bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Hebrews 1
Hebrews 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 2 →
1
Kale Mungu alisema na baba zetu vinywani mwa wafumbuaji mara nyingi na kufuata njia.
2
Siku hizi za mwisho amesema na sisi kinywani mwa Mwanawe, aliyemweka kuwa kibwana chao yaliyo yake yote. Yeye ndiye, ambaye aliumba naye hata ulimwengu wote.
3
Huyu hutuangazia utukufu wake, kwani kama Mungu alivyo, ndivyo, naye alivyo; tena yeye huvitunza vyote kwa Neno lake lenye nguvu. Alipokwisha kutupatia osho liyaondoalo makosa, akaketi kuumeni kwa mwenye ukuu mbinguni juu,
4
akapata kuwa mtukufu kuliko malaika kwa hivyo, alivyorithi Jina linalolipita lao.
5
Kwani yuko malaika, Mungu aliyemwambia siku iwayo yote: Wewe ndiwe Mwanangu, siku hii ya leo mimi nimekuzaa? Na tena: Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu?
6
Kwa ajili ya siku, alipotaka kumwingiza mzaliwa wake wa kwanza tena ulimwenguni, anasema: Malaika wote wa Mungu sharti wamwangukie yeye!*
7
Mambo ya malaika anayasema kwamba: Huwatumia malaika zake kuwa upepo nao watumishi wake kuwa mioto iwakayo.
8
Lakini mambo ya mwana anayasema kwamba: Mungu, kiti chako cha kifalme kiko kale na kale pasipo mwisho, nayo fimbo ya ufalme wako ndiyo fimbo inyoshayo mambo ya watu.
9
Wewe ulipenda wongofu, ukachukia upotovu. Kwa hiyo Mungu aliye Mungu wako alikupaka mafuta ya kufurahisha kuliko yale ya wenzio.
10
Tena anasema: Wewe Bwana, mwanzoni uliiweka misingi ya nchi, mbingu nazo ni kazi ya mikono yako wewe.
11
Hizo zitaangamia, lakini wewe unafuliza kuwapo. Kweli, zote zitachakaa kama nguo,
12
nawe utazizinga kama nguo ya kujitandia; zitachujuka kama nguo. Lakini wewe ndiwe yuleyule uliyekuwa, miaka yako haitakoma.
13
Lakini yuko malaika, aliyemwambia po pote: keti kuumeni kwangu, mpaka niwaweke adui zako chini miguuni pako?
14
Hawa wote si roho tu za kutumika zitakazotumwa kuwatumikia wale watakaourithi wokovu?
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13