bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Isaiah 66
Isaiah 66
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 65
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
1
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Mbingu ni kiti changu cha enzi, dunia ni kiti cha kuwekea miguu yangu. Mtanijengea nyumba ya namna gani basi, Mahali nitakapoweza kupumzika?
2
Mimi mwenyewe nilivifanya vitu hivi vyote, na hivi vyote ni mali yangu. Lakini ninachojali mimi ni mtu mnyenyekevu na mwenye majuto, mtu anayetetemeka asikiapo neno langu.
3
“Lakini watu hawa wanafanya wanavyotaka: Wananitolea tambiko ya ng'ombe na mara wanaua watu kutambikia. Wananitolea sadaka ya mwanakondoo na pia wanamvunja mbwa shingo. Wananitolea tambiko ya nafaka na pia kupeleka damu ya nguruwe. Wanachoma ubani mbele yangu na kwenda kuabudu miungu ya uongo. Hao wamechagua kufuata njia zao wenyewe.
4
Basi, nitawaletea taabu; yatawapata yaleyale wanayoyahofia; maana nilipoita hakuna aliyeitika, niliponena hawakusikiliza. Bali walifanya yaliyo maovu mbele yangu, walichagua yale ambayo hayanipendezi.”
5
Sikilizeni neno la Mwenyezi-Mungu, enyi msikiao neno lake mkatetemeka: “Ndugu zenu ambao wanawachukia, na kuwapiga marufuku kwa sababu yangu, wamesema kwa dharau ‘Mungu na aoneshe utukufu wake, nasi tuwaone nyinyi mkishinda!’ Lakini wao wenyewe ndio watakaoaibishwa!
6
Sikilizeni, ghasia kutoka mjini, sauti kutoka hekaluni! Hiyo ni sauti ya Mwenyezi-Mungu akiwaadhibu maadui zake!
7
“Mji wangu mtakatifu, ni kama mama ajifunguaye bila kuona uchungu; kabla uchungu kuanza, amekwisha zaa mtoto.
8
Ni nani aliyepata kusikia jambo kama hilo? Ni nani aliyewahi kuona jambo kama hilo? Je, nchi nzima yaweza kuzaliwa siku moja? Je, taifa zima laweza kuzaliwa mara moja? Maana Siyoni, mara tu alipoanza kuona uchungu, alijifungua watoto wake.
9
Je, nitawatunza watu wangu mpaka karibu wazaliwe, halafu niwazuie wasizaliwe? Au mimi mwenye kuwajalia watoto, nitafunga kizazi chao? Mimi Mungu wenu nimesema.”
10
Shangilieni na kufurahi pamoja na Yerusalemu enyi mnaoupenda! Shangilieni pamoja nao enyi nyote mlioulilia!
11
Kama mama, Yerusalemu utawanyonyesha, nanyi mtashiba kwa riziki zake; mtakunywa shibe yenu na kufurahi, kutokana na wingi wa fahari yake.
12
Maana Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Nitakuletea fanaka nyingi kama mto, utajiri wa mataifa kama mto uliofurika. Nanyi mtanyonya na kubebwa kama mtoto mchanga, mtabembelezwa kama mtoto magotini mwa mama yake.
13
Kama mama amtulizavyo mwanawe, kadhalika nami nitawatuliza; mtatulizwa mjini Yerusalemu.
14
Mtayaona hayo na mioyo yenu itafurahi; mifupa yenu itapata nguvu kama majani mabichi. Hapo itajulikana kuwa mimi Mwenyezi-Mungu huwalinda watumishi wangu, lakini nikikasirika huwaadhibu maadui zangu.”
15
Mwenyezi-Mungu atakuja kama moto, na magari yake ya vita ni kimbunga. Ataiacha hasira yake ifanye kazi yake kwa ukali, na onyo lake litekelezwe kwa miali ya moto.
16
Mwenyezi-Mungu atatoa hukumu kwa moto, atawaadhibu watu wote kwa upanga; nao atakaowaangamiza watakuwa wengi.
17
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Wapo watu wanaojitakasa na kutawadha wapate kuingia kwenye bustani za ibada za sanamu; wanafanya maandamano na kuhani akiwa kati yao. Watu hao hula nguruwe, panya na vyakula vingine haramu. Watu hao hakika watakufa wote pamoja.
18
Nayajua matendo yao na mawazo yao. Naja kuwakusanya watu wa mataifa yote na lugha zote, wajumuike pamoja na kuuona utukufu wangu.
19
Nitaweka kati yao alama ya uwezo wangu. Watakaosalimika kati yao nitawapeleka kwa watu wa mataifa huko Tarshishi, Puti, Ludi, nchi zenye wapiga upinde stadi; watakwenda pia Tubali na Yowani na nchi ambapo watu hawajapata kusikia umaarufu wangu wala kuuona utukufu wangu. Hao wajumbe wangu watautangaza utukufu wangu katika mataifa hayo.
20
Watawarejesha ndugu zenu wote kutoka katika mataifa yote kama matoleo yangu mimi Mwenyezi-Mungu. Watawaleta wamepanda farasi, nyumbu, ngamia na magari ya farasi mpaka Yerusalemu, kwenye mlima wangu mtakatifu. Watawaleta kama Waisraeli waletavyo sadaka ya nafaka katika chombo safi hadi nyumbani kwangu mimi Mwenyezi-Mungu.
21
Pia nitawachagua baadhi yao kuwa makuhani na baadhi yao kuwa Walawi. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
22
“Kama vile mbingu mpya na dunia mpya nitakazoumba zitakavyodumu milele kwa uwezo wangu, ndivyo wazawa wako na jina lako litakavyodumu.
23
Katika kila sikukuu ya mwezi mpya, na katika kila siku ya Sabato, binadamu wote watakuja kuniabudu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
24
“Kisha watakwenda kuziona maiti za wale walioniasi. Wadudu watakaowala hawatakufa, na moto utakaowachoma hautazimika kamwe. Watakuwa chukizo kwa watu wote.”
← Chapter 65
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66