bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Joshua 15
Joshua 15
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 16 →
1
Shina la wana wa Yuda kura ikalipata nchi za kuzigawanyia koo zao kwenye mpaka wa Edomu; mpaka wao wa kusini uliipita nyika ya Sini iliyokuwa mwisho wa upande wa kusini.
2
Huo mpaka wao wa upande wa kusini ulianzia mwishoni kwa Bahari ya Chumvi kwenye pembe yake ielekeayo kusini.
3
Kutoka kule kusini ulipita hapo pa kukwelea Akarabimu, ulipitia Sini, ulipanda tena upande wa kusini wa Kadesi-Barnea, ulipita Hesironi na kupanda tena Adari, ulizungukia Karka,
4
ulifika Asimoni, kisha ulitokea kwenye mto wa Misri, mwisho ulitokea baharini. Huu ndio mpaka wenu wa kusini.
5
Mpaka wa upande wa maawioni kwa jua ni Bahari ya Chumvi kuufikia mwisho wa Yordani. Nao mpaka wa upande wa kaskazini ulianzia hapo pembeni kwa bahari kwenye mwisho wa Yordani.
6
Kutoka huko mpaka ulipanda Beti-Hogla, ulipitia Beti-Araba upande wake wa kaskazini, kisha mpaka uliupanda mwamba wa Bohani, mwana wa Rubeni.
7
Kutoka Bondeni kwa Akori mpaka ulipanda Debiri, uligeukia kaskazini kufika Gilgali unaoelekea hapo pa kukwelea Adumimu ulioko kusini kwenye kijito; kisha mpaka ulipita penye maji ya Eni-Semesi na kutokea Eni-Rogeli (Chemchemi ya Wafua nguo).
8
Kisha mpaka ulipanda katika bonde la Mwana wa Hinomu kufika kando kwao Wayebusi upande wao wa kusini, ni huko Yerusalemu; kisha mpaka ulipanda kufika juu ya mlima ulioko mbele ya Bonde la Hinomu upande wa baharini mwishoni kwa Bonde la Majitu upande wake wa kaskazini.
9
Toka juu ya mlima huo mpaka uliendelea, ufike kwenye chemchemi ya maji ya Nefutoa, utokee kwenye miji ya mlima wa Efuroni; uliendelea tena kufika Bala, ndio Kiriati-Yearimu.
10
Huko Bala mpaka uligeukia tena upande wa baharini kuufikia mlima wa Seiri, tena ulipita kando ya mlima wa Yearimu upande wake wa kaskazini, ndio Kesaloni; toka huko ulishuka Beti-Semesi, ufike Timuna.
11
Toka huko mpaka uliendelea kando ya Ekroni upande wa kaskazini, kisha uliendelea kufika Sikroni, uliupita mlima wa Bala, utokee Yabuneli, nao mwisho wake mpaka ulikuwa hapo, ulipotokea baharini.
12
Nao mpaka wa upande wa baharini ulikuwa Bahari Kubwa na nchi yake ya pwani. Hii ilikuwa mipaka ya kuzizunguka nchi za wana wa Yuda za kuzigawanyia koo zao.
13
Kalebu, mwana wa Yefune, akampa fungu katikati ya wana wa Yuda, liwe lake kwa hivyo, Bwana alivyomwambia Yosua; ni mji wa Arba, baba yao Waanaki, ndio Heburoni.
14
Huko Kalebu akafukuza wana watatu wa Anaki, Sesai na Ahimani na Talmai, waliozaliwa na Anaki.
15
Toka huko akawaendea wenyeji wa Debiri, nalo jina la Debiri lilikuwa kale Kiriati-Seferi.
16
Hapo Kalebu akasema: Atakayeupiga Kiriati-Seferi na kuuteka nitampa mtoto wangu Akisa kuwa mkewe.
17
Otinieli, mwana wa Kenazi, ndugu yake Kalebu, alipouteka, akampa mtoto wake Akisa kuwa mkewe.
18
Ikawa, huyu alipofikia kwake akamhimiza mumewe kuomba shamba kwa baba yake Kalebu; basi, Akisa aliposhuka katika punda, Kalebu akamwuliza: Unataka nini?
19
Naye akamwambia: Nipe tunzo la kunibariki! Kwa kuwa umenipeleka katika nchi ya kusini, nipe nazo mboji za maji! Ndipo, alipompa zile mboji zilizokuwa upande wa juu, nazo zilizokuwa upande wa chini.
20
Hizi ndizo nchi za shina la wana wa Yuda za kuzigawanyia koo zao, ziwe mafungu yao:
21
kwenye mwisho wa nchi ya shina la wana wa Yuda kuuelekea mpaka wa Edomu upande wa kusini kulikuwa na miji hii: Kabuseli na Ederi na Yaguri,
22
na Kina na Dimona na Adada,
23
na Kedesi na Hasori na Itinani,
24
Zifu na Telemu na Baloti,
25
na Hasori-Hadata na Kerioti-Hesironi, ndio Hasori.
26
Amamu na Sema na Molada,
27
na Hasari-Gada na Hesimoni na Beti-Peleti,
28
na Hasari-Suali na Beri-Seba na Biziotia,
29
Bala na Iyimu na Esemu,
30
na Eltoladi na Kesili na Horma,
31
na Siklagi na Madimana na Sanisana,
32
Lebaoti na Silihimu na Aini na Rimoni; miji hii yote pamoja ni 29 pamoja na mitaa yao.
33
Katika nchi ya tambarare: Estaoli na Sora na Asina,
34
na Zanoa na Eni-Ganimu, Tapua na Enamu,
35
Yarmuti na Adulamu, Soko na Azeka,
36
na Saraimu na Aditaimu na Gedera na Gederotaimu; ni miji 14, pamoja na mitaa yao.
37
Senani na Hadaa na Migidali-Gadi,
38
na Dilani na Misipe na Yokiteli,
39
Lakisi na Boskati na Egloni,
40
na Kaboni na Lamasi na Kitilisi,
41
na Gederoti, Beti-Dagoni na Nama na Makeda; ni miji 16 pamoja na mitaa yao.
42
Libuna na Eteri na Asani,
43
Ifuta na Asina na Nesibu,
44
na Keila na Akizibu na Maresa; ni miji 9 pamoja na mitaa yao.
45
Ekroni na vijiji vyake na mitaa yake.
46
Toka Ekroni upande wa baharini miji yote iliyoko kando ya Asdodi pamoja na mitaa yao.
47
Asdodi na vijiji vyake na mitaa yake, Gaza pamoja na vijiji vyake na mitaa yake mpaka kwenye mto wa Misri, nao mpaka wake ni Bahari Kubwa.
48
Tena milimani: Samiri na Yatiri na Soko,
49
na Dana na Kiriati-Sana, ndio Debiri,
50
na Anabu na Estemo na Animu,
51
na Goseni na Holoni na Gilo; ni miji 11 pamoja na mitaa yao.
52
Arabu na Duma na Esani,
53
Yanumu na Beti-Tapua na Afeka,
54
na Humuta na Kiriati-Arba, ndio Heburoni, na Siori; ni miji 9 pamoja na mitaa yao.
55
Maoni, Karmeli na Zifu na Yuta,
56
na Izireeli na Yokidamu na Zanoa,
57
Kaini, Gibea na Timuna; ni miji 10 pamoja na mitaa yao.
58
Halihuli, Beti-Suri na Gedori,
59
na Marati na Beti-Anoti na Eltekoni; ni miji 6 pamoja na mitaa yao.
60
Kiriati-Baali, ndio Kiriati-Yearimu, na Raba; ni miji 2 pamoja na mitaa yao.
61
Nyikani: Beti-Araba, Midini na Sekaka,
62
na Nibusani na Mji wa Chumvi na Engedi ni miji 6 pamoja na mitaa yao.
63
Lakini Wayebusi, ndio wenyeji wa Yerusalemu, wana wa Yuda hawakuweza kuwafukuza; kwa hiyo Wayebusi wakakaa pamoja na wana wa Yuda mle Yerusalemu mpaka siku hii ya leo.
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 16 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24