bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Hebrews 5
Hebrews 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 6 →
1
Kwani kila mtambikaji mkuu anayechaguliwa katika watu huwekwa kwa ajili ya watu, awafanyizie kazi kwake Mungu akimtolea matoleo na vipaji vya tambiko kwa ajili ya makosa yao.
2
Huyu anaweza kuwavumilia kidogo wasiojua maana, wakipotezwa, kwa sababu hata yeye ni mwenye unyonge.
3
Kwa ajili yake huo hana budi kujipatia mwenyewe kole ya makosa yake yeye vivyo hivyo, kama anavyowapatia watu.
4
Wala hakuna ajipaye mwenyewe cheo hiki, ila huitwa na Mungu, kama naye Haroni alivyoitwa.
5
Vivyo naye Kristo hakujipa utukufu mwenyewe kuwa mtambikaji mkuu, ila ni yeye aliyemwambia: Wewe ndiwe Mwanangu, siku hii ya leo mimi nimekuzaa.
6
Ndivyo anavyosema hata pengine: Wewe u mtambikaji wa kale na kale, kama Melkisedeki alivyokuwa.
7
Naye siku zile allikuwapo mwenye mwili wa kimtu, akamwomba na kumbembeleza yule aliyeweza kumwokoa katika kufa. Alipokaza kumlalamikia na kutoa machozi akasikiwa naye, kwa sababu alimcha Mungu.
8
Naye angawa Mwana, lakini katika kuteswa ndimo, alimojifunzia kutii.
9
Tena hapo, mambo yake yalipotimilika, akawapatia wote wamtiio wokovu wa kale na kale.
10
Kwa hiyo alipewa na Mungu jina la mtambikaji mkuu, kama Melkisedeki alivyokuwa.
11
Hapo tunayo maneno mengi ya kusema, lakini ni magumu ya kuyaeleza vema, nanyi mmekuwa wavivu wa kusikia.
12
Kwani tukizipima siku, mlizofundishwa, msingekuwa na budi kuwa wafunzi; lakini mwapaswa, mtu aanze tena kuwafundisha, maneno ya Mungu yalivyoanza; maana yawafaliayo ni maziwa, vyakula vigumu sivyo.
13
Kwani kila anayenyonyeshwa maziwa ni mtu asiyejua bado yaongokayo, kwani ni mtoto mchanga.
14
Lakini walio watu wazima hilishwa vyakula vigumu; kwani hao wameizoeza mioyo yao kujua maana, kwa hiyo hupambanua yaliyo mazuri nayo yaliyo maovu.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13