bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Isaiah 14
Isaiah 14
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 15 →
1
Mwenyezi-Mungu atawahurumia tena watu wa Yakobo, atawateua tena Waisraeli. Atawarudisha katika nchi yao wenyewe, na wageni watakuja na kukaa pamoja na watu wa Yakobo.
2
Watu wa mataifa watawasaidia Waisraeli kurudi katika nchi waliyopewa na Mwenyezi-Mungu. Na hapo watawatumikia Waisraeli kama watumwa. Wale waliowateka sasa watatekwa na Waisraeli, na watawatawala wale waliowadhulumu.
3
Ewe Israeli, wakati Mwenyezi-Mungu atakapokufariji baada ya mateso, misukosuko na utumwa uliofanyiwa,
4
utaimba utenzi huu wa kumdhihaki mfalme wa Babuloni: “Jinsi gani mdhalimu alivyokomeshwa! Ujeuri wake umekomeshwa!
5
Mwenyezi-Mungu amelivunja gongo la waovu, ameivunja fimbo ya kifalme ya watawala,
6
ambao walipiga nayo watu kwa hasira bila kukoma, na kuwatawala kwa udhalimu bila huruma.
7
Sasa dunia yote ina utulivu na amani, kila mtu anaimba kwa furaha.
8
Misonobari inafurahia kuanguka kwako, nayo mierezi ya Lebanoni pamoja yasema: ‘Kwa vile sasa umeangushwa, hakuna mkata miti atakayekuja dhidi yetu!’
9
“Kuzimu nako kumechangamka, ili kukulaki wakati utakapokuja. Kunaiamsha mizimu ije kukusalimu na wote waliokuwa wakuu wa dunia; huwaamsha kutoka viti vyao vya enzi wote waliokuwa wafalme wa mataifa.
10
Wote kwa pamoja watakuambia: ‘Nawe pia umedhoofika kama sisi! Umekuwa kama sisi wenyewe!
11
Fahari yako imeteremshwa kuzimu pamoja na muziki wa vinubi vyako. Chini mabuu ndio kitanda chako, na wadudu ndio blanketi lako!’
12
“Jinsi gani ulivyoporomoshwa toka mbinguni, wewe uliyekuwa nyota angavu ya alfajiri. Jinsi gani ulivyoangushwa chini, wewe uliyeyashinda mataifa!
13
Wewe ulijisemea moyoni mwako: ‘Nitapanda mpaka mbinguni; nitaweka kiti changu juu ya nyota za Mungu, nitaketi juu ya mlima wakutanapo miungu, huko mbali pande za kaskazini.
14
Nitapanda vilele vya mawingu nitajifanya kuwa sawa na Mungu Mkuu.’
15
Lakini umeporomoshwa hadi kuzimu; umeshushwa chini kabisa shimoni.
16
“Watakaokuona watakukodolea macho, watakushangaa wakisema: ‘Je, huyu ndiye aliyetetemesha dunia na kuzitikisa falme,
17
aliyegeuza dunia kuwa kama jangwa, akaangamiza miji yake, na kuwanyima wafungwa wake kurudi kwao?’
18
Wafalme wote wa mataifa wamezikwa kwa heshima kila mmoja ndani ya kaburi lake.
19
Lakini wewe umetupwa nje ya kaburi lako; kama mtoto wa kuchukiza aliyezaliwa mfu maiti yako imekanyagwakanyagwa, umerundikiwa maiti za waliouawa kwa upanga, waliotupwa mashimoni penye mawe.
20
Lakini wewe hutaunganishwa nao katika mazishi, maana uliiharibu nchi yako, wewe uliwaua watu wako. Wazawa wa waovu na wasahaulike kabisa!
21
Kaeni tayari kuwachinja watoto wake kwa sababu ya makosa ya baba zao, wasije wakaamka na kuimiliki nchi, na kuijaza dunia yote miji yao.”
22
Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Nitaushambulia mji wa Babuloni na kuuangamiza kabisa. Nitaharibu kila kitu, mji wote, watoto na yeyote aliyebaki hai. Mimi Mwenyezi-Mungu nimenena.
23
Nitaufanya kuwa makao ya nungunungu, na utakuwa madimbwi ya maji. Nami nitaufagilia mbali kwa ufagio wa maangamizi. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimenena.”
24
Mwenyezi-Mungu wa majeshi ameapa: “Kama nilivyopanga, ndivyo itakavyokuwa; kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyokamilika.
25
Nitauvunja uwezo wa Waashuru nchini mwangu; nitawakanyagakanyaga katika milima yangu. Nitawaondolea watu wangu nira ya dhuluma yao, na mzigo wa mateso yao.”
26
Huu ndio uamuzi wake Mwenyezi-Mungu kuhusu dunia yote; hii ndiyo adhabu atakayotoa juu ya mataifa yote.
27
Kama Mwenyezi-Mungu wa majeshi ameamua, nani atakayeweza kubatilisha uamuzi wake? Kama amepania kutoa adhabu, ni nani atakayempinga?
28
Mwaka alipofariki mfalme Ahazi, Mungu alitoa kauli hii:
29
“Msishangilie enyi Wafilisti wote, kwamba Ashuru, fimbo iliyowapiga, imevunjika; maana, nyoka wa kawaida atazaa nyoka mwenye sumu, na nyoka mwenye sumu atazaa joka lirukalo.
30
Wazaliwa wa kwanza wa maskini watashiba, na fukara watakaa kwa usalama. Lakini chipukizi wenu nitawaua kwa njaa; na yeyote wenu atakayebaki nitamuua.
31
Piga yowe ewe lango; lia ewe mji; yeyuka kwa hofu ewe nchi yote ya Filistia. Maana moshi wa askari waja kutoka kaskazini, wala hakuna atakayechelewa katika majeshi yake.”
32
Basi watapewa jibu gani wajumbe wa taifa hilo? Wataambiwa: Mwenyezi-Mungu ameijenga imara Siyoni, na maskini wa watu wake watakimbilia usalama huko.
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 15 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66