bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Isaiah 17
Isaiah 17
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 18 →
1
Kauli ya Mungu dhidi ya Damasko. “Damasko utakoma kuwa mji; utakuwa rundo la magofu.
2
Mitaa yake imeachwa mahame milele. Itakuwa makao ya makundi ya wanyama, wala hakuna mtu atakayewatisha.
3
Ngome za kujihami za Efraimu zitatoweka, na utawala wa Damasko utakwisha. Waashuru ambao watabaki hai, watakuwa na fedheha kama wazawa wa Israeli. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimenena.
4
“Siku hiyo, fahari ya Yakobo itaporomoshwa, na unono wake ataupoteza.
5
Atakwisha kama shamba lililovunwa, atafanyiwa kama mvunaji avunavyo nafaka, atakuwa kama shamba lililovunwa bondeni Refaimu.
6
Atabakiziwa wachache kama vile baada ya zeituni: Zeituni mbili, tatu katika tawi la juu; nne, tano katika matawi ya mti uzaao sana. Mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nimenena.”
7
Siku hiyo, watu watamwangalia Muumba wao, na kuelekeza macho yao kwa huyo Mtakatifu wa Israeli.
8
Hawatazielekea tena madhabahu ambazo ni kazi za mikono yao wenyewe, wala kuzitazamia tena kazi za mikono yao wenyewe, yaani sanamu za mungu Ashera na madhabahu za kufukizia ubani.
9
Siku hiyo miji yao imara itaachwa mahame, kama miji ambayo Wahivi na Waamori waliihama walipokuwa wakiwakimbia wazawa wa Israeli. Kila kitu kitakuwa uharibifu.
10
Maana wewe Israeli umemsahau Mungu aliyekuokoa, hukumkumbuka Mwamba wa usalama wako. Kwa hiyo, hata mkipanda mimea ya Baali, na kuiweka wakfu kwa mungu wa kigeni;
11
hata mkiifanya ikue siku hiyohiyo mliyoipanda na kuifanya ichanue asubuhi hiyohiyo, mavuno yenu yatatoweka siku hiyo ya balaa na maumivu yasiyoponyeka.
12
Lo! Ngurumo ya watu wengi! Wananguruma kama bahari. Lo! Mlio wa watu wa mataifa! Yanatoa mlio kama wa maji mengi.
13
Mataifa yananguruma kama ngurumo ya maji mengi, lakini Mungu atayakemea, nayo yatakimbilia mbali. Yatafukuzwa kama makapi mlimani mbele ya upepo; kama vumbi litimuliwalo na kimbunga.
14
Wakati wa jioni yanaleta hofu kuu, lakini kabla ya asubuhi yametoweka! Hilo ndilo litakalowapata wanaonyakua mali yetu, ndilo litakalowapata wanaotupora.
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 18 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66