bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
/
Jeremiah 11
Jeremiah 11
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 12 →
1
Yawe akanitolea mimi Yeremia ujumbe, akisema:
2
Sikiliza maneno ya agano hili, kisha uende kuyatangazia watu wa Yuda na wakaaji wa Yerusalema.
3
Utawaambia hivi: Yawe, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Alaaniwe mutu yeyote asiyeshika masharti ya agano hili.
4
Hili ni agano nililowaagiza babu zenu kutii nilipowaondoa katika inchi ya Misri, kutoka katika shimo la moto. Niliwaambia wanitii na kufanya yote niliyowaamuru, na kwamba wakifanya hivyo, watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.
5
Na kwa njia hiyo mimi nitatimiza ahadi niliyowatolea babu zenu, kwamba nitawapa inchi inayojaa maziwa na asali, kama inavyokuwa hata leo. Nami nikajibu: Ikuwe hivyo, ee Yawe.
6
Yawe akaniambia: Tangaza maneno hayo yote katika miji ya Yuda na katika barabara za Yerusalema. Uwaambie watu wayasikilize masharti ya agano hili na kuyashika.
7
Maana niliwaonya vikali babu zao nilipowaondoa katika inchi ya Misri, nami nimeendelea kuwaonya wanitii mpaka siku hii ya leo.
8
Lakini wao hawakunitii, wala hawakunisikiliza. Kila mumoja wao alizidi kuwa mugumu na mwovu. Basi, niliwaazibu kulingana na masharti ya agano hili nililowaamuru kushika, lakini hao wakakataa kulishika.
9
Tena Yawe akaniambia: Watu wa Yuda na wakaaji wa Yerusalema wanafanya shauri baya la kuniasi.
10
Wameurudilia uovu wa babu zao ambao walikataa kusikiliza maneno yangu; wanaiabudu miungu mingine na kuitumikia. Watu wa Israeli na watu wa Yuda wamevunja agano nililofanya na babu zao.
11
Kwa hiyo, Yawe anasema hivi: Nitaleta hasara juu yao ambayo hawataweza kuiepuka. Hata kama wakinililia namna gani, sitawasikiliza.
12
Kwa hiyo wakaaji wa Yuda na wa Yerusalema watakapoiendea miungu yao ambayo wanaifukizia ubani, lakini miungu hiyo haitaweza kuwaokoa wakati huo wa hasara itakayowapata.
13
Enyi watu wa Yuda, hesabu ya miji yenu ni sawasawa na hesabu ya miungu yenu. Na kama vile barabara zenu za Yerusalema zinavyokuwa nyingi, ndivyo mulivyojenga mazabahu ya haya, ni kusema ya kufukizia ubani kwa mungu Bali.
14
Basi, wewe Yeremia, usiwaombee watu hawa, usinililie kwa ajili yao, wala kunisihi. Maana, hata wakiniomba watakapokuwa katika hasara, sitawasikiliza.
15
Yawe anasema: Watu wangu wapendwa wana haki gani ya kuingia ndani ya hekalu langu ikiwa wametenda maovu? Wanazani kwamba viapo vyao na sadaka zao wanazonitolea zitawakingia hasara ile.
16
Wakati fulani, mimi nilisema kwamba wao ni muzeituni wenye majani mabichi, muzeituni muzuri na wenye matunda mema; lakini sasa, kwa ngurumo ya zoruba kubwa, nitauchoma kwa moto na kuyateketeza matawi yake.
17
Mimi Yawe wa majeshi niliuotesha huu muzeituni; lakini sasa ninatangaza hasara juu yake, kwa sababu ya maovu ambayo watu wa Israeli na Yuda wameyafanya. Wamenikasirikisha kwa kumufukizia mungu Bali ubani.
18
Yawe alinijulisha, nami nikaelewa; Yawe alinijulisha shauri lao baya.
19
Nami nilikuwa kama kondoo mupole anayepelekwa kuchinjwa; sikujua kwamba shauri walilofanya lilikuwa juu yangu. Wao walisema: Tuuharibu muti pamoja na matunda yake, tumwue apate kusahaulika katika dunia, jina lake lisikumbukwe tena.
20
Lakini, ee Yawe wa majeshi, wewe unayehukumu kwa haki, unayechunguza mioyo na akili za watu, unijalie nione jinsi utakavyowalipiza kisasi, maana ninayaweka maneno yangu kwako.
21
Kwa hiyo Yawe wa majeshi anasema hivi juu ya watu wa Anatoti ambao wanataka kuniua na kuniambia: Usitutabirie kwa jina la Yawe, kama si vile tutakuua.
22
Ndiyo, Yawe wa majeshi anasema hivi: Nitawaazibu watu hao. Vijana wao watauawa kwa upanga; watoto wao wanaume na wanawake watakufa kwa njaa.
23
Nimepanga muda wa kuleta maangamizi juu ya watu wa Anatoti. Wakati huo utakapofika, hakuna hata mumoja wao atakayebaki muzima.
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 12 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52