bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Hebrews 3
Hebrews 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 4 →
1
Kwa hiyo, ndugu zangu watakatifu, mlioitwa kama sisi na mwito utokao mbinguni, yaelekezeni macho kwake Yesu, tunayemwungama kuwa mtume na mtambikaji mkuu!
2
Naye aliyempa kazi hiyo alimtumikia kwa welekevu, kama Mose alivyotumika katika nyumba yake yote.
3
Lakini huyu amepaswa kutukuzwa kuliko Mose; ni vivyo hivyo kama vya nyumba; mwenye kuijenga hupata cheo kuliko ile nyumba yenyewe,
4
kwani kila nyumba hujengwa na mtu. Lakini anayevitengeneza vyote ndiye Mungu.
5
Naye Mose alitumika kwa welekevu katika nyumba yake yote kama mtumishi; hivyo aliyashuhudia yale yatakayosemwa.
6
Lakini Kristo alitumika kama mwana aliye mwenye nyumba yake. Nayo nyumba yake ni sisi, tunapoikaza mioyo yetu, ichangamke, tena tunapofuliza kujivunia kingojeo chetu mpaka mwisho.
7
Kwa hiyo fanyeni, kama Roho Mtakatifu anavyosema: Leo, mtakapoisikia sauti yake,
8
msiishupaze mioyo yenu, kama hapo, mioyo ilipokuwa yenye uchungu, siku ile ya kujaribiwa kule nyikani.
9
Ndipo, baba zenu waliponijaribu na kunipima, tena walikuwa wameyaona matendo yangu miaka arobaini.
10
Nikachafuliwa moyo nao wa kizazi hicho, nikasema: Siku zote hupotea njia mioyoni mwao; lakini hawakuzitambua njia zangu.
11
Kwa hiyo nilijiapia kwa makali yangu kwamba: Hawataingia kamwe kwenye kituo changu!
12
Tazameni, ndugu, pasiwe mmoja wenu mwenye moyo mbaya usiomtegemea Mungu, ukijitenga kwake yeye aliye Mwenye uzima!
13
Ila mwonyane wenyewe siku kwa siku, pangali pakiitwa leo, kusudi kwenu kusipatikane mwenye moyo mgumu uliodanganywa na ukosaji!
14
Kwani tumekwisha kuwa wenziwe Kristo, tunapokishika kingojeo chetu cha kwanza, kisitupotelee mpaka mwisho.
15
Paliposemwa: Leo, mtakapoisikia sauti yake, msiishupaze mioyo yenu kama hapo, mioyo ilipokuwa yenye uchungu!
16
Hapo walioyasikia na kupata mioyo yenye uchungu walikuwa akina nani? Sio hao wote waliotoka Misri wakiongozwa na Mose?
17
Tena ni akina nani waliochafua moyo wake miaka 40? Sio hao waliokosa, wao waliokufa nyikani, miili yao ikiachwa hapohapo?
18
Tena ni akina nani, aliowaapia kwamba: Hawataingia kamwe kwenye kituo chake, wasipokuwa wale waliokataa kutii?
19
Nasi twaona, ya kuwa hawakuweza kuingia, kwa sababu hawakumtegemea.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13