bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Isaiah 40
Isaiah 40
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 39
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 41 →
1
Mungu wenu asema: “Wafarijini watu wangu, nendeni mkawafariji.
2
Semeni na wenyeji wa Yerusalemu kwa upole, waambieni kwamba utumwa wao umekwisha, wamesamehewa uovu wao. Mwenyezi-Mungu amewaadhibu maradufu kwa sababu ya dhambi zao zote.”
3
Sauti ya mtu anaita jangwani: “Mtayarishieni Mwenyezi-Mungu njia, nyosheni barabara kuu kwa ajili ya Mungu wetu.
4
Kila bonde litasawazishwa, kila mlima na kilima vitashushwa; ardhi isiyo sawa itafanywa sawa, mahali pa kuparuza patalainishwa.
5
Kisha utukufu wa Mwenyezi-Mungu utafunuliwa, na watu wote pamoja watauona. Mwenyezi-Mungu mwenyewe ametamka hayo.”
6
Sikiliza! Kuna sauti inasema, “Tangaza!” Nami nikauliza, “Nitangaze nini?” Naye: “Tangaza: Binadamu wote ni kama majani; uthabiti wao ni kama ua la shambani.
7
Majani hunyauka na ua hufifia, Mwenyezi-Mungu avumishapo upepo juu yake. Hakika binadamu ni kama majani.
8
Majani hunyauka na ua hufifia, lakini neno la Mungu wetu ladumu milele.”
9
Nenda juu ya mlima mrefu, ewe Siyoni, ukatangaze habari njema. Paza sauti yako kwa nguvu, ewe Yerusalemu, ukatangaze habari njema. paza sauti yako bila kuogopa. Iambie miji ya Yuda: “Mungu wenu anakuja.”
10
Bwana Mungu anakuja na nguvu, kwa mkono wake anatawala. Zawadi yake iko pamoja naye, na tuzo lake analo.
11
Atalilisha kundi lake kama mchungaji, atawakusanya wanakondoo mikononi mwake, atawabeba kifuani pake, na kondoo wanyonyeshao atawaongoza polepole.
12
Nani awezaye kupima maji ya bahari kwa konzi yake, kuzipima mbingu kwa mikono yake? Nani awezaye kuutia udongo wa dunia kikombeni; kuipima milima kwa mizani au vilima kwa kipimo cha uzani?
13
Nani awezaye kuiongoza akili ya Mwenyezi-Mungu, au kuwa mshauri wake na kumfunza?
14
Mwenyezi-Mungu alimtaka nani shauri, ndipo akapata kuwa mwenye ujuzi? Nani aliyemfunza njia za haki? Nani aliyemfundisha maarifa, na kumwonesha namna ya kuwa na akili?
15
Kwake mataifa ni kama tone la maji katika ndoo, ni kama vumbi juu ya mizani. Kwake visiwa ni vyepesi kama vumbi laini.
16
Kuni zote za Lebanoni na wanyama wake wote havitoshi kwa sadaka ya kuteketezwa mbele yake.
17
Mataifa yote si kitu mbele yake; kwake ni vitu duni kabisa na batili.
18
Mtamlinganisha Mungu na nini basi, au ni kitu gani cha kumfananisha naye?
19
Je, anafanana na kinyago? Hicho, fundi hukichonga, mfua dhahabu akakipaka dhahabu, na kukitengenezea minyororo ya fedha!
20
Au ni sanamu ya mti mgumu? Hiyo ni ukuni mtu anaochagua, akamtafuta fundi stadi, naye akamchongea sanamu imara!
21
Je, nyinyi bado hamjui? Je, hamjapata kusikia? Je, hamkuambiwa tangu mwanzo? Je, hamjafahamu mwanzo wa dunia?
22
Dunia iliumbwa na huyo aketiye juu ya mbingu; kutoka huko wakazi wa dunia ni kama panzi! Yeye amezitandaza mbingu kama pazia, na kuzikunjua kama hema la kuishi.
23
Yeye huwaporomosha wakuu wenye nguvu, watawala wa dunia huwafanya kuwa si kitu.
24
Mara tu wanaposimikwa na kuanza kuota, hata kabla hawajatoa mizizi kama miti udongoni, Mwenyezi-Mungu akiwapulizia hunyauka, kimbunga huwapeperusha kama makapi!
25
Mungu Mtakatifu auliza hivi: “Nani basi, mtakayemlinganisha nami? Je, kuna mtu aliye kama mimi?”
26
Inueni macho yenu juu mbinguni! Je, ni nani aliyeziumba nyota hizo? Ni yule aziongozaye kama jeshi lake, anayeijua idadi yake yote, aziitaye kila moja kwa jina lake. Kwa sababu yeye ni mwenye nguvu nyingi, hakuna hata moja inayokosekana.
27
Enyi watu wa Israeli wazawa wa Yakobo, kwa nini mnalalamika na kusema: “Mwenyezi-Mungu hatujali sisi! Mungu wetu hajali haki yetu!”
28
Je, nyinyi bado hamjui? Je, hamjapata kusikia? Mwenyezi-Mungu ndiye Mungu wa milele; yeye ndiye Muumba wa kila kitu duniani. Yeye hafifii kamwe wala kuishiwa nguvu. Maarifa yake hayachunguziki.
29
Yeye huwapa uwezo walio hafifu, wanyonge huwapa nguvu.
30
Hata vijana watafifia na kulegea; naam, wataanguka kwa uchovu.
31
Lakini wote wanaomtumainia Mwenyezi-Mungu, watapata nguvu mpya. Watapanda juu kwa mabawa kama tai; watakimbia bila kuchoka; watatembea bila kulegea.
← Chapter 39
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 41 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66