bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Song of Solomon 8
Song of Solomon 8
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
1
Laiti ungekuwa kama umbu aliyeyanyonya maziwa ya mama yangu! Kama ningekukuta nje ningekunonea pasipo kuona watu watakaonibeza.
2
Ningekuongoza, nikupeleke nyumbani mwa mama yangu, ungenifundisha; kisha ningekunywesha mvinyo yenye viungo, nayo ni mbichi iliyotengenezwa kwa komamanga zangu.
3
Mkono wake wa kushoto ungekuwa chini ya kichwa changu, nao wa kuume ungenikumbatia.
4
Nawaapisha ninyi, wanawake wa Yerusalemu, msimwamshe, wala msimhangaishe yeye, ninayempenda, ila mwacheni tu, mpaka atakapopendezwa mwenyewe.
5
“Ni nani huyu mke apandaye kutoka nyikani akimwegemea mpendwa wake?” “Chini ya mchungwa nilikuamsha; ndipo, mama yako aliposhikwa na uchungu alipokuzaa na kuona uchungu.
6
Na uniweke moyoni mwako kama pete yenye muhuri! Na uniweke napo mkononi pako kama pete yenye muhuri! Kwani upendo ni wenye nguvu kama kifo, hushupaa kama kuzimu kwa wivu, miali yake ni miali ya moto, ni moto uwakao kwa kuwashwa na Bwana.
7
Maji mengi hayawezi kuuzima upendo, majito makuu hayautosi, Kama mtu angezitoa mali zote zilizomo nyumbani mwake kwa kwamba: apate kupendwa, watu wangemsimanga kabisa.” Tumepata ndugu wa kike mdogo,
8
naye maziwa yake hayako bado; sasa huyu ndugu yetu wa kike tumfanyie nini siku atakapoposwa?
9
“Tutajenga juu yake kingio la fedha, kama yeye ni ukuta, lakini kama ni mlango tutaufunga kwa mbao za miangati.”
10
Mimi ni ukuta, nayo maziwa yangu ni kama minara. Kwa hiyo nikawa machoni pake mahali patokeapo utulivu.
11
Salomo alikuwa na shamba la mizabibu huko Baali-Hamoni, naye akawakodisha walinzi hilo shamba la mizabibu, kila mtu amtolee fedha elfu kwa matunda yake.
12
Shamba langu la mizabibu ni langu, ninaliangalia mimi; zile fedha ninakuachia wewe, Salomo, tena mia mbili za kuwapa wao wayalindao matunda yake.
13
“Wewe ukaaye bustanini, wenzako huisikiliza sauti yako; itoe namo masikioni mwangu mimi!”
14
Kimbia, mpendwa wangu, kama paa au kijana wa kulungu warukao milimani kwenye manukato!
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8