa, nayo hupita polepole midomoni mwao walalao usingizi.”
10
Mimi ni wake, mpendwa wangu, naye ananitunukia.
11
Njoo, mpendwa wangu, tutoke kwenda shambani, tulale vijijini!
12
Na tuondoke mapema kwenda mizabibuni, tutazame, kama mizabibu inachanua na kuyafunua maua. tutazama nayo mikomamanga, kama imepata maua! Hapo ndipo, nitakapokupa kukumbatiana na mimi.
13
Mitunguja sasa inanuka, napo milangoni petu yapo matunda mazuri, mapya na ya mwaka uliopita; ndiyo, niliyokuwekea, mpendwa wangu.
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8