bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Hebrews 8
Hebrews 8
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 9 →
1
Neno lililo kuu katika hayo, tuliyoyasema, ni hili: Tunaye mtambikaji mkuu aliyeketi mbinguni kuumeni kwa kiti cha kifalme chenye ukuu.
2
Naye ni mtunzaji wa Patakatifu na wa Hema lile la kweli, Bwana alilolisimamisha, siye mtu aliyelisimamisha.
3
Kwani kila mtambikaji huwekwa kupeleka matoleo na vipaji vya tambiko. Kwa hiyo hata huyu amepaswa kuwa na kitu cha kumpelekea Mungu.
4
Kama angekuwa ulimwenguni, asingekuwa mtambikaji, maana wako wanaompelekea Mungu vipaji, kama walivyoagizwa.
5
Nao huvitumikia vile vilivyo mfano na kivuli cha vile vilivyoko mbinguni. Ndivyo, Mose naye alivyoagizwa alipotaka kulitengeneza lile hema, kwamba: Angalia, uyafanye yote kwa mfano, ulioonyeshwa mlimani!
6
Lakini sasa huyu amepata utumikizi ulioupita, kwani agano, alilotuletea, ni zuri kuliko lile, tena limeunganishwa na maagizo na viagio vilivyo vizuri navyo kuliko vile.
7
Kwani lile la kwanza kama lingalikuwa pasipo masazo, pasingalitafutwa mahali pa kuwekea la pili.
8
Kwani anawakanya na kuwaambia: Bwana anasema: Mtaona, siku zikija, ndivyo asemavyo Bwana; ndipo, nitakapowatimilizia wao wa mlango wa Isiraeli nao wa mlango wa Yuda Agano Jipya!
9
Halitakuwa, kama Agano lile lilivyokuwa, nililolifanya na baba zao siku ile, nilipowashika mikono, niwatoe katika nchi ya Misri; kwani wao wenyewe hawakulishika Agano langu, nami nikawakataa; ndivyo, asemavyo Bwana.
10
Kwani Bwana asema: Agano, nitakalolifanya nao wa mlango wa Isiraeli, siku hizi zitakapokuwa zimepita, ni hili, asema Bwana: Nitawapa Maonyo yangu, yakae katika mawazo yao, tena nitayaandika mioyoni mwao; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
11
Hawatafundishana tena mtu na mwenziwe wala mtu na ndugu yake kwamba: Mtambue Bwana! Kwani wote watanijua, hivyo walivyo wadogo, mpaka wakiwa wakubwa.
12
Kwani nitawahurumia kwa ajili ya mapotovu yao, nisiyakumbuke tena makosa yao.
13
Agano anapoliita Jipya, lile la kwanza amekwisha kulifanya kukuu. Lakini lililo kukuu na chakavu limefikia kutoweka.
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 9 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13