bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Hebrews 11
Hebrews 11
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 12 →
1
Kumtegemea Mungu ni kuyatumaini, tunayoyangojea, pasipo kuyaonea mashaka yasiyonekana bado.
2
Kwani wakale walishuhudiwa kuwa wenye kumtegemea hivyo.
3
Kwa kumtegemea Mungu twajua, ya kuwa ulimwengu ulitengenezwa kwa Neno lake Mungu, mtu asiseme: Tunavyoviona kwa macho, vilipata kuwapo kwa nguvu yao vile vinavyoonekana.
4
Kwa kumtegemea Mungu Abeli alimtolea Mungu kipaji cha tambiko kilichokuwa kikubwa kuliko chake Kaini, akashuhudiwa nacho kuwa mwongofu, kwani Mungu alipendezwa na vipaji vyake. Naye angawa amekufa, kwa hiyo anasema bado.
5
Kwa kumtegemea Mungu Henoki alichukuliwa, asione kufa. Naye hakuonekana tena, kwa kuwa Mungu alikuwa amemchukua. Naye alipokuwa hajachukuliwa bado, alikuwa ameshuhudiwa, ya kuwa alimpendeza Mungu.
6
Lakini pasipo kumtegemea haiwezekani kumpendeza Mungu. sharti. Kwani atakayemjia Mungu, amtegemee kwamba: Yupo, nao watakaomtafuta huwalipa.
7
Kwa kumtegemea Mungu Noa alionyeshwa mambo yaliyokuwa hayajaonekana bado, naye kwa hivyo, alivyomcha Mungu, akakitengeneza chombo, awaokoe waliokuwamo nyumbani mwake. Ndivyo, alivyouumba ulimwengu, lakini yeye akaurithi wongofu unaopatikana kwa kumtegemea Mungu.
8
Kwa kumtegemea Mungu Aburahamu alitii alipoitwa, ahame, aende mahali, atakapopewa kuwa urithi wake. Akahama, asijue, aendako.
9
Kwa kumtegemea Mungu akawa mgeni katika nchi, aliyoagiwa, kama siyo yake, akakaa katika mahema pamoja na Isaka na Yakobo waliokuwa wenziwe wenye urithi wa kiagio kilekile.
10
Kwani alikuwa akiutazamia mji wenye misingi iliyotengenezwa na kujengwa na Mungu.
11
Kwa kumtegemea Mungu naye Sara alipewa nguvu ya kupata mimba hapo, alipokwisha kuwa mzee; kwani alimwazia yule aliyemwagia hivyo kuwa mwelekevu.
12
Kwa hiyo wale waliozaliwa na yeye mume mmoja aliyekuwa mwenye mwili uliokwisha kufa walikuwa wengi kama nyota za mbinguni na kama mchanga wa ufukoni penye bahari usiohesabika.
13
Hao wote walikufa na kumtegemea Mungu: kwa kuwa hawakuyapata, waliyoagiwa, ila waliyaona, yako mbali bado, wakaenda kuyakutia kule, wakaungama: Nchini tu wageni wanaopita tu.
14
Kwani wenye kusema hivyo wanaonekana kuwa wenye kutafuta nchi ya kutua.
15
Nao kama wangaliikumbuka nchi ile, waliyotoka, wangaliweza kurudi.
16
Lakini sasa wanaitaka nchi iliyo nzuri kuliko ile, nayo iko mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni soni ya kuitwa Mungu wao, kwani aliwatengenezea mji.
17
Kwa kumtegemea Mungu Aburahamu alipojaribiwa alimtoa Isaka, awe ng'ombe ya tambiko, yeye aliyekuwa mwana wake wa pekee.
18
Naye alikuwa amevipokea viagio, alivyowekewa kwamba: Wa Isaka ndio watakaoitwa uzao wako.
19
Alidhani, ya kuwa Mungu anaweza kuamsha mtu hata kwenye wafu. Kwa hiyo alimpata tena papo hapo, alipokwisha kumtoa.
20
Kwa kumtegemea Mungu Isaka alimbariki Yakobo na Esau kwa ajili ya mambo, watakayoyaona.
21
Kwa kumtegemea Mungu Yakobo alipokuwa mwenye kufa aliwaombea mema kila mmoja wao wana wa Yosefu, akawaombea na kuinama, akiiegemea ncha ya mkongojo wake.
22
Kwa kumtegemea Mungu Yosefu alipofikisha kufa alikumbuka, ya kuwa wana wa Isiraeli wataitoka ile nchi, akawaagizia mifupa yake.
23
Kwa hiyo, wazazi wake walivyomtegemea Mungu, Mose alipozaliwa alifichwa nao miezi mitatu; kwa sababu walimwona mtoto kuwa mzuri, hawakuliogopa agizo la mfalme.
24
Kwa kumtegemea Mungu Mose alipokuwa mtu mzima alikataa kuitwa mwana wa binti Farao,
25
akapendezwa kufanyiziwa maovu pamoja na watu wa Mungu, akayakataa mazuri yaliyopatikana kwa kukosa, maana huishia upesi.
26
Kwani alifikiri hivyo: kubezwa kwa kuwa wake Kristo ni kilimbiko kikuacho kuliko mali zote za Misri, maana aliyatazamia malipo ya mwisho.
27
Kwa kumtegemea Mungu akatoka Misri, asiyaogope makali ya mfalme, kwani yeye asiyeonekana alishikamana naye, kama anamwona.
28
Kwa kumtegemea Mungu akaifanya Pasaka na kupaka damu, mwenye kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse.
29
Kwa kumtegemea Mungu wakapita katika Bahari Nyekundu, kama ni nchi kavu, lakini Wamisri walipovijaribu wakatoswa.
30
Kwa hivyo, Waisiraeli walivyomtegemea Mungu, maboma ya Yeriko yakaanguka yalipozungukwa siku saba.
31
Kwa kumtegemea Mungu Rahabu, angawa alikuwa mwanamke mgoni, hakuangamia pamoja na wale wasiotii, maana wale wapelelezi aliwapokea na kuwatuliza mioyo.
32
Nisemeje tena? Kwani saa hazingenitosha, kama ningeyasimulia mambo ya Gideoni na ya Baraka na ya Samusoni na ya Yefuta na ya Dawidi na ya Samweli na ya wafumbuaji.
33
Hao kwa kumtegemea Mungu walipigana na wafalme, wakawashinda, wakaamua kwa wongofu, wakaona, viagio vilivyotimia, wakavifunga vinywa vya simba,
34
wakazima mioto yenye nguvu, wakapona ukali wa panga. Walipokuwa wanyonge walipewa nguvu tena, wakawa wakali vitani, wakakimbiza vikosi vizima vya wageni.
35
Kwa kufufuka kwao, ambao walifiwa nao, wanawake waliwapata tena wao hao, waliofiwa nao. Lakini wengine walipoteswa walitaka kuuawa, wakakataa kukombolewa, wapate ufufuko ulio mzuri uliko huo.
36
Wengine walijaribiwa na kufyozwa pamoja na kupigwa, wengine wakafungwa minyororo, wakatiwa vifungoni.
37
Waliuawa kwa kupigwa mawe, walipondwa, walipasuliwa, walikufa kwa kuchomwa majisu, walifukuzwa po pote, wajiendee wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi tu, wakiwa na njaa, wakiumia kwa maovu, waliyofanyiziwa.
38
Kweli haikuupasa ulimwengu huu kuwa nao, wakatangatanga maporini na milimani na mapangoni na mashimoni ndani ya nchi.
39
Hao wote walipoteseka, ndipo, walipotimiza kumtegemea Mungu, lakini hawakuona, kiagio kilivyotimia.
40
Kwani Mungu alikuwa ametupatia kale kitu kilicho kizuri sana, maana wale wasipate kutimilika pasipo sisi.
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 12 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13