bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Hebrews 9
Hebrews 9
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 10 →
1
Nalo Agano la kwanza lilikuwa na maongozi ya kumtambikia Mungu, tena lilikuwa na Patakatifu palipopasa ulimwenguni.
2
Kwani palikuwa pamesimamishwa hema la kuingilia; mwake mlikuwamo taa na meza na mikate aliyowekewa Bwana. Ndipo palipoitwa Patakatifu.
3
Lakini mle ndani mbele ya pazia lililoko katikati mlikuwamo hema lililoitwa Patakatifu Penyewe.
4
Humo mlikuwa na kivukizio cha uvumba cha dhahabu tupu na Sanduku la Agano lililofunikizwa po pote na mabati ya dhahabu; ndani yake mlikuwa na kitungi cha dhahabu chenye Mana na fimbo yake Haroni iliyochipuka na vibao vya Agano.
5
Lakini juu ilikuwa imefunikwa na Makerubi yenye utukufu waliokipatia hicho Kiti cha Upozi kivuli. Hayo yote hatuwezi kuyasema sasa moja moja.
6
Hivi vilipokwisha kutengenezwa hivyo, watambikaji huingia kila siku katika hema la kwanza wakifanya kazi za tambiko.
7
Lakini katika hema la pili humwingia mtambikaji mkuu peke yake kila mwaka mara moja tu, naye hamwingii pasipo damu, anayoipeleka, iwe kole yake yeye na ya makosa ya watu wanaojikosea tu.
8
Hivyo Roho Mtakatifu hueleza kwamba: Njia ya kupaingilia Patakatifu Penyewe haijafunguka siku, hema la kwanza litakapokuwa likingali limesimama bado.
9
Nalo lilikuwa mfano wa kuonyesha, siku hizi za sasa zilivyo: kwani mle watu humpelekea Mungu matoleo na vipaji vya tambiko visivyoweza kumpa mwenye kuvitoa moyo uliotulia wote.
10
Kwani miiko ya kula na ya kunywa nayo maosho mengi ni maongozi ya miili tu, yatufikishe hapo, siku za kuinyosha njia zitakapokutia.
11
*Lakini Kristo alikuja kuwa mtambikaji mkuu wa yale mema yatakayotokea, akapita katika hema lililo kubwa na timilifu kulipita lile lililotengenezwa na mikono ya watu, maana halikufanywa na viumbe vilivyopo nchini.
12
Naye hakupeleka damu za mbuzi na za ndama, ila damu yake mwenyewe, akapaingia nayo Patakatifu Penyewe ile mara moja, akatupatia ukombozi usio na mwisho.
13
Kwani kale damu za mbuzi na za ng'ombe na majivu ya mori aliyechomwa yalinyunyiziwa wenye uchafu, yawatakase, uchafu wa miili uwaondoke;
14
lakini sasa kwa hivyo, Kristo alivyojitoa kwa nguvu ya Roho aliye wa kale na kale kumwia Mungu ng'ombe ya tambiko isiyo na kilema, damu yake itazidi kuing'aza sana mioyo yetu yote, tuyaache matendo yenye kutuua, tupate kumtumikia Mungu aliye mwenye uzima.
15
Kwa sababu hii alikuwa mpatanishi aliyetuletea Agano Jipya kwamba: Walioitwa na waupate urithi wao ulio wa kale na kale, kama walivyoagiwa, kwani kufa kumeoneka kunakokomboa katika makosa yaliyofanyika siku za Agano la kwanza.*
16
Kwani hapo palipo na agano, sharti kwanza mwenye kuliweka afe.
17
Kwani agano hutimizwa na kufa, lakini halina maana kabisa, mwenye kuliweka angali yu hai.
18
Kwa hiyo hata lile la kwanza halikueuliwa pasipo damu.
19
Kwani Mose alipokwisha kuwaambia watu wote kila agizo la maonyo, akachukua damu za ndama na za mbuzi, kisha akachukua na maji na pamba nyekundu na kivumbasi, akakinyunyizia Kitabu chenyewe, kisha nao watu wote,
20
akisema: Hizi ni damu za Agano, Mungu alilowaagizia.
21
Hata hema na vyombo vyote vya kutambikia akavinyunyizia damu vilevile.
22
Nayo Maonyo yaliagiza, vyombo vyote vitakaswe na damudamu, maana pasipo kumwagika damu hakuna ondoleo.
23
Basi, mifano ya vile vilivyoko mbinguni ilipasa kutakaswa hivyo. Lakini vile vya mbinguni vyenyewe vilipaswa na vipaji vya tambiko vilivyo vyenye nguvu kuliko vile.
24
Kwani Kristo hakupaingia Patakatifu palipofanywa na mikono, palipo mfano wa Patakatifu pa kweli, ila aliingia mbinguni kwenyewe, atokee sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu sisi.
25
Lakini hakuingia, ajitoe mara nyingi, kama mtambikaji mkuu anavyopaingia Patakatifu kila mwaka na kupeleka damu isiyo yake.
26
Yeye angalipaswa na kuteswa mara nyingi, kuanzia hapo, ulimwengu ulipoumbwa. Lakini sasa ameonekana mara moja tu, siku zilipotimia, azitangue nguvu za ukosaji na kujitoa kuwa kipaji cha tambiko.
27
Kama inavyowapasa watu, wafe mara moja, kisha wahukumiwe,
28
vivyo naye Kristo ametolewa mara moja, awe kipaji cha tambiko cha kuyaondoa makosa ya watu wengi. Lakini mara ya pili atawatokea pasipo kosa wale wanaomngojea, awaokoe.
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 10 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13