bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Hebrews 10
Hebrews 10
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 11 →
1
Maonyo hufanana, kama ni kivuli tu cha yale mema yatakayotokea, wala siyo sura yao yenyewe, ni kufanana tu nayo. Navyo vipaji vya tambiko, walivyovipeleka kila mwaka, ni vivyo hivyo kale na kale, navyo haviwezi kuwapa utimilifu wenye kuvitoa.
2
Je? Hao wenye kutambika wakiisha kutakaswa mara moja, kama wasingejua mioyoni kwamba: Makosa yako, hawangeacha kupeleka vipaji vya tambiko?
3
Lakini hivyo vipaji vya tambiko ndivyo vinavyowakumbusha makosa yao mwaka kwa mwaka,
4
kwani damu za ng'ombe na za mbuzi haziwezi kuondoa makosa.
5
Kwa hiyo anasema anapoingia ulimwenguni: Ng'ombe na vyakula vya tambiko hukuvitaka; lakini umenitengenezea mwili.
6
Ng'ombe za tambiko zinazoteketezwa nzima navyo vipaji vya kulipa makosa hukupendezwa navyo.
7
Ndipo, niliposema: Tazama, ninakuja! Mambo yangu yameandikwa katika kitabu cha kale, niyafanye, uyatakayo wewe, Mungu.
8
Kwanza anasema: Ng'ombe na vyakula vya tambiko, nazo ng'ombe za tambiko zinazoteketezwa nzima, navyo vipaji vya kulipa makosa hukuvitaka, wala hukupendezwa navyo, tena hutolewa, kama vilivyoagizwa.
9
Kisha alisema: Tazama, ninakuja, nifanye uyatakayo wewe. Hivyo analitangua lile la kwanza, apate kulisimamisha lile la pili.
10
Kwa hayo, aliyoyataka, tumetakaswa, kwani mwili wake Yesu Kristo ulitolewa mara moja.
11
Kila mtambikaji husimama siku kwa siku akitambika, navyo vipaji vya tambiko, anavyovitoa mara nyingi, ni vivyo hivyo visivyoweza kabisa kuondoa makosa.
12
Lakini huyu alitoa kipaji kimoja tu cha tambiko kwa ajili ya makosa ya watu, nacho ni cha kale na kale, kisha aliketi kuumeni kwa Mungu.
13
Sasa anangoja tu, adui zake wawekwe chini miguuni pake.
14
Kwani kwa kukitoa kile kipaji chake kimoja cha tambiko amewapa wenye kutakaswa utimilifu ulio wa kale na kale.
15
Naye Roho Mtakatifu anatushuhudia hivyo. Kwani kwanza anasema:
16
Bwana anasema: Agano, nitakalolifanya nao, siku hizi zitakapokuwa zimepita, ni hili: Nitawapa maonyo yangu, yakae mioyoni mwao; tena nitayaandika katika mawazo yao.
17
Sitayakumbuka tena makosa yao na mapotovu yao.
18
Basi, hayo yanapoondolewa, hapo hapana tena kutoa kipaji cha tambiko kwa ajili ya ukosaji.
19
*Ndugu, changamko letu la sasa ni hili la kwamba: Tunayo njia inayotuingiza Patakatifu, ni damu ya Yesu;
20
njia hii ni ya siku hizi, tena inatupa uzima; yeye ameifungua hapo, alipopaingia Patakatifu Penyewe, ni hapo, alipoutoa mwili wake.
21
Kwa hiyo tunaye mtambikaji mkuu wa Nyumba ya Mungu.
22
Basi, na tumwendee kwa mioyo yenye kweli, inayojikaza kumtegemea! Kwa hivyo, tulivyonyunyizwa mioyo, isijue tena ubaya, tena kwa hivyo, miili yetu ilivyooshwa kwa maji yatakatayo,
23
na tufulize kukiungama kingojeo chetu, tusichoke! Kwani yeye aliyetupa kiagio chake ni mwelekevu.
24
Tena tuangaliane, tupate kuhimizana, tupendane kwa kufanya matendo mazuri!
25
Kisha tusiache makutano yetu, kama wengine walivyojizoeza, ila tuonyane! Tena tukaze kuonyana kwa hivyo, tunavyoona: Siku ile inakaribia!*
26
Kwani sisi tuliokwisha kuyatambua yaliyo ya kweli tukikosa tena kwa kuyapenda makosa, hakuna kipaji cha tambiko tena kilichotusalia cha kuondoa makosa,
27
ila kinachotusalia ni woga wa kuingoja hukumu na ukali wa moto utakaowala wabishi.
28
Mtu ayatanguaye Maonyo ya Mose huuawa pasipo kuonewa uchungu, akisutwa na mashahidi wawili au watatu.
29
Tena je? Silo lipizi baya kuliko hilo limpasalo mtu, aliyemponda Mwana wa Mungu na kuiwazia damu ya Agano, aliyotakaswa nayo, kwamba: Haifai kitu? Huko siko kumkorofisha Roho aliyemgawia mema?
30
Kwani twamjua aliyesema: Lipizi ni langu mimi, ni mimi nitakayelipisha. Na tena: Bwana atawaamulia walio ukoo wake.
31
Kunatia woga sana kutumbukia mikononi mwa Mungu aliye Mwenye uzima.
32
*Lakini mzikumbuke siku za kwanza, mlipoangazwa! Hapo mlivumilia mapigano mengi mkiteseka.
33
Siku nyingine mkatolewa wenyewe kutazamwa na watu, mkitukanwa pamoja na kuumizwa, siku nyingine mliwatazama wenzenu, wakifanyiziwa hivyo.
34
Kwani wale waliofungwa mliteseka pamoja nao; nanyi mliponyang'anywa, mliyokuwa nayo, mliitikia na kufurahi, kwani mlitambua, ya kuwa mnacho kilimbiko kiyapitacho yale kuwa kizuri, maana hakichakai.
35
Basi, msikitupe kingojeo chenu! Kwani kitawapatia malipo makubwa.
36
Lakini mnapaswa na uvumilivu, myafanye, Mungu ayatakayo, myapokee yale, mliyoagiwa.
37
Kwani pamesalia padogo penyewe, patokee mwenye kuja, hatakawia.
38
Naye mwongofu wangu atapata uzima kwa kunitegemea. Lakini atakayerudi nyuma hataipendeza roho yangu.
39
Lakini sisi hatu wenye kurudi nyuma, tuangamie, ila wenye kumtegemea, tuziokoe roho zetu.*
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 11 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13