bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Hebrews 4
Hebrews 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 5 →
1
Kwa kuwa kile kiagio cha kuingia kwenye kituo chake kiko bado, na tuogope, pasionekane hata mmoja wenu ajiwaziaye kwamba: Nimekikosa!
2
Kwani nasi tumepigiwa hiyo mbiu njema kama wale. Lakini wale lile neno, waliloambiwa, halikuwafalia, kwani hawakulitegemea, wajiunge nao walisikiao.
3
Maana sisi tumtegemeao Mungu twaingia kwenye kituo kile, kama alivyosema: Kwa hiyo nilijiapia kwa makali yangu kwamba: Hawataingia kamwe kwenye kituo changu! Nazo kazi zake zilikuwa zimekwisha kufanyika hapo, alipokwisha kuumba ulimwengu,
4
kwani pako mahali, alipoisema maana ya siku ya saba kwamba: Siku ya saba Mungu alizipumzikia kazi zake zote.
5
Napo pale alisema: Hawataingia kamwe kwenye kituo changu!
6
Hivyo vinajulika: wako bado watakaokiingia; lakini wale walioanza kupigiwa mbiu yake njema hawakukiingia, kwani walikataa kutii.
7
Miaka ilipokwisha kupita mingi mno, akaweka tena siku, ni hii ya leo, alipomwambia Dawidi, kama alivyosema kale: Leo, mtakapoisikia sauti yake, msiishupaze mioyo yenu!
8
Kwani kama Yosua angalikuwa amewapeleka kwenye kituo, asingalisema siku nyingine iliyoko nyuma bado.
9
*Kwa hiyo twasema: Liko pumziko, watu wa Mungu walilowekewa bado.
10
Kwani aliyeingia kwenye kituo chake, huyo kuzipumzikia kazi zake yeye, kama Mungu alivyozipumzikia kazi zake mwenyewe.
11
Sasa tujihimize kuingia kwenye kituo kile, pasipatikane mtu atakayeangushwa akiyafuata mafunzo yao walewale waliokataa kutii!
12
Kwani neno la Mungu ni lenye uzima na nguvu, tena ni lenye makali kupita ya upanga wenye makali pande mbili. Nalo hupenya, mpaka litenge moyo na roho, nacho kiini na mifupa. Nalo huyaumbua mapenzi na mawazo yaliyomo moyoni.
13
Hakuna kiumbe kiwezacho kujitowesha mbele yake yeye, ila vyote viko uchi na waziwazi machoni pake yeye, naye ndiye, ambaye tunatangaza Neno lake.*
14
Tunaye mtambikaji mkuu kupita wengine aliyepaa mbinguni, ndiye Yesu, Mwana wake Mungu; kwa hiyo na tuyashike, tunayoyaungama!
15
*Kwani hatuna mtambikaji mkuu asiyeteseka pamoja na sisi kwa ajili ya manyonge yetu. Maana naye alijaribiwa katika mambo yote kama sisi, lakini hakukosa.
16
Kwa hiyo twende, tufike pasipo woga penye kiti chake cha kifalme, tutakapogawiwa huruma na upole, tumwone yeye atakayetusaidia hapo, tutakapomtakia!*
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13