bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
/
Song of Solomon 4
Song of Solomon 4
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 5 →
1
Hakika sura yako ni nzuri, ewe mupenzi wangu, hakika sura yako ni nzuri! Macho yako ni mazuri kama ya njiwa ndani ya ushungi wako. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi wanaoshuka kwenye milima ya Gileadi.
2
Meno yako ni kama kundi la kondoo dike waliokatwa manyoya, wanaotoka kwenye maji kisha kuogeshwa; kila mumoja akiwa na pacha lake, na hakuna yeyote aliyekufiwa.
3
Midomo yako ni kama utepe mwekundu, kinywa chako kinapendeza kweli. Mashavu yako ni kama nusu mbili za makomamanga ndani ya ushungi wako.
4
Shingo yako ni kama munara wa Daudi, uliojengwa kwa kulinda silaha, ambako ngao elfu moja zimetundikwa, zote zikiwa za mashujaa.
5
Maziba yako ni kama paa mapacha, ambao wanachungwa penye yungiyungi.
6
Nitakaa kwenye mulima wa marasi, na kwenye kilima cha ubani, mpaka pale kutakapopambazuka, na giza kutoweka.
7
Wewe ni nzuri kabisa, ee mupenzi wangu, wewe hauna kilema chochote.
8
Kuja, muchumba wangu, tuondoke Lebanoni, na tuiache mbali milima ya Lebanoni. Shuka toka kilele cha mulima Amana, toka kilele cha Seniri na Hermoni, toka mashimo ya simba, toka kwenye milima ya chui.
9
Umeua moyo yangu, dada yangu, muchumba wangu, umeua moyo yangu, kwa kunitupia jicho mara moja tu, na kwa ule mukufu wako katika shingo.
10
Dada yangu, muchumba wangu; mapendo yako yananivuta ajabu. Ni bora kuliko divai, marasi yako yananuka vizuri kuliko viungo vyote.
11
Midomo yako inadondosha asali, ee muchumba wangu, ulimi wako una asali na maziwa. Harufu nzuri ya nguo zako ni kama miti ya Lebanoni.
12
Dada yangu, muchumba wangu, ni bustani yangu ya pekee, chemichemi inayochungwa.
13
Machipukizi yako ni bustani ya mikomamanga pamoja na matunda bora kuliko yote, hina na nardo,
14
nardo na zafarani, muchai na mudalasini, ubani na udi, na mimea mingine yenye harufu nzuri.
15
Wewe ni chemichemi ya bustani, kisima cha maji yasiyokauka, vijito vinavyotiririka kutoka milima ya Lebanoni.
16
Vuma, ewe upepo wa kaskazini, kuja, ewe upepo wa kusini, muvume juu ya bustani yangu, mujaze anga kwa marasi, mupenzi wangu akuje katika bustani yake akule matunda yake bora kuliko yote.
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8