bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Isaiah 13
Isaiah 13
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 14 →
1
Kauli ya Mungu dhidi ya Babuloni ambayo Isaya, mwana wa Amozi, alipewa katika maono:
2
Mungu asema: “Twekeni bendera juu ya mlima usio na miti. Wapaazieni sauti askari wapungieni watu mkono waingie malango ya mji wa wakuu.
3
Mimi nimewaamuru wateule wangu, nimewaita mashujaa wangu, hao wenye kunitukuza wakishangilia, waje kutekeleza lengo la hasira yangu.”
4
Sikilizeni kelele milimani kama za kundi kubwa la watu! Sikilizeni kelele za falme, na mataifa yanayokusanyika! Mwenyezi-Mungu wa majeshi analikagua jeshi linalokwenda vitani.
5
Wanakuja kutoka nchi za mbali, wanatoka hata miisho ya dunia: Mwenyezi-Mungu na silaha za hasira yake anakuja kuiangamiza dunia.
6
Lieni maana siku ya Mwenyezi-Mungu imekaribia; inakuja kama maafa kutoka kwa Mungu Mwenye Nguvu.
7
Kwa hiyo mikono ya kila mtu italegea, kila mtu atakufa moyo.
8
Watu watafadhaika, watashikwa na hofu na maumivu, watakuwa na uchungu kama mama anayejifungua. Watatazamana kwa mashaka, nyuso zao zitawaiva kwa haya.
9
Siku ya Mwenyezi-Mungu inakuja, siku kali, ya ghadhabu na hasira kali. Itaifanya nchi kuwa uharibifu, itawaangamiza wenye dhambi wake.
10
Nyota na vilimia vyake angani hazitaangaza; jua linapochomoza litakuwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake.
11
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Nitauadhibu ulimwengu kwa uovu wake, waovu kwa sababu ya makosa yao. Nitakikomesha kiburi cha wenye majivuno, na kuporomosha ubaradhuli wa watu katili.
12
Nitawafanya watu kuwa wachache kuliko dhahabu safi; binadamu watakuwa wachache kuliko dhahabu ya Ofiri.
13
Nitazitetemesha mbingu nayo nchi itatikisika katika misingi yake kwa sababu ya ghadhabu yangu Mwenyezi-Mungu siku ile ya hasira yangu kali.
14
“Kama swala anayewindwa, kama kondoo wasio na mchungaji, kila mmoja atajiunga na watu wake kila mtu atakimbilia nchini mwake.
15
Yeyote atakayeonekana atatumbuliwa, atakayekamatwa atauawa kwa upanga.
16
Watoto wao wachanga watapondwapondwa mbele yao, watanyanganywa nyumba zao, na wake zao watanajisiwa.
17
“Ninawachochea Wamedi dhidi yao; watu ambao hawajali fedha wala hawavutiwi na dhahabu.
18
Mishale yao itawaua vijana, hawatakuwa na huruma kwa watoto, wala kuwahurumia watoto wachanga.
19
Babuloni johari ya falme zote na umaarufu wa kiburi cha Wakaldayo utakuwa kama Sodoma na Gomora, wakati Mungu alipoiangamiza.
20
Kamwe hautakaliwa tena na watu, watu hawataishi humo katika vizazi vyote. Hakuna Mwarabu atakayepiga hema lake humo, wala mchungaji atakayechunga wanyama wake humo.
21
Badala yake watakuwamo wanyama wakali wa porini, bundi watajaa katika nyumba zake. Mbuni wataishi humo, na majini yatachezea humo.
22
Mbwamwitu watalia ndani ya ngome zake, mbweha wataonekana ndani ya nyumba zao za anasa. Wakati wa Babuloni umekaribia, wala siku zake hazitaongezwa.”
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 14 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66