bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Isaiah 29
Isaiah 29
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 28
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 30 →
1
Ole wako Yerusalemu, madhabahu ya Mungu; mji ambamo Daudi alipiga kambi yake! Miaka yaja na kupita, na sikukuu zako zaendelea kufanyika;
2
lakini mimi Mungu nitauhuzunisha Yerusalemu, nako kutakuwa na vilio na maombolezo, mji wenyewe utakuwa kama madhabahu iliyolowa damu ya watu waliouawa.
3
Mimi nitapanga jeshi dhidi ya Yerusalemu, nami nitauzingira na kuushambulia.
4
Utaangushwa mbali sana ndani ya ardhi; kutoka huko mbali utatoa sauti; maneno yako yatatoka huko chini mavumbini; sauti yako itatoka ardhini kama ya mzimu.
5
Kundi la maadui zako litakuwa kama vumbi laini, waliokutendea ukatili watakuwa kama makapi. Hayo yatafanyika ghafla.
6
Mwenyezi-Mungu wa majeshi atakuja kukusaidia; atakuja na ngurumo, tetemeko la ardhi na sauti kubwa; atakuja na kimbunga, tufani na moto uunguzao.
7
Hapo, kundi la mataifa yote yanayoshambulia Yerusalemu, wote wanaoshambulia ngome yake na kuutia wasiwasi, watatoweka kama ndoto, kama maono ya usiku.
8
Mataifa yote yanayoushambulia mji wa Yerusalemu yatakuwa kama mtu mwenye njaa anayeota anakula lakini aamkapo bado anaumwa na njaa! Au mtu mwenye kiu anayeota kuwa anakunywa, lakini anaamka mdhaifu, bado ana kiu.
9
Endeleeni kuwa wapumbavu na kuduwaa! Jipofusheni na kuwa vipofu! Leweni lakini si kwa divai; pepesukeni lakini si kwa pombe.
10
Mwenyezi-Mungu amewamiminia hali ya usingizi mzito; ameyafumba macho yenu enyi manabii, amefunika vichwa vyenu enyi waonaji.
11
Basi, kwenu nyinyi maono yote haya ni kama ujumbe ulioandikwa katika kitabu kilichofungwa kwa mhuri. Ukimpelekea mtu yeyote ajuaye kusoma, ukamwambia, “Hebu nisomee kitabu hiki,” atasema, “Siwezi kukisoma kwani kimefungwa kwa mhuri.”
12
Na ukimpa mtu yeyote asiyejua kusoma, ukamwambia, “Hebu nisomee kitabu hiki,” atakuambia, “Sijui kusoma.”
13
Bwana asema, “Watu hawa huja kuniabudu kwa maneno matupu, hali mioyo yao iko mbali nami. Wananiheshimu kulingana na mapokeo ya watu tu, jambo walilojifunza wao wenyewe.
14
Hivyo, nitawatenda tena watu hawa maajabu, mambo ya ajabu na ya kushangaza. Nao wenye hekima wao wataishiwa hekima, na busara ya wenye busara wao itatoweka.
15
“Ole mnaomficha Mwenyezi-Mungu mipango yenu, mnaotenda matendo yenu gizani na kusema: ‘Hamna atakayetuona; nani awezaye kujua tunachofanya?’
16
Nyinyi mnafanya mambo kinyume kabisa! Je, mfinyanzi na udongo ni hali moja? Chombo hakiwezi kumwambia aliyekitengeneza: ‘Wewe hukunitengeneza.’ Kilichofinyangwa hakiwezi kumwambia aliyekiumba, ‘Wewe hujui chochote.’”
17
Bado kidogo tu, msitu wa Lebanoni utageuzwa kuwa shamba lenye rutuba, na shamba lenye rutuba kuwa msitu.
18
Siku hiyo viziwi watasikia ujumbe ukisomwa kitabuni na kutoka gizani vipofu wataanza kuona.
19
Wanyofu watapata furaha mpya kwa Mwenyezi-Mungu, na maskini wa watu watashangilia kwa furaha kwa sababu ya Mungu, Mtakatifu wa Israeli.
20
Majitu makatili yataangamizwa, wenye kumdhihaki Mungu watakwisha, wote wanaootea kutenda maovu watatokomezwa.
21
Watatoweka wale wanaopotosha kesi ya mtu mahakamani, watu wanaowafanyia hila mahakimu na wasemao uongo kuwanyima haki yao wasio na hatia.
22
Kwa hiyo, Mwenyezi-Mungu aliyemkomboa Abrahamu, asema hivi kuhusu wazawa wa Yakobo: “Wazawa wa Yakobo hawataaibishwa tena, hawatainamisha vichwa vyao tena kwa aibu.
23
Watakapowaona watoto wao, watoto niliowajalia mimi mwenyewe, watalitukuza jina langu mimi Mtakatifu wa Yakobo; watakuwa na uchaji kwangu mimi Mungu wa Israeli.
24
Waliopotoka rohoni watapata maarifa na wenye kununa watakubali kufunzwa.”
← Chapter 28
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 30 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66