bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Hebrews 6
Hebrews 6
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 7 →
1
Kwa hiyo na tuyaache mafundisho ya kwanza ya Kristo, tuendelee kuwafundisha yaliyo ya kutimiza! Tusiweke tena msingi na kuwafundisha kwamba: Juteni mkiyaacha matendo yawauayo! Kisha mtegemeeni Mungu!
2
Tuyaache nayo mafundisho ya ubatizo na ya kubandikiwa mikono na ya ufufuko wa wafu na ya hukumu ya kale na kale!
3
Hayo tutayafuata, Mungu atakapotupa ruhusa.
4
Kwani waliokwisha kuangazwa mioyo na kukionja kipaji kitokacho mbinguni na kugawiwa Roho takatifu
5
na kulionja Neno la Mungu lililo zuri na kuzionja nguvu za siku zitakazokuja,
6
basi, walio hivyo wakitengeka, haiwezekani tena kuwapatia upya, wapate kujuta. Kwani hao humwamba msalabani Mwana wa Mungu mara kwa mara pamoja na kumfyoza, huku ndiko kujiangamiza.
7
Kwani nchi, ikiinywa mvua iinyeayo mara nyingi, huzaa maboga yanayowafalia wailimao, ikichipushwa na Mungu.
8
Lakini ikizaa miiba na mibigili haifai tena, ikafikia kuapizwa, nayo mwisho huteketea.
9
Lakini hata tukisema hivyo, wapendwa, kwa ajili yenu ninyi tumejipa moyo wa kwamba: Yale mema yatupayo wokovu mnayo.
10
Kwani Mungu siye mpotovu, hatayasahau matendo ya upendo wenu, mliyoyatumia ya kulikuza Jina lake na kuwatumikia watakatifu toka kale hata sasa.
11
Lakini twataka sana, kila mmoja wenu ajikaze vivyo hivyo, apate kukishika kingojeo chetu chote kizima mpaka mwisho,
12
msipate kuwa wavivu, ila mwaige wale walio wenye kuvirithi viagio kwa hivyo, walivyovitegemea na kuvumilia.
13
Kwani Mungu alipomwekea Aburahamu kiagio aliapa na kujitaja mwenyewe kwa kukosa aliye mkubwa kumpita, amtaje akiapa.
14
Akasema: Nitakubariki kweli, nikupe kuwa watu wengi sana.
15
Naye alipovumilia akaona, kiagio kilivyotimia.
16
Kwani watu wakiapa hutaja aliye mkubwa kuliko wao, nacho kiapo hukomesha kwao mabishano yote na kulitia nguvu lile neno.
17
Naye Mungu alipotaka sana kuwaonyesha wenye kiagio kwamba: Ayatakayo yeye hayatanguki kamwe, akaapa, wapate kutulia.
18
Akataka, hayo mambo mawili yasiyotanguka kamwe - maana haiwezekani, Mungu aseme uwongo - yatupe matulizo yenye nguvu sisi tuliomkimbilia, tupate kukishika kingojeo chetu, tulichowekewa.
19
Hicho tunakishika, kiwe nanga ya moyo isiyokosa nguvu za kutuliza; nacho ndicho kituingizacho namo mle ndani, tulimopingiwa na lile pazia.
20
Humo ndimo, Yesu alimoingia, atufungulie njia, akawa mtambikaji mkuu wa kale na kale, kama Melkisedeki alivyokuwa.
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 7 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13