bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
/
Psalms 119
Psalms 119
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
← Chapter 118
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 67
Chapter 68
Chapter 69
Chapter 70
Chapter 71
Chapter 72
Chapter 73
Chapter 74
Chapter 75
Chapter 76
Chapter 77
Chapter 78
Chapter 79
Chapter 80
Chapter 81
Chapter 82
Chapter 83
Chapter 84
Chapter 85
Chapter 86
Chapter 87
Chapter 88
Chapter 89
Chapter 90
Chapter 91
Chapter 92
Chapter 93
Chapter 94
Chapter 95
Chapter 96
Chapter 97
Chapter 98
Chapter 99
Chapter 100
Chapter 101
Chapter 102
Chapter 103
Chapter 104
Chapter 105
Chapter 106
Chapter 107
Chapter 108
Chapter 109
Chapter 110
Chapter 111
Chapter 112
Chapter 113
Chapter 114
Chapter 115
Chapter 116
Chapter 117
Chapter 118
Chapter 119
Chapter 120
Chapter 121
Chapter 122
Chapter 123
Chapter 124
Chapter 125
Chapter 126
Chapter 127
Chapter 128
Chapter 129
Chapter 130
Chapter 131
Chapter 132
Chapter 133
Chapter 134
Chapter 135
Chapter 136
Chapter 137
Chapter 138
Chapter 139
Chapter 140
Chapter 141
Chapter 142
Chapter 143
Chapter 144
Chapter 145
Chapter 146
Chapter 147
Chapter 148
Chapter 149
Chapter 150
Chapter 120 →
1
Heri watu wanaoishi katika ukamilifu, wanaofuata sheria ya Yawe.
2
Heri wanaoshika maagizo yake, wanaomutafuta kwa moyo wao wote,
3
watu wasiotenda uovu hata kidogo, lakini wanafuata siku zote njia zake.
4
Ee Mungu, umetupatia kanuni zako kusudi tuzishike kwa uangalifu.
5
Heri mwenendo wangu ungeimarika kwa kuyafuata masharti yako!
6
Nikichunguza amri zako zote, hapo kweli sitapata haya.
7
Nitakusifu kwa moyo wenye kunyooka, nikijifunza maamuzi yako ya haki.
8
Nitafuata masharti yako; usiniache hata kidogo.
9
Namna gani kijana ataweza kujichunga katika njia safi? Ni kwa kufuatilia neno lako.
10
Ninakutafuta kwa moyo wote; usiniachilie kugeuka mbali na amri zako.
11
Nimeshika neno lako ndani ya moyo wangu, kusudi nisikukosee.
12
Utukuzwe, ee Yawe! Unifundishe masharti yako.
13
Nitarudiliarudilia kwa sauti maamuzi yako yote uliyotoa.
14
Ninafurahi kufuata maagizo yako, kuliko kuwa na utajiri mwingi.
15
Ninafikiri juu ya kanuni zako, na kuangalia njia zako.
16
Ninafurahia masharti yako; sitasahau neno lako.
17
Unitendee mimi mutumishi wako kwa wema, nipate kuishi na kushika neno lako.
18
Uyafungue macho yangu, nipate kuona maajabu ya sheria yako.
19
Mimi ni mugeni tu hapa katika dunia; usinifiche amri zako.
20
Roho yangu inaugua kwa hamu kubwa ya kutaka kujua siku zote maamuzi yako.
21
Wewe unawakaripia wenye kiburi waliolaaniwa, ambao wanageuka mbali na amri zako.
22
Uniepushe na matusi na mazarau yao, maana ninafuata maagizo yako.
23
Hata kama wakubwa wananifanyia shauri baya, mimi mutumishi wako nitafikiri juu ya masharti yako.
24
Maagizo yako ndiyo furaha yangu; hayo ndio washauri wangu.
25
Ninagaagaa chini ndani ya mavumbi; unirudishie uzima sawa ulivyoahidi.
26
Nimeungama niliyotenda, nawe ukanijibu; unifundishe masharti yako.
27
Unifundishe namna ya kushika kanuni zako, nami nitafikiri juu ya matendo yako ya ajabu.
28
Ninalia kwa uchungu; unirudishie nguvu kama ulivyoahidi.
29
Uniepushe na njia za upotovu; unifundishe kwa huruma sheria yako.
30
Nimechagua njia ya uaminifu; nitafuatilia maamuzi yako.
31
Ninashikamana na maagizo yako, ee Yawe; usikubali nipatishwe haya!
32
Nitafuatilia amri zako, maana unanifungua akili zaidi.
33
Ee Yawe, unifundishe kutii masharti yako, nami nitayashika mpaka mwisho.
34
Unieleweshe nipate kushika sheria yako, niifuate kwa moyo wangu wote.
35
Uniongoze katika njia ya amri zako, maana humo ninapata furaha yangu.
36
Uvute moyo wangu kufuata maagizo yako, na si kwa ajili ya kupata faida isiyofaa.
37
Uniepushe nisifuate mambo ya ovyo; unionyeshe njia yako, unipe uzima.
38
Unitimizie mimi mutumishi wako ahadi yako; ahadi unayowapa wale wanaokuheshimu.
39
Uniepushe na matusi ninayoogopa; maana maamuzi yako ni mema.
40
Ninatamani sana kutii kanuni zako; unirudishie uzima maana wewe ni wa haki.
41
Wema wako unifikie, ee Yawe; uniokoe kama ulivyoahidi.
42
Hapo nitaweza kuwajibu hao wanaonitukana, maana mimi ninatumainia neno lako.
43
Unijalie kusema ukweli wako siku zote, maana ninatumainia maamuzi yako.
44
Nitatii sheria yako siku zote, nitaishika milele na milele.
45
Nitaishi katika uhuru kamili, maana ninashugulika na kanuni zako.
46
Nitawatangazia wafalme maagizo yako, wala sitaona haya.
47
Furaha yangu ni kuzitii amri zako, ambazo mimi ninazipenda.
48
Ninaziheshimu na kuzipenda amri zako; nitafikiri juu ya masharti yako.
49
Ukumbuke ahadi yako kwangu mimi mutumishi wako, ahadi ambayo imenipa matumaini.
50
Hata katika taabu, inanituliza, maana ahadi yako inanipa uzima.
51
Wasiomujali Mungu wananizarau siku zote, lakini mimi sigeuki mbali na sheria yako.
52
Ninapokumbuka maamuzi yako ya tangu zamani, ninafarijika, ee Yawe.
53
Ninashikwa na hasira kali, ninapoona waovu wakivunja sheria yako.
54
Masharti yako yamekuwa wimbo wangu, nikikuwa huku kama mugeni.
55
Usiku ninakukumbuka, ee Yawe, na kushika sheria yako.
56
Hili ni pato langu, kwamba ninashika kanuni zako.
57
Wewe, ee Yawe, ndiwe hitaji langu lote; ninaahidi kushika maneno yako.
58
Ninataka kukupendeza kwa moyo wangu wote; unionee huruma kama ulivyoahidi!
59
Nimefikiri juu ya mwenendo wangu, na nimerudi nifuate maagizo yako.
60
Bila kukawia ninafanya haraka kushika amri zako.
61
Waovu wametega mitego waninase, lakini mimi sisahau sheria yako.
62
Usiku kati ninaamuka kwa kukusifu, kwa sababu ya maamuzi yako ya haki.
63
Mimi ni rafiki ya wote wanaokuheshimu, rafiki ya wanaoshika kanuni zako.
64
Dunia imejaa wema wako, ee Yawe, unifundishe masharti yako.
65
Umenitendea vizuri mimi mutumishi wako, kama ulivyoahidi, ee Yawe.
66
Unipe hekima na ufahamu, maana ninaaminia amri zako.
67
Mbele sijateswa nilikuwa nimepotea, lakini sasa ninashika neno lako.
68
Wewe ni muzuri na unatenda mazuri; unifundishe masharti yako.
69
Wenye kiburi wanasema uongo juu yangu, lakini mimi ninashika kanuni zako kwa moyo wote.
70
Mioyo yao inafungana sana, lakini mimi ninafurahia sheria yako.
71
Nimefaidika kutokana na taabu yangu, maana imeniwezesha kujifunza masharti yako.
72
Sheria uliyoweka ni bora kwangu, kuliko mali zote za dunia.
73
Kwa mikono yako wewe mwenyewe uliniumba; unijalie akili nijifunze amri zako.
74
Wanaokuheshimu wataniona na kufurahi, maana tumaini langu liko katika neno lako.
75
Ninajua kwamba maamuzi yako ni ya haki, ee Yawe, na kwamba umeniazibu maana wewe ni mwaminifu.
76
Wema wako unifariji, kama ulivyoniahidi mimi mutumishi wako.
77
Unionee rehema nipate kuishi, maana sheria yako ni furaha yangu.
78
Wenye kiburi wafezeheke, maana wananisumbua na maneno ya uongo, lakini mimi nitafikiri juu ya kanuni zako.
79
Wote wanaokuheshimu wakuje kwangu, wapate kujua maagizo yako.
80
Moyo wangu ukuwe mukamilifu juu ya masharti yako, kusudi nisifezeheke.
81
Ninachoka kwa kukungojea uniokoe; ninatumainia neno lako.
82
Macho yangu yanafifia nikingojea ulichoahidi. Ninauliza: “Utakuja wakati gani kunifariji?”
83
Nimekunjamana kama mufuko wa ngozi katika moshi, hata hivyo sijasahau masharti yako.
84
Mimi mutumishi wako nitavumilia mpaka wakati gani? Utawaazibu wakati gani wale wanaonitesa?
85
Wenye kiburi wamenichimbia mashimo, watu ambao hawafuati sheria yako.
86
Amri zako zote ni za kuaminiwa; watu wananitesa bila haki; unisaidie!
87
Walifikia karibu ya kuniangamiza, lakini mimi sikuvunja kanuni zako.
88
Kwa wema wako, unirudishie uzima, nipate kufuata maagizo uliyotangaza.
89
Neno lako, ee Yawe, linadumu milele; linasimama imara mbinguni.
90
Uaminifu wako unadumu kwa vizazi vyote, umeweka dunia pahali pake, nayo inadumu.
91
Kwa amri yako viumbe vyote viko leo, maana vitu vyote ni chini ya mamlaka yako.
92
Kama sheria yako isingekuwa furaha yangu, ningalikwisha kuangamia kwa taabu zangu.
93
Sitasahau hata kidogo kanuni zako, maana kwa njia yao unanirudishia uzima.
94
Mimi ni wako, uniokoe, maana nimejitoa kushika kanuni zako.
95
Waovu wananivizia wapate kuniua; lakini mimi ninafikiri juu ya maagizo yako.
96
Nimetambua kwamba kila kitu kina mwisho, lakini amri yako haina mupaka.
97
Ninapenda sana sheria yako! Ninafikiri juu yake muchana kutwa!
98
Amri yako iko nami siku zote, inanipa hekima kuliko waadui zangu.
99
Ninaelewa kuliko walimu wangu wote, kwa sababu ninafikiri juu ya maagizo yako.
100
Ninawapita wazee kwa akili yangu, kwa sababu ninashika kanuni zako.
101
Ninajizuiza kufuata njia mbaya, kusudi nipate kushika neno lako.
102
Sikugeuka mbali na maamuzi yako, maana wewe mwenyewe ulinifundisha.
103
Maagizo yako ni matamu sana kwangu; ni matamu kuliko asali!
104
Kwa kanuni zako ninapata hekima, kwa hiyo ninachukia kila mwenendo mubaya.
105
Neno lako ni taa ya kuniongoza, na mwangaza katika njia yangu.
106
Nimeapa na kuhakikisha kiapo changu, kwamba nitashika maamuzi yako ya haki.
107
Ee Yawe, ninateseka sana; unirudishie uzima kama ulivyoahidi.
108
Ee Yawe, upokee maombi yangu ya shukrani, na kunielezea maamuzi yako.
109
Maisha yangu yako katika hatari siku zote, lakini sisahau sheria yako.
110
Waovu wamenitegea mitego, lakini sigeuki mbali na kanuni zako.
111
Maagizo yako ni urizi mukubwa kwangu milele; hayo ni furaha ya moyo wangu.
112
Nimekusudia kwa moyo wote kufuata masharti yako milele.
113
Ninachukia watu wanafiki, lakini ninapenda sheria yako.
114
Wewe ni ngao yangu, na kimbilio langu; ninaweka tumaini langu katika neno lako.
115
Muondoke kwangu, enyi waovu, kusudi nipate kushika amri za Mungu wangu.
116
Uniimarishe sawa ulivyoahidi, nami nitaishi; usikubali nifezeheke katika tumaini langu.
117
Unishike nipate kuwa salama, nikuwe siku zote musikilivu kwa masharti yako.
118
Unawakataa wote wanaogeuka mbali na masharti yako; mawazo yao maovu ni ya bure.
119
Unaona waovu wote kama vile takataka, kwa hiyo mimi ninapenda maagizo yako.
120
Ninatetemeka kwa kukuogopa wewe; nimejaa hofu kwa sababu ya maamuzi yako.
121
Nimefanya mambo mema na ya haki; usiniache katika makucha ya waadui zangu.
122
Uhakikishe kunisaidia mimi mutumishi wako; usikubali wenye kiburi wanitese.
123
Macho yangu yanafifia nikingojea uniokoe, nikingojea utimize uliyoahidi.
124
Unitendee mimi mutumishi wako kadiri ya wema wako, unifundishe masharti yako.
125
Mimi ni mutumishi wako. Unipe akili nipate kujua maagizo yako.
126
Ee Yawe, sasa ni wakati wa kutenda kitu, kwa maana watu wanavunja sheria yako.
127
Kweli, ninapenda amri zako, kuliko hata zahabu safi kabisa.
128
Kwa hiyo, ninafuata kanuni zako zote; ninachukia kila njia ya upotovu.
129
Maagizo yako ni ya ajabu; kwa hiyo ninayashika kwa moyo wote.
130
Maelezo ya mafundisho yako yanaleta mwangaza; yanawapa akili wajinga.
131
Ninafungua kinywa kwa hamu kubwa, maana ninatamani sana amri zako.
132
Unigeukie na kunionea huruma, kama unavyowatendea wanaokupenda.
133
Uniimarishie hatua zangu kama ulivyoahidi; usikubali mimi nitawaliwe na uovu.
134
Unikomboe kutoka mateso ya wanadamu, kusudi nipate kushika kanuni zako.
135
Uniangazie uso wako kwa wema, unifundishe masharti yako.
136
Macho yangu yanatiririka machozi kama muto, kwa sababu watu hawaishiki sheria yako.
137
Ee Yawe, wewe ni wa haki; na hukumu zako ni za usawa.
138
Umetoa maagizo yako, kwa haki na uaminifu.
139
Upendo wangu kwako unanifanya niwake hasira, maana waadui zangu hawajali maneno yako.
140
Ahadi yako ni hakika kabisa, nami mutumishi wako ninaipenda.
141
Mimi ni mudogo na ninazarauliwa; hata hivyo sisahau kanuni zako.
142
Haki yako ni haki ya milele; sheria yako ni ya kweli.
143
Taabu na huzuni vimenipata, lakini amri zako ndizo furaha yangu.
144
Maagizo yako ni ya haki siku zote; unijalie akili nipate kuishi.
145
Ninakulilia kwa moyo wangu wote; unijibu, ee Yawe, nifuate masharti yako.
146
Ninakulilia, uniokoe nipate kushika maagizo yako.
147
Ninaamuka mbele ya mapambazuko na kukuomba musaada; ninaweka tumaini langu katika maneno yako.
148
Ninakaa macho wazi usiku kucha, kusudi nifikiri juu ya ahadi zako.
149
Kwa wema wako, ee Yawe, unisikilize; kwa haki yako, unirudishie uzima.
150
Wale wanaonitesa vibaya wanakaribia, hao wako mbali kabisa na sheria yako.
151
Lakini wewe ni karibu nami, ee Yawe, na amri zako zote ni za kuaminiwa.
152
Tangu zamani, nimejifunza maagizo yako ambazo umeziweka hata zidumu milele.
153
Uangalie mateso yangu, uniokoe, kwa maana sikusahau sheria yako.
154
Unitetee na kunikomboa; unirudishie uzima kama ulivyoahidi.
155
Waovu hawataokolewa hata kidogo, maana hawajali juu ya masharti yako.
156
Rehema yako ni kubwa, ee Yawe, unirudishie uzima kama ulivyoahidi.
157
Waadui na watesaji wangu ni wengi, lakini mimi sigeuki mbali na maagizo yako.
158
Ninapowaona waasi hao ninachukizwa sana, kwa sababu hawashiki amri zako.
159
Angalia, ee Mungu, ninavyopenda kanuni zako! Unirudishie uzima kadiri ya wema wako.
160
Kifungo cha neno lako ni ukweli, maamuzi yako yote ya haki yanadumu milele.
161
Wakubwa wananitesa bila sababu, lakini mimi ninaheshimu maneno yako kwa moyo wote.
162
Ninafurahi kwa sababu ya neno lako, kama mutu aliyekuta kitu cha bei kali.
163
Ninachukia kabisa uongo, lakini ninapenda sheria yako.
164
Ninakusifu mara saba kila siku, kwa sababu ya maamuzi yako ya haki.
165
Wanaopenda sheria yako wana amani kubwa; hakuna kinachoweza kuwaangusha.
166
Ee Yawe, ninakungojea uniokoe; mimi ninatimiza amri zako.
167
Ninashika maagizo yako; ninayapenda kwa moyo wote.
168
Ninashika kanuni na maagizo zako; wewe unaona mwenendo wangu wote.
169
Kilio changu kikufikie, ee Yawe! Unijalie akili kama ulivyoahidi.
170
Ombi langu likufikie; uniokoe kama ulivyoahidi.
171
Midomo yangu itatangaza sifa zako, maana unanifundisha masharti yako.
172
Nitaimba juu ya neno lako, maana amri zako zote ni za haki.
173
Ukuwe siku zote tayari kunisaidia, maana nimeamua kufuata kanuni zako.
174
Ninatamani sana uniokoe, ee Yawe; sheria yako ndiyo furaha yangu.
175
Unijalie kuishi nipate kukusifu; na maamuzi yako yanisaidie.
176
Ninatangatanga kama kondoo aliyepotea; ukuje kunitafuta mimi mutumishi wako, maana sikusahau amri zako.
← Chapter 118
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 67
Chapter 68
Chapter 69
Chapter 70
Chapter 71
Chapter 72
Chapter 73
Chapter 74
Chapter 75
Chapter 76
Chapter 77
Chapter 78
Chapter 79
Chapter 80
Chapter 81
Chapter 82
Chapter 83
Chapter 84
Chapter 85
Chapter 86
Chapter 87
Chapter 88
Chapter 89
Chapter 90
Chapter 91
Chapter 92
Chapter 93
Chapter 94
Chapter 95
Chapter 96
Chapter 97
Chapter 98
Chapter 99
Chapter 100
Chapter 101
Chapter 102
Chapter 103
Chapter 104
Chapter 105
Chapter 106
Chapter 107
Chapter 108
Chapter 109
Chapter 110
Chapter 111
Chapter 112
Chapter 113
Chapter 114
Chapter 115
Chapter 116
Chapter 117
Chapter 118
Chapter 119
Chapter 120
Chapter 121
Chapter 122
Chapter 123
Chapter 124
Chapter 125
Chapter 126
Chapter 127
Chapter 128
Chapter 129
Chapter 130
Chapter 131
Chapter 132
Chapter 133
Chapter 134
Chapter 135
Chapter 136
Chapter 137
Chapter 138
Chapter 139
Chapter 140
Chapter 141
Chapter 142
Chapter 143
Chapter 144
Chapter 145
Chapter 146
Chapter 147
Chapter 148
Chapter 149
Chapter 150
Chapter 120 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66
67
68
69
70
71
72
73
74
75
76
77
78
79
80
81
82
83
84
85
86
87
88
89
90
91
92
93
94
95
96
97
98
99
100
101
102
103
104
105
106
107
108
109
110
111
112
113
114
115
116
117
118
119
120
121
122
123
124
125
126
127
128
129
130
131
132
133
134
135
136
137
138
139
140
141
142
143
144
145
146
147
148
149
150