bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Hebrews 12
Hebrews 12
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 13 →
1
*Kwa sababu tuna mashahidi walio wengi hivyo, wanaotuzunguka, kama ni wingu, na tuyatue yote yatulemeayo, tujitenge na makosa yanayoshikamana nasi! Tena katika mashindano, tuliyo nayo, na tukikimbilie kikomo na kuvumilia
2
tukiyaelekeza macho kwake Yesu, maana ndiye aliyetuanzisha kumtegemea, tena ndiye anayetaka kukutimiliza. Yeye akayaacha yaliyoufurahisha moyo wake, akajitwika msalaba, pasipo kuona soni. Kisha akaketi kuumeni penye kiti cha kifalme cha Mungu.
3
Mkumbukeni aliyevumilia alipobishiwa hivyo na wakosaji, msipate kuchoka mioyoni mwenu wala kulegea!
4
Hapo, mnapopigania kushinda makosa, hamjajifikisha kwenye kuuawa na kumwagwa damu.
5
Nanyi mmeyasahau matulizo ya mioyo, aliyotuambia, ya kama tu wana wake kwamba: Mwanangu, usiseme: Si kitu, ukichapwa na Bwana, wala usilegee, unapokanywa naye!
6
Kwani Bwana humchapa anayempenda, naye humpiga kila mwana, anayempokea.*
7
Vumilieni, mwonyeke! Mungu huwatunza kama wanawe. Kwani ni mwana gani, baba yake asiyempiga?
8
Lakini mkiwa hampigwi, kama wote walivyopigwa, basi, ninyi m wana wa kitumwa, ham wana wa kiungwana.
9
Tena, tukiwa tumepigwa na baba zetu waliotuzaa, tukaonyeka, je? Hatutajikaza sana kumtii Baba aliyezizaa roho zetu, tupate kuishi?
10
Kwani wale waliotupiga siku chache, kama walivyowaza wenyewe kuwa vema. Lakini huyo hutupigia yafaayo, tugawiwe naye utakatifu wake.
11
Mapigo yote, yanapokuwapo, hatuyawazii kuwa furaha, ila masikitiko. Lakini siku za nyuma wale waliofundishwa nayo huona, yanavyowazalia matunda yenye utengemano na wongofu.
12
*Kwa hiyo mikono iliyolegea nayo magoti yaliyopooza yatieni nguvu tena!
13
Nayo miguu yenu ishikisheni mapito yaliyo malinganifu! Maana wachechemeao wasipotezwe, ila wapate kupona vema!
14
Kukimbilieni kupatana nao watu wote! Tena ukimbilieni utakaso! Kwani hata mmoja hatammwona Bwana asipokuwa ametakaswa.
15
Angalieni, mtu asiyakose mema, Mungu ayagawiayo! Wala pasichipuke shina lenye uchungu, likiwasumbua na kuchafua wengi!
16
Wala kusionekane mwenye ugoni wala mwenye kumbeza Mungu kama Esau aliyeuuza ukubwa wake kwa chakula kimoja!
17
Kwani mnajua, hapo nyuma, alipotaka kuirithi mbaraka, alitupwa. Kwani hakupata tena penye kujutia, angawa alipatafuta sana kwa machozi.*
18
*Kwani hamkufika penye mlima uliogusika, ukiwaka moto, wala penye wingu jeusi na giza na upepo mkali,
19
wala penye mlio wa baragumu na uvumi wa maneno yaliyowashinda wenye kuyasikia, wakaomba, wasiambiwe tena neno.
20
Kwani hawakuweza kulipokea lile agizo la kwamba: Hata nyama atakayeugusa mlima auawe kwa kupigwa mawe au kwa kuchomwa mikuki.
21
Nayo yaliyoonekana yalikuwa yamewatia woga mkubwa sana, hata Mose akasema, nimeingiwa na kituko, nikatetemeka.
22
Ila mmefika penye mlima wa Sioni, ndipo penye mji wa Mungu Mwenye uzima, ni Yerusalemu ulioko mbinguni, panapo malaika maelfu na maelfu wanaowashangilia
23
wateule waliozaliwa wa kwanza, ndio walioandikwa majina mbinguni. Kisha mmefika penye Mungu aliye mhukumu wa watu wote; ndipo, nazo roho za wenye wongofu waliotimilika zilipo,
24
ndipo, alipo naye Yesu aliyetuletea Agano Jipya, hata damu ya kunyunyizia inayosema na nguvu kuipita ile ya Abeli ipo papo hapo.*
25
Angalieni, msimkataye yeye anayesema! Kwani kama wale waliomkataa, aliposema nao nchini, hawakuweza kukimbia, sisi tutawezaje kukimbia tukijitenga naye, anaposema nasi toka mbinguni?
26
Sauti yake ndiyo iliyoitingisha nchi siku ile; lakini sasa kiko kiagio cha kwamba: Mimi nitatetemesha tena mara moja, si nchi tu, ila hata mbingu.
27
Lakini neno hili la kwamba: Tena mara moja linaeleza, ya kuwa vinavyotingishika hugeuka, kwa kuwa viliumbwa hivyo, kusudi vile visivyotengishika vikae vivyo hivyo.
28
Kwa sababu tumepewa ufalme usiotingishika, na tuyavumishe hayo mema, tuliyogawiwa! Hivyo tutamtambikia Mungu, kama inavyompendeza, tukimcha na kumwogopa.
29
Kwani Mungu wetu ni moto ulao kwa kuteketeza.
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 13 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13