bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Isaiah 60
Isaiah 60
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 59
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 61 →
1
Inuka ee Siyoni uangaze; maana mwanga unachomoza kwa ajili yako, utukufu wa Mwenyezi-Mungu unakuangaza.
2
Tazama, giza litaifunika dunia, giza nene litayafunika mataifa; lakini wewe, Mwenyezi-Mungu atakuangazia, utukufu wake utaonekana kwako.
3
Mataifa yataujia mwanga wako, wafalme waujia mwanga wa pambazuko lako.
4
Inua macho utazame pande zote; wote wanakusanyika waje kwako. Wanao wa kiume watafika toka mbali, wanao wa kike watabebwa mikononi.
5
Utaona na uso wako utangara, moyo wako utasisimka na kushangilia. Maana utajiri wa bahari utakutiririkia, mali za mataifa zitaletwa kwako.
6
Makundi ya ngamia yataifunika nchi yako, naam, ndama wa ngamia kutoka Midiani na Efa; wote kutoka Sheba watakuja. Watakuletea dhahabu na ubani, wakitangaza sifa za Mwenyezi-Mungu.
7
Makundi ya kondoo wa Kedari yatakusanywa kwako, utaweza kuwatumia kondoo madume wa Nebayothi kuwa kafara; utawatoa kuwa tambiko inayokubalika madhabahuni pa Mungu, naye ataitukuza nyumba yake tukufu.
8
Nani hao wanaopepea kama mawingu, kama njiwa wanaoruka kwenda viotani mwao?
9
Ni meli zitokazo nchi za mbali, zikitanguliwa na meli za Tarshishi. Zinawaleta watoto wako, pamoja na fedha na dhahabu yao, kwa sifa ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, kwa sifa ya Mungu, Mtukufu wa Israeli, maana amewafanya mtukuke.
10
Mwenyezi-Mungu asema: “Wageni watazijenga upya kuta zako, wafalme wao watakutumikia. Maana kwa hasira yangu nilikupiga, lakini kwa fadhili yangu nimekuhurumia.
11
Malango yako yatakuwa wazi daima; usiku na mchana hayatafungwa, ili watu wakuletee utajiri wa mataifa, pamoja na wafalme wao katika maandamano.
12
Kila ufalme au taifa lisilokutumikia litaangamia; mataifa hayo yatatokomezwa kabisa.
13
“Utaletewa fahari ya msitu wa Lebanoni: Mbao za miberoshi, mivinje na misonobari, zitumike kupamba mahali pa maskani yangu; nami nitaparembesha hapo ninapokaa.
14
Wazawa wa wale waliokudhulumu, watakuja na kukuinamia kwa heshima. Wote wale waliokudharau, watasujudu mbele ya miguu yako. Watakuita: ‘Mji wa Mwenyezi-Mungu’, ‘Siyoni, Mji wa Mtakatifu wa Israeli’.
15
“Wewe ulikuwa umeachwa na kuchukiwa, hakuna aliyependa hata kupitia kwako. Lakini sasa nitakufanya uwe na fahari milele, utakuwa mji wa furaha kizazi hata kizazi.
16
Utaletewa chakula na watu wa mataifa, naam, wafalme watakupatia chakula bora. Hapo utatambua kuwa mimi Mwenyezi-Mungu ni Mwokozi wako; mimi Mwenye Nguvu wa Yakobo ni Mkombozi wako.
17
“Badala ya shaba nitakuletea dhahabu, badala ya chuma nitakuletea fedha, badala ya miti, nitakuletea shaba, na badala ya mawe nitakuletea chuma. Amani itatawala juu yako, uadilifu utakuongoza.
18
Ukatili hautasikika tena nchini mwako; wala uharibifu na maangamizi ndani ya mipaka yako. Utaweza kuziita kuta zako: ‘Wokovu’, na malango yako: ‘Sifa’.
19
“Hutahitaji tena jua kukuangazia mchana, wala mwezi kukumulikia usiku; maana mimi Mwenyezi-Mungu ni mwanga wako milele; mimi Mungu wako nitakuwa fahari yako.
20
Mwanga wako mchana hautatua kama jua, wala mwangaza wako usiku kufifia kama mbalamwezi; maana Mwenyezi-Mungu ni mwanga wako milele, nazo siku zako za kuomboleza zitakoma.
21
Watu wako wote watakuwa waadilifu, nao wataimiliki nchi milele. Hao ni chipukizi nililopanda mimi, kazi ya mikono yangu kwa ajili ya utukufu wangu.
22
Aliye mdogo kati yenu atakuwa ukoo, aliye mdogo kuliko wote atakuwa taifa kubwa. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu; wakati ufikapo nitayatekeleza hayo haraka.”
← Chapter 59
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 61 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66