bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Hebrews 7
Hebrews 7
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 8 →
1
Kwani huyo Melkisedeki alikuwa mfalme wa Salemu na mtambikaji wa Mungu alioko mbinguni juu. Hapo Aburahamu aliporudi na kutoka katika vita vya wafalme, alimwendea, akampongeza.
2
Naye Aburahamu akamgawia fungu la kumi la mali zote. Maana ya jina lake kwanza ni kwamba: Mfalme wa wongofu; tena ni kwamba: Mfalme wa Salemu, ndio mfalme wa utengemano.
3
Baba yake na mama yake nao wakale wake hawajuliki, wala siku zake za kuishi hazijuliki, zilipoanzia, wala zilipokomea, maana amefananishwa na Mwana wa Mungu, ni mtambikaji wa kale na kale.
4
Lakini tazameni, huyo alivyokuwa, baba yetu mkuu Aburahamu akimpa fungu la kumi la mateka!
5
Kweli nao wana wa Lawi waliopewa utambikaji waliagizwa na Maonyo kuwatoza fungu la kumi wenzao wa ukoo walio ndugu zao, tena ndio waliotoka pamoja nao kiunoni mwa Aburahamu.
6
Lakini yule asiyekuwa wa ukoo wao alimtoza Aburahamu fungu la kumi, akampongeza yule aliyekuwa mwenye kiagio.
7
Lakini hili halibishiki kwamba: Kilicho kidogo hupongezwa nacho kilicho kikubwa.
8
Napo hapo watu walio wenye kufa hutoza fungu la kumi; lakini alilitoza mtu anayeshuhudiwa kwamba: Anaishi.
9
Tena, ikiwezekana kusema hivyo, katika Aburahamu hata Lawi aliye mwenye kutoza fungu la kumi alitozwa naye fungu la kumi.
10
Kwani alikuwa kiunoni mwa babu yake, Melkisedeki alipokutana naye.
11
Kama utambikaji wa Kilawi ungaliyatimiza yote, (kwani hapo, ulipokuwapo, watu walipewa Maonyo), ni kwa sababu gani tena ikisemwa: Sharti painuke mtambikaji mwingine, kama Melkisedeki alivyokuwa, isiposemwa: Kama Haroni alivyokuwa?
12
Kwani utambikaji unapogeuzwa, hapo sharti Maonyo nayo yageuke.
13
Kwani yule aliyesemwa yale maneno alikuwa wa shina jingine, ambalo hakutoka kwake mtu ye yote aliyefanya kazi ya utambikaji.
14
Kwani hujulikana: Bwana wetu alitoka katika shina la Yuda, nalo shina hilo Mose hakuliambia hata neno moja la utambikaji.
15
Tena huelekea kabisa: Pakiinuka mtambikaji mwingine anayefanana na Melkisedeki,
16
yeye utambikaji wake haukutoka kwenye Maonyo yaagizayo mambo ya kimtu, ila umetoka kwenye nguvu ya uzima usiolegezeka.
17
Kwani unashuhudiwa kwamba: Wewe u mtambikaji wa kale na kale, kama Melkisedeki alivyokuwa.
18
Hivyo lile agizo la kale linatanguka, kwa sababu lilikuwa nyonge, tena halikufaa;
19
kwani hakuna lililotimizwa na Maonyo. Lakini mahali pake paliingizwa kingojeo kilicho kikuu kuyapita Maonyo, maana kinatufikisha kwake Mungu.
20
Tena hivi havikufanyika pasipo kiapo: kwani wale wengine waliupata utambikaji pasipo kiapo,
21
lakini huyu aliupata, yeye Mungu akiapa na kujitaja alipomwambia: Bwana aliapa, naye hatajuta: Wewe u mtambikaji wa kale na kale.
22
Hivyo Yesu ni mtimizaji wa agano lililo kuu kulipita lile.
23
Nao wale ni wengi waliokuwa watambikaji, kwa sababu kufa kuliwazuia, wasikae.
24
Lakini huyu anao utambikaji usiopokezanwa, kwa sababu anakaa kale na kale.
25
Kwa hiyo anaweza kuwaokoa kale na kale wanaomjia Mungu na kumfuata yeye; kwani yeye anaishi siku zote, apate kuwaombea.
26
Kwani mtambikaji mkuu, ambaye tunapaswa naye, ni yule mcha Mungu, asiye mwovu, asiye mwenye madoa, aliyetengeka na wakosaji, alioko juu kuliko mbingu.
27
Hapaswi kama wale watambikaji wakuu, kila siku kwanza kujipatia yeye kole ya makosa yake mwenyewe, kisha kuwapatia watu nao kole ya makosa yao. Kwani huyu amevifanya hivyo mara moja hapo alipojitoa mwenyewe kuwa kole.
28
Kwani Maonyo huweka watu wenye unyonge kuwa watambikaji wakuu. Lakini neno la kiapo kilichoyafuata Maonyo nyuma linamweka Mwana kuwa mtambikaji mtimilifu wa kale na kale.
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13