bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Song of Solomon 2
Song of Solomon 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 3 →
1
Mimi ni ua la uwago wa Saroni, ni nyinyoro ya mabondeni.
2
“Kama ua lilivyo katikati ya miiba, ndivyo, mpenzi wangu alivyo katikati ya wanawali.”
3
Kama mchungwa ulivyo katikati ya miti ya msituni, ndivyo, mpendwa wangu alivyo katikati ya vijana. Kwa kumtunukia nilikaa kivulini kwake; tunda lake ni tamu sana, nikilila.
4
Akaniingiza nyumbani, wanyweamo mvinyo, nayo bendera yake iliyokuwa juu yangu, ni upendo.
5
Nitieni nguvu kwa maandazi ya zabibu, kaniinueni kwa machungwa! Kwani mimi ni mgonjwa kwa kupenda sana.
6
Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu, nao wa kuume unanikumbatia.
7
“Nawaapisha ninyi, wanawake wa Yerusalemu, nikiwataja paa na kulungu wake walioko porini, msimwamshe, wala msimhangaishe yeye ninayempenda, ila mwacheni tu, mpaka atakapopendezwa mwenyewe!”
8
Iko sauti ya mpendwa wangu, naisikia, anakuja akiruka milimani, akichezacheza vilimani.
9
Mpendwa wangu anafanana na paa mume au na kijana wa kulungu. Mtazame! Yuko akisimama nyuma ya kitalu chetu, akichungulia madirishani, akaonekana penye vyuma vyao.
10
Mpendwa wangu ananiita na kuniambia: “Inuka, mpenzi wangu mzuri, uje hapa!
11
Kwani tazama! Kipupwe kimepita, mvua nayo ikakoma, ikaenda zake.
12
Maua yanaonekana katika nchi, siku za kuimba zimetimia, sauti za hua zinasikilika katika nchi yetu.
13
Mkuyu unaanza kuziivisha kuyu zake changa, nayo mizabibu inachanua maua yanukayo vema; inuka, mpenzi wangu mzuri, uje hapa!
14
Hua yangu hapo ngomeni penye mwamba, ulijificha magengeni, nipe kuuona uso wako, nipe kuisikia nayo sauti yako! Kwani sauti yako ni tamu, nao uso wako unapendeza.
15
Tukamatieni nyegere, nyegere wale wadogo! Maana huiharibu mizabibu, nayo mizabibu yetu inachanua.”
16
Mpendwa wangu ni wangu, nami ni wake yeye alishaye penye nyinyoro.
17
Mpaka jua la mchana lipunguke ukali, vivuli vikijiendea mbiombio, geuka, mpendwa wangu, uruke kama paa au kijana wa kulungu, milimani kwenye makorongo!
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8