bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Song of Solomon 3
Song of Solomon 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 4 →
1
Nilipolala usiku nilimtafuta yeye, roho yangu inayempenda; nilimtafuta, lakini sikumwona.
2
Na niinuke, nizunguke mjini, roho yangu inayempenda nimtafute barabarani na viwanjani; nilimtafuta, lakini sikumwona.
3
Walinzi wazungukao mjini waliponiona, nikawauliza: Mmemwona yeye, roho yangu inayempenda?
4
Nilipokwisha kuwapita kwenda mbele kidogo, ndipo, nilipomwona yeye, roho yangu inayempenda. Nikamshika, nisimwachie tena, mpaka nikamwingiza nyumbani mwa mama yangu, chumbani mwake yeye aliyenizaa.
5
“Nawaapisha ninyi, wanawake wa Yerusalemu, nikiwataja paa na kulungu wake walioko porini, msimwamshe, wala msimhangaishe yeye ninayempenda, ila mwacheni tu, mpaka atakapopendezwa wenyewe!”
6
Ni nani huyo apandaye kutoka nyikani? Anafanana kuwa kama wingu la moshi lililo kama nguzo, ni manemane na uvumba aliyovukiziwa na mavumbi ya manukato yote ya mchuuzi yanukayo vizuri.
7
Tazameni! Kiko kiti, ni cha kifalme cha Salomo! Wanguvu sitini wanakizunguka, ndio wanguvu wa Waisiraeli.
8
Wao wote wanashika panga, ni mafundi wa vita, kila mmoja anao upanga wake kiunoni pake wa kukingia mastusho ya usiku.
9
Kiti hicho mfalme Salomo alijitengenezea kwa miti ya Libanoni,
10
miguu yake aliifanya kwa fedha, maegemeo ni ya dhahabu, pa kukalia ni nguo nyekundu za kifalme. Hapo kati yako marembo mazuri mno yaliyoshonwa na wanawake wa Yerusalemu ya kumpendeza mfalme.
11
Tokeni, wanawake wa Yerusalemu, mmtazame mfalme Salomo! Amevika kilemba, mama yake alichomfunga siku ya ndoa yake, maana ndiyo siku, moyo wake uliyoifurahia.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8