bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Song of Solomon 4
Song of Solomon 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 5 →
1
Nikikutazama, mpenzi wangu, u mwanamke mzuri, nikikutazama, u mwanamke mzuri kweli, macho yako huwa ya hua yakichungulia katika mtandio wako; nywele zako zinafanana na kundi la mbuzi walalao upande wa kushukia wa mlimani kwa Gileadi.
2
Meno yako ni kama kundi la kondoo waliokatwa manyoya, wanaopanda na kutoka majini wakiisha kuogeshwa, wote pia ni wenye wana wa pacha, kwao hakuna hata mmoja aliye peke yake.
3
Midomo yake ni kama uzi wenye rangi nyekundu, kinywa chako kinapendeza nacho. Shavu lako huonekana mtandioni mwako kuwa kama komamanga ipevukayo sana.
4
Shingo yako ni kama mnara wa Dawidi uliojengewa selaha, vigao elfu viko vimeangikwa kwake, vyote pia ni vya kuwakingia mafundi wa vita.
5
Maziwa yako mawili yanafanana na vitoto viwili vya kulungu au na wana wa pacha wa paa walishwao penye nyinyoro.
6
Mpaka jua la mchana lipunguke ukali, vivuli vijiendee mbiombio, ndipo, nitakapokwenda zangu mlimani kwenye manemane, hata kilimani kwenye uvumba.
7
Wewe, mpenzi wangu, u mzuri peke yako, huna doadoa kabisa.”
8
Toka Libanoni, mchumba wangu, twende pamoja! Toka Libanoni, twende pamoja, njoo! Tazama, huko juu Amana nako juu Seniri na Hermoni ndiko, simba wanakokaa, hata machui wako kule milimani.
9
Umenipokonya moyo wangu, uliye umbu na mchumba wangu; umenipokonya moyo wangu, kwa kunitazama na jicho lako moja tu, ukanifunga kwa kikufu kimoja, unachokivaa shingoni pako.
10
Ni kuzuri mno kukumbatiana na wewe, uliye umbu langu na mchumba wangu; kukumbatiana na wewe kunapendeza kuliko kunywa mvinyo, mnuko wa mafuta yako ni mzuri kuliko wa manukato yote.
11
Midomo yako, mchumba wangu, inadondoka asali safi, asali na maziwa ndiyo yaliyoko chini ya ulimi wako, nao mnuko wa mavazi yako ni mzuri kama wa Libanoni.
12
Umbu langu aliye mchumba wangu ni bustani iliyofungwa, ni kisima kilichofungwa, ni chemchemi iliyozibwa na kutiwa muhuri.
13
Machipukizi yako ni kimwitu cha mikomamanga izaayo matunda yapendezayo sana, nayo mihina na miafu iko.
14
Iko hata mianjano na mikumbi na mikoroshi na midalasini, miti yote itokayo uvumba na manemane nayo mishubiri iko, tena iko miti yote itokayo manukato yapitayo mengine.
15
Nayo chemchemi iko bustanini na kisima chenye maji ya uzima na vijito vitokavyo Libanoni.”
16
Inuka, upepo wa kaskazini! Njoo, upepo wa kusini! Vuma bustanini mwangu, minuko yake mizuri ifurikie!
17
Mpendwa wangu aingie bustanini pake, ayale matunda yake yapendezayo!
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8