bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Hebrews 13
Hebrews 13
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
1
*Kaeni na kupendana kindugu!
2
Msisahau kuwakaribisha wageni! Kwani hivyo wengine walikaribisha malaika, nao wenyewe hawakuwajua.
3
Mwakumbuke waliofungwa, kama m wafungwa wenzao! Mwakumbuke wenye kufanyiziwa maovu! Maana ninyi wenyewe mmo miilini bado.
4
Unyumba sharti uheshimiwe nao wote, hapo penye kitanda chao wanyumba pasifanywe chochote chenye uchafu. Kwani Mungu atawahukumu wagoni na wazinzi.
5
Msiwe wapenda fedha, mtoshewe nayo yaliyo yenu! Kwani yeye mwenyewe anasema: Sitakuacha, wala sitakuepuka.
6
Kwa hiyo sisi hujipa moyo wa kusema: Bwana akiwa ananisaidia, sitaogopa; maana aliye mtu atanifanyia nini?
7
Mwakumbuke waliowaongoza ninyi, waliowaambia Neno la Mungu! Tazameni, walivyotoka ulimwenguni, mviige, walivyomtegemea Mungu!
8
Yesu Kristo alivyokuwa jana na leo, ndivyo, atakavyokuwa kale na kale.
9
Msijipoteze na kujifunza mafundisho mengi yaliyo mageni! Kwani ni vizuri, moyo ukishupaa kwa kugawiwa nguvu, si kwa miiko ya vyakula; kwani waifuatao hawajipatii chochote.*
10
Sisi tunapo petu pa kutolea vipaji vya tambiko, napo ni penye mwiko wa kuvila kwao watambikiao Hemani.
11
Kwani damu za nyama zikiisha kupelekwa Patakatifu na mtambikaji mkuu kwa ajili ya makosa, basi, miili yao hao nyama huteketezwa nje ya kambi.
12
Kwa hiyo hata Yesu aliteswa nje ya mlango wa mji, awatakase watu kwa damu yake mwenyewe
13
Kwa hiyo tumtokee tukitoka kambini na kuvumilia maumivu yenye soni yalinganayo nayo yake!
14
Kwani huku hatuna mji ukaao, ila tunaufuata ule ujao.
15
Tukiwa naye yeye, tumtolee Mungu po pote vipaji vya tambiko vya kumsifu, ndiyo matunda ya midomo iliungamayo Jina lake!
16
Msisahau kutenda mema na kugawiana na wenzenu yaliyo yenu! Kwani vipaji kama hivyo humpendeza Mungu.
17
Wenye kuwaongoza watiini na kuwanyenyekea! Kwani hao huzikeshea roho zenu, maana ndio watakaoulizwa kwa ajili yao, nao hutaka kuzifanya kazi zao kwa furaha pasipo kupiga kite. Kwani hivi haviwafalii kitu ninyi.
18
Tuombeeni sisi! Kwani mioyo yetu hutushuhudia, tuyajuayo kwamba: Twataka kufanya mwenendo mzuri katika mambo yote.
19
Lakini nakaza kuwahimiza, mfanye hivyo, nirudishwe kwenu upesi.
20
Mungu mwenye utengemano aliyemtoa kwenye wafu Bwana wetu Yesu aliye mchungaji mkuu wa kondoo kwa nguvu ya damu ya Agano la kale na kale,
21
yeye Mungu awape nguvu ya kuyafanya mema yote, ayatakayo! Maana yeye ndiye anayetupa kuyafanya yapendezekayo mbele yake, akitushikisha njia yake Yesu Kristo. Huyu na atukuzwe kale na kale pasipo mwisho!
22
Lakini nawahimiza, ndugu, yatieni mioyoni maneno haya ya kuwaonya! Kwani nimewaandikia na kukatakata.
23
Jueni, ya kuwa ndugu yetu Timoteo amefunguliwa! Akija upesi, tutaonana nanyi pamoja na yeye.
24
Nisalimieni wote wawaongozao na watakatifu wote! Nao wenzetu wa Italia wanawasalimu.
25
Upole uwakalie ninyi nyote! Amin.
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13