bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Song of Solomon 6
Song of Solomon 6
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 7 →
1
“Je? Ndiko wapi, mpendwa wako alikokwenda, wewe uliye mzuri miongoni mwa wanawake? Ameshika njia gani mpendwa wako, tumtafute pamoja na wewe?”
2
Mpendwa wangu ameshuka kwenda bustanini pake, kutembea bustanini penye matuta ya manukato, apate kuchuma nyinyoro.
3
Mimi ni wake mpendwa wangu, naye mpendwa wangu ni wangu mimi; hulisha penye nyinyoro.
4
“Kweli u mzuri kama Tirsa, unapendeza kama Yerusalemu, tena unaogopesha, mpenzi wangu, kama vikosi vyenye bendera.
5
Yageuze macho yako, yasinitazame, kwani hunitatanisha; nywele zako zinafanana na kundi la mbuzi walalao upande wa kushukia wa milimani kwa Gileadi.
6
Meno yako ni kama kundi la kondoo wanaotoka kuogeshwa, wote pia ni wenye wana wa pacha, kwao hakuna hata mmoja aliye peke yake.
7
Shavu lako huonekana mtandioni mwako kuwa kama komamanga ipevukayo sana.
8
Wako wanawake wa kifalme sitini na masuria themanini, tena wako wanawali wasiohesabika.
9
Lakini yuko mmoja tu aliye hua wangu na mwenzangu atakataye, ni mwana wa pekee wa mama yake, aliyemzaa humpenda sana; wanawali wenzake wakimwona humwazia kuwa mwenye shangwe, nao wanawake wa kifalme na masuria humtukuza.”
10
“Nani huyu mwanamke aonekaye kama mapambuzuko? Ni mzuri kama mwezi, anang'aa kama jua, anaogopesha kama vikosi vilivo vyenye bendera.”
11
Nilishuka kwenda bustanini penye milozi, nijifurahishe kwa kuyaona machipukizi mapya yaliyoko bondeni; tena nilitaka kuitazama mizabibu, kama imechanua, nayo mikomamanga, kama imepata maua.
12
Nilipokuwa siviangalii, roho yangu ikanipeleka, ikaniweka penye magari, nayo yalikuwa ya wakuu wa kwetu.
13
“Rudi! Rudi, Sulamiti! Rudi! Rudi, tukutazame vema!” Mnatakaje kumtazama Sulamiti? Anafanana na michezo ya vita ya Mahanaimu?
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 7 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8