bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Song of Solomon 5
Song of Solomon 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 6 →
1
“Ninaingia bustanini pangu, umbu langu na mchumba wangu, niunge manemane na manukato yangu, nile masega yangu pamoja na asali yangu, ninywe mvinyo yangu na maziwa yangu. Nanyi wenzangu, leni, nyweni, mpaka mleweshwe na upendo!
2
Nililala usingizi, lakini moyo ulikuwa macho; mara nikasikia, mpendwa wangu akigonga mlango: “Nifungulie, umbu langu, mpenzi wangu, hua yangu, mwenzangu atakataye! Kwa kuwa nimejazwa umande kichwani pangu, kwa kuwa misuko ya nywele zangu imejaa unyevu wa usiku.”
3
Nikajibu: Nimekwisha kuivua kanzu yangu, nitaivaaje tena? Nikaisha kuiogesha miguu yangu, nitawezaje kuichafua tena?
4
Ndipo, mpendwa wangu alipoutia mkono wake tunduni, moyo wangu ukarukaruka ndani kwa ajili yake.
5
Nikainuka kumfungulia yeye mpendwa wangu, manemane yalipokuwa yanachuruzika mikononi pangu, navyo vidole vyangu vikadondokea manemane hapo pa kulishikia komeo.
6
Lakini nilipokwisha kumfungulia mpendwa wangu, alikuwa ametoweka kabisa, yeye mpendwa wangu. Hapo aliposema, roho yangu ilitaka kuzimia, kwa hiyo nikamtafuta, lakini sikumwona, nikamwita, lakini hakunijibu.
7
Walinzi wazungukao mjini waliponiona wakanipiga na kuniumiza, wakanivua mtandio wangu wale walinzi wa boma.
8
Nawaapisha ninyi, wanawake wa Yerusalemu: Mkimwona mpendwa wangu mtampasha habari gani? Ya kuwa mimi nimeugua kwa upendo tu!
9
“Mpendwa wako anawapitaje wapendwa wengine, wewe uliye mzuri miongoni mwa wanawake?
10
Mpendwa wako anawapitaje wapendwa wengine, ukituapisha hivyo?” Mpendwa wangu ni mweupe sana, tena mwekundu, anajulikana katika elfu kumi.
11
Mkikitazama kichwa chake, ni kama dhahabu tupu, misuko ya nywele zake nayo ni makuti yaning'iniayo, nazo ni nyeusi kama kunguru.
12
Macho yake kama ya hua waliopo penye vijito vya maji, hujiogesha katika maziwa, huwapo na kuchangamka sana.
13
Mashavu yake ni kama matuta yaliyopandwa manukato, namo juu mna vijanijani vinukavyo vizuri; midomo yake ni nyinyoro zidondokazo manemane ya majimaji.
14
Mikono yake ni vigogo vya dhahabu zilizotiwa vito vingi vya Tarsisi, tumbo lake ni urembo wa meno ya tembo uliofunikwa na vito vya safiro.
15
Paja zake ni nguzo za mawe meupe juu ya misingi ya dhahabu tupu; ukimtazama, anafanana na Libanoni, ni mtukufu kama miangati.
16
Kinywa chake husema matamu tu, yaliyo yake yote pia hupendeza. Ndivyo mpendwa wangu alivyo, ndivyo, mwenzangu alivyo, ninyi wanawake wa Yerusalemu.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8